Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Acheni kuwa defensive- kazi imewashinda nyie.
 
Na hujuma hizo watakuwa haohao wa juu huko..ishu kama hizi hazituhusu sis maskini
 
Wenye mabasi ya abiria na magari ya mizigo watakuwa hawaupendi kwa kuwa hawatawapiga tena Watanzania kwa gharama za usafirishaji. Shida iliyopo ni kuwa viongozi nao wanamiliki vyombo hivyo vya usafiri sasa sijui nani atamfunga paka kengele.
 
kama taifa, tuungane dhidi ya hao wanaoleta njama, kwa hakika wanataka kuturudisha nyuma, tusikubali. tuwafichue popote walipo, hata kama ni boss wako ingia anonymous mfichue ili tuwashinde.
 
Huyu haeleweki. Basi yeye ndiye anayelihujumu shirika.
Watu wengi walisema hayo yeye akayapinga kabisa.
Alisema kwa sababu ni mradi mpya na unaendeshwa na vijana wa kitanzania bado hawajawa wazoefu sana.

Pili alidiriki kusema wote wanaoongea kuwa ni hujuma ndio mwisho wa upeo wao.

Sasa anaongea vitu gani? Yeye ndio tatizo namba moja.
 
Unakuta mhujumu ni MTU mkubwa ndani ya chama tawala na mchangiaji mkuu wa Hali na Mali wa shughuli za chama, na ana ukwasi unaowazidi akina Kadogosa 19!

Nje ya mada, jina halisi la Abood ni Nani?
Azizi Abood
 
Kutatua matatizo ya hii nchi ni kama kukata tawi ulilokalia mtini🤣! Chanzo kiko kwenye shina la mti ambao ndio umekupa tawi ukalie ila cha ajabu watu wanauogopa sana mti😁!

Wakiwaza kudili na tawi pia wanajikuta wako kwenye sintofahamu maana mtu akilikata atajikuta wapo mavumbini😂. Mti utaendelea kuwepo utazalisha tawi jingine. Anaona bora apige mikwara tu ujumbe ufike ila haisaidii
 
Leo ni wiki sasa hatuwezi kukata Tickets online bado wanasema kuna External Hujuma?
Hawa TRC waache mchezo na Kodi zetu wananchi hio ni Mega Projects, Kadogoso acheze kwanza na watu wake wa ndani mfano hao wa IT ambao ndio wanahusika na Issue za Tickets mambo ya Hujuma kwenye Miundombinu Ni national security issue najua wahusika wako aware
 
Kiongozi anaongea maneno ya kwenye khanga.
Kiongozi unaongeaje upuuzi?
Ushahidi upo peleka police
Ushahidi haupo but unajua hujuma police wapo , tiss wapo pccb wapo omba msaada huko. Media zitakusaidia nini?
Au umeona hutoshi kwenye hiyo nafasi unatafuta kiki!
Haya ndio yale, mpaka Rais analaumu huku yeye ni amiri mkuu
 
Kiongozi anaongea maneno ya kwenye khanga.
Kiongozi unaongeaje upuuzi?
Ushahidi upo peleka police
Ushahidi haupo but unajua hujuma police wapo , tiss wapo pccb wapo omba msaada huko. Media zitakusaidia nini?
Au umeona hutoshi kwenye hiyo nafasi unatafuta kiki!
Haya ndio yale, mpaka Rais analaumu huku yeye ni amiri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…