Uchaguzi 2020 Kadri siku za Kampeni zinavyojongea kufika kiroho changu kinaongezeka kudunda ile mbaya!

Uchaguzi 2020 Kadri siku za Kampeni zinavyojongea kufika kiroho changu kinaongezeka kudunda ile mbaya!

Tila-lila2

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
652
Reaction score
1,058
Acha kabisa!

Watu wanajipanga na hoja maridhawa. Inaonesha kabisa CCM wataula wa chuya kwa kuzuia ile mikutano. Unajua ni kwa nini nasema hivyo?
Ni kwamba watu washaona kuwa kwa muda mrefu wao ni wanyonge hawana nguvu tena wasemee wapi na wasikie kutoka wapi na kwa nani.

Wakati wa Kampeni ule usemi wa Mwanaharakati Voiltaire utaonekana wazi kuwa : "I disapprove of what you say, but I will defend to the death your right to say it". Kampeni zinaenda kuwa wagombea na wnanchi kuongea ambayo walinyimwa kuyaongea kwa takribani miaka minne au mitano sasa. Wanakuja kusikia wakati huu.

Wale vijana waliokuwa na miaka 16 Mwaka 2015 wamekuta hamna uhuru wa kuongea, sasa wanakuja kuuona uhuru huo na pia wameandikishwa kama wapiga kura. Wataona kumbe ukosoaji unaruhusiwa wakati huu. Watabadilishwa na Kampeni. Hawa wamebalehe wakikuta hamna uhuru wa kuongea - sio kosa lao ni kosa la awamu hii.

Ni bora kusemwa semwa siku zote kwani anayekusema unaweza kumgeuza akaonekana ni mwehu kuliko kuja kusemwa siku moja wakati ulishazoea kutokusemwa. Mtachanganyikiwa na kuanza kurusha ngumi.

CCM zikianza Kampeni wajiandae kurusha ngumi. Wakirusha ngumi nchi yetu itazizima na itakuwa kama USA ilivyotokea hivi majuzi. George Floyd kishatuonesha mfano!

Tunasubiri Kampeni zianza kwa hamu sana. Mwaka huu CCM kama sio chali basi mtabanwa kila kona kisawasawa! Na wabunge manaweza msifikishe hata nusu. Muda ni jibu! Tusubiri tuone!
 
Miezi minne kabla ya uchaguzi unasubiri kampeni zianze tu?

Na nani kakwambia CCM inategemea kura kushinda chaguzi?

Unajua kwamba uchaguzi wa 1985 urais Zanzibar, Idris Abdul Wakil alishindwa (uchaguzi wa Ndiyo/Siyo, mgimbea mmoja tu, lakini alishindwa) na bado akapitishwa akawa rais?

CCM ikishindwa na kugeuza matokeo watu watafanya nini? Watajuaje?
 
Miezi minne kabla ya uchaguzi unasubiri kampeni zianze tu?

Na nani kakwambia CCM inategemea kura kushinda chaguzi?

Unajua kwamba uchaguzi wa 1985 urais Zanzibar, Idris Abdul Wakil alishindwa (uchaguzi wa Ndiyo/Siyo, mgimbea mmoja tu, lakini alishindwa) na bado akapitishwa akawa rais?

CCM ikishindwa na kugeuza matokeo watu watafanya nini? Watajuaje?
Mwaka huu hamna kupokwa ushindi. Subiri tuone!
 
Huwa nasema ccm itatangazwa na tume ya uchaguzi ndio washindi, huwa haitegemei kura.

Watu wameshasahau uchaguzi wa serikali za mitaa, ccm ilijitangazia ushindi nchi nzima na hakuna kiluchotokea.

Chaguzi zote zingekuwa chini ya tume ya uchaguzi lakini ule wa serikali za mitaa uko tamisemi, na Jafo akaambiwa hakuna kurudia na akafanya kama alivyoagixwa na mkatulia. Hata huu ujao hakuna jipya.

Mpaka sasa bado mnazuiliwa kufanya kampeni, mnasubiria nini na huu ni mwaka wa uchaguzi?!

Mmesha sahau rufaa ya ma DC kutokusimamia uchaguzi, mko busy na vitu vingine. Hamtatangazwa na mtawekewa mapingamizi ya kijinga na wote mtabaki kulialia.
 
vijana watanzania mabwabwa nyanya munanyanganywa haki zenu munakenua tu mutafanyaje hata kampeni ziwe za matarumbeta kwanza mumeanza kusema hampigi kura hamuwezi kitu nyie waoga kama nini
 
2015 watu walisema hivyo hivyo.

Kilichobadilika ni kipi?
Ulitegemea pandikizi la CCM Lowassa aingize watu mtaani kupinga matokeo????

Ndo mana mwaka huu tunaitaji mtu wa upinzani pure Tundu Antipas Lissu sio pandikizi la CCM Membe kwa sababu ikitokea CCM wakafanya ufilauni TUNDU ANTIPAS LISSU atahamasisha nguvu ya umma na watu tutaingia mtaani kweli
 
Mashine za kupumulia zinatakiwa ziongezwe maana 'bp na shell vyote vitakuwepo'
 
Mkuu

Kuna makosa mengine nimeona ambayo mawe ata-pay dearly,nayo ni:

1.Urais wa Zanzibar,kura za wazanzibar hawamtaki Mwinyi kabisa,refer mgawanyo wa kura kwenye uteuzi uone kwamba,kura za Wazanzibar hata moja haikwenda kwa Mwinyi,na guess what ni the same result kwa wapiga kura wa Zanzibar

2.CCM wa zamani kudharaulika na kunyimwa nafasi na nafasi kupewa wahamiaji.Hasira za hawa watu zitakuja kumtokea Mawe,ndani ya uchaguzi!

3.Ujinga kutegemea nguvu power ya jeshi kumsaidia hiyo october ni shortcut na sio rahisi kama anavyodhani.Hataweza cover kote at once maana nguvu kazi hiyo haipo.Hivyo mambo yataenda kama yalivyo.Wasimamia uchaguzi ili kujiokoa na hasira ya mapanga hawataweza kuiba kura kama wanavyodhani!

Kuiba kura sio kazi ndogo,ukitaka rejea wizi wa Kinondoni juzi,walikufa watu.

October 2020 will be even worse kwa wasimamizi maana watauwawa wasipoangalia!
 
haya yote yangewezekana kama tu Mwenyekiti angebadilishwa na awekwe mtu aggressive na mwenye karba kama J. Heche mbowe ni mwepesi sana ilitakiwa 2015 aingize watu road ila aka kaa kimya huku akirubuniwa na mapandikizi Sumaye na Lowasa
 
vijana watanzania mabwabwa nyanya munanyanganywa haki zenu munakenua tu mutafanyaje hata kampeni ziwe za matarumbeta kwanza mumeanza kusema hampigi kura hamuwezi kitu nyie waoga kama nini
Habari ya mutafanya nini?Angalia Mali kunavyowaka...
 
Hii siyo 2015! Sasa Basi, elewa Hilo neno "SASA BASI!!!"

Subiri halafu muda ukifika ufananishe na 2015
Sasa nimeuliza swali liko wazi, kilichobadilika ni kipi?

Unajibu hii siyo 2015.

Ni kweli, hii siyo 2015. Kwa sasa upinzani umebanwa zaidi, serikali inaendeshwa kibabe zaidi, rais anasema ovyo zaidi, Polisi wanajinadi kuwa ni wa chama tawala wazi zaidi. Yani mambo yamebadilika sana against upinzani.

Sasa kama upinzani ulishindwa kujipanga kuzuia upepo wa mwaka 2015, utaweza kuzuia tsunami ya CCM kutaka kushinda "by hooks and crooks" 2020?

Kama upinzani ulishindwa kuzuia ushindi wa CCM wakati mikutano iliporuhusiwa, na rais alipokuwa muungwana Kikwete, utaweza kuzuia ushindi wa CCM muda huu mikutano imepigwa marufuku na rais ni gubegube barubaru Magufuli?

Yani huu upinzani ulioshindwa kufanya maandamano mwaka wa uchaguzi ndiyo unategemea uweze kumzuia Magufuli na CCM yake kufanya anachotaka?

Kwa kipi cha zaidi?

Mimi siandiki haya kama mtetezi wa CCM au Magufuli, kwa kweli wananichefua sana.

Ila, kama realist, inabidi nikubali ukweli tu.

Ikiwa - nasisitiza neno ikiwa, Magufuli anaweza "kushinda" kihalali kwa muktadha finyu isiwe-, lakini ikiwa Magufuli kashindwa kura, akalazimisha ushindi, upinzani utafanya nini?
 
Wapinzani bwana huwa mnaandika tu theories kibao mitandaoni lakini huko field C CM wanawapiga.

Umemsikia jana Pinda kazi aliyokuwa anaifanya??

Bado mnasafari ndefu sana.
 
Ulitegemea pandikizi la CCM Lowassa aingize watu mtaani kupinga matokeo????

Ndo mana mwaka huu tunaitaji mtu wa upinzani pure Tundu Antipas Lissu sio pandikizi la CCM Membe kwa sababu ikitokea CCM wakafanya ufilauni TUNDU ANTIPAS LISSU atahamasisha nguvu ya umma na watu tutaingia mtaani kweli
Lowassa mbona mnamsingizia tu, kwani mwaka 2000 Lowassa alikuwa CHADEMA?
 
Ukweli ni hata kama ni pandikizi kwa kuwa ataleta kura hamna ubaya wowote!
Falsafa hii iliwaletea matatizo CHADEMA kwa John Shibuda, ikawaletea matatizo kwa Edward Lowassa na itaendelea kuwaletea matatizo tena.
 
Back
Top Bottom