Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, amehoji Bungeni leo Oktoba 28, 2026, kuhusu hatma ya ujenzi wa barabara ya Mgumu–Nata inayoelekea Serengeti, akieleza kuwa inasababisha watalii kukwama wakati wa mvua.
Mbunge huyo amesisitiza kuwa kwa vile Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni kitovu cha utalii nchini, ukamilishwaji wa upembuzi yakinifu na ujenzi wa barabara hiyo ni muhimu sana katika kuongeza pato la taifa na kurahisisha usafiri.
Akijibu swali hilo bungeni leo, Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amesema serikali haiwezi kujenga nchi nzima kwa wakati mmoja, lakini imeweka vipaumbele kwenye barabara zenye umuhimu mkubwa kiuchumi na itafika katika eneo hilo kadiri fedha zitakapopatikana.