Kadima Kabangu: Nitafunga sana nikicheza Simba

Job Richard

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
3,876
Reaction score
2,190
Kabangu: Nikicheza na Chama, Luis Nitafunga Sana

MSHAMBULIAJI wa DC Motema Pembe ya DR Congo, Kadima Kabangu, amesema ubora walionao viungo wa Simba wakiongozwa na Clatous Chama na Luis Miquissone, utamfanya afunge mabao mengi iwapo atatua ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

Kabangu ndani ya msimu huu wa Ligi kuu ya DR Congo akiwa na Motema Pembe, amefanikiwa kufunga mabao 9 na kutoa asisti 4 katika michezo 16, huku akifanikiwa kufunga mabao 3 katika michezo minne ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mshambuliaji huyo ameweka wazi kuwa tayari amewasiliana na Kocha wa Simba, Didier Gomes kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kabangu alisema: “Simba wana viungo wazuri wa kutengeneza mabao kama Chama, Luis na Bwalya (Rally), hivyo naamini kupitia wao nitafunga mabao mengi sana kama nitafanikiwa kukamilisha usajili wangu wa kujiunga na Simba katika siku zijazo.

“Ligi ya Tanzania nimeifuatilia na bado naendelea kuifuatilia, ni ligi nzuri na yenye ushindani mkubwa, unatakiwa kujituma kila siku ili uweze kufanikiwa kufunga kama ukiwa mshambuliaji, binafsi nimejiandaa kwa kupambana.”

STORI: MARCO MZUMBE, Dar
 
Wachezaji wengi wanaoshindwa kucheza kwenye matimu makubwa kama Olando wakija Bongo wanaheshimika sana kwa vile Ligi yetu haina ubora
Hata hapa bongo wakishindwa Simba wakienda timu zingine wanakua wakali
 
kipindi hiki maknjanja yakishirikiana na mawakala njaa wanauza makanyaboya sana ,kumbuka mwaka jana mkongo anaitwa aziz mpiana mara ikasemakana simba,yanga wanamtaka siku ya mwisho kaenda azam fc ni vituko vitupu sijui hata kama ana goal moja huko...na congo alikuwa mfungaji bora wa tatu sijui
 
Wachezaji wengi wanaoshindwa kucheza kwenye matimu makubwa kama Olando wakija Bongo wanaheshimika sana kwa vile Ligi yetu haina ubora
Mpira hauko hivyo, sanchez katoka arsenal wa moto kaenda kuwa mashuzi tu manchester,mifano ipo kede kede.. Torres alitoka liver wa motooo, chelsea akenda kuwa baridiiii..

Haya mambo yanachangiwa na vitu vingi mnoo, moja wapo ni kocha, mchezaji anaweza kuwa popoma kwa malimu huyu, ila akija mwingine anakuwa moyo balaa.. Wakina victor moses chini ya conte
 
wala usihangaike nao hao ingia you tube mcheki jamaa anaitwa moses phiri hata chipolopolo yuko ndani ndo anakuja huyo, attacking mido la ukweli skills mahala pake goals anafunga kwa sasa ana goals 13 huko kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…