This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,050
- 5,204
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Seminari hizi za kikatoliki hawana habari na mtoto wa maskini.
Nilimpeleka mtoto wa ndugu yangu aliyesoma shule za serikali kufanya interview kwa ajili ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Nilipomfikisha pale seminari nilikutana na mdau na ni mtu wa kanisa/kasisi ambaye nilisoma nae chuo kikuu akiwa mwalimu pale.
Katika maongezi akaniambia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kila darasa lina wanafunzi 110 na ktk wote hao watoto waliosoma Kayumba hawazidi kumi.
Wanachukua watoto wa English Meadium na hizi zinzoitwa Academy.
Na baada ya kufuatilia baadae niligundua kwamba kwa mwaka huu 2024 ambao ndiyo kijana alipaswa kujiunga form one walichukua kijana mmoja tu kutoka kayumba.
Si kwamba hawa vijana hawana uwezo kitaaluma la hasha.
Mdau yule nilimdodosa na kumuuliza kwa nini kupotezea watu muda na rasilimali bila sababu.UKIZINGATIA mchakato wa usaili unaanzia Parokia anayotoka kijana. Pia wanafanya usaili kwenye vikarieti written na oral mara mbili na baada ya hapo ndipo wanaitwa kwenye seminari husika kwa usaili tena na kote huko unalipia.
Jibu alilonipa ni kwamba wanataka wazazi wenye uwezo wa kulipa ada kwa uhakika. Kuchangia harambee mbalimbali zinazoitishwa na mambo mengine mengi.
Kigezo kingine umahiri ktk kuzungumza kiingereza.(Hili nilishangaa kidogo sababu najua kabisa kuongea kiingeeza kunarahisisha ufundishaji lakin kujua kiingereza si kigezo cha uwezo wa kiakili wa mtoto.) Ni vitu viwili tofauti.
Hivyo inaonyesha kadiri miaka inavyosogea hata katika imani tutajikuta tunaongozwa na makasisi kutoka familia za kitajiri na maskini hana chake hata ktk kanisa.
Seminari ninayoizungumzia iko moshi marangu mlimani huko. Ni maarufu sana. Japo siku hizi haivumi sana kama zamani katika rank za kitaifa.