Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 579
- 887
Hii Ofisi haijali mtu yeyote si Walemavu, wazee wala wagonjwa ni mwendo wa huduma mbovu tu kwa kila aliyeko mbele yao hata uso wa aibu hakuna, Mambo yao ni ya usaniiusanii ahadi za uongo na kutopokea simu, nimehangaishwa humu hadi najiuliza kama kweli kuna uongozi kwenye hii Ofisi unaofuatilia hawa Watumishi waliolewa Mishahara au vipi.
Kwa muda wa miezi mitatu nahangaika na changamoto zangu za Mafao njoo kesho zimekuwa nyingi sana na ukitoka tu Ofisini watumishi waliokuhudumia hawapokei simu hadi urudi tena pale.
Nimefuatilia kwenye simu zao za Customer care tatizo linaonekana liko hapa NSSF Mkoa wa Kinondoni hawatekelezi wajibu wao na ni waongo kwangu, nimepambana kwa miezi mitatu sasa bado inaonekana jitihada zangu za kufanikiwa hapa ni ngumu.
Mwenye uzoefu naomba msaada baada ya kucheleweshewa haki yangu vya kutosha hapa wapi naweza kwenda wanisaidie?