Habari wadau..
Nimesoma habari kwenye gazeti la the Citizen kwamba kuna mvutano Kati ya Mkurugenzi wa TRC ndugu Kadogosa na Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma yaani PPRA Kuhusu kutoa tenders za ujenzi wa reli vipande vya makutopola Tabora na Tabora Isaka yaani lot 3 na 4.
Kwamba bwana Kadogosa hataki ushindani ufanyike badala yake anataka tender apewe Mturuki yaani kampuni ya Yapi Merkez bila kishindanishwa.
Sababu anazozitoa ni za kipuuzi na zinalengo la kumbeba huyo mkandarasi wake.
Kwa upande wa PPRA wao wanataka sheria ifuate mkondowake kwa kuweka ushindani Ili kupata thamani halisi ya fedha.
Wakaenda mbali zaidi kwa kutoa mfano kwamba kipande cha Isaka Mwanza baada ya ushindani mkandarasi aliyepatokana kampuni ya Kichina ili tender bei ya chini kuliko Yapi Merkez na tofauti ya bei baina yao ilikuwa ni zaidi ya Tilioni 1 na hivyo Serikali kuokoa pesa endapo wangepewa Yapi Merkez bila ushindani.
Sasa inashangaza bwana Kadogosa haoni hili ila anataka bei zake walizokubaliana na Yapi Merkez wapewe bila ushindani Ili apate chake.
Serikali fukizeni huyu mtu hawezi tena kuaminika na huenda anatupiga hata kwenye bei za Lots zilizotangulia.Hawa ndio Mwendazake alikuwa anawaita wazalendo wake,ni hatari sana hii.
Karibuni kwa mjadala. 👇
View attachment 1951944
View attachment 1951945
View attachment 1951946
View attachment 1951947