Mshambuliaji wa DC Motema Pembe, Kadima Kabangu amesema anaamini mabingwa watarajiwa wa Tanzania Simba SC watamsaini.
Amesema ameshafanya mazungumzo na kocha wa Simba, Didier Gomes na amemhakikishia yupo kwenye mipango yake kwa ajili ya msimu ujao, Kabangu ana umri wa miaka 27.
Mshambuliaji huyo amewahi kuzichezea timu za Saint Eloi Lupopo, Motema Pembe, Budapest Honved, Shirak ya Armenia, na Maghreb de Fes ya Morroco.
Kati ya vitu vinavyomtambulisha Kabangu awapo uwanjani ni mbio zake, nguvu, na jicho lake la kulenga lango la utopolo na wengine wote atakaokutana nao.
Chanzo: Mwanaspoti & Goal.com