Uchaguzi 2020 Kadri siku za Kampeni zinavyojongea kufika kiroho changu kinaongezeka kudunda ile mbaya!

Uchaguzi 2020 Kadri siku za Kampeni zinavyojongea kufika kiroho changu kinaongezeka kudunda ile mbaya!

Sasa nimeuliza swali liko wazi, kilichobadilika ni kipi?

Unajibu hii siyo 2015.

Ni kweli, hii siyo 2015. Kwa sasa upinzani umebanwa zaidi, serikali inaendeshwa kibabe zaidi, rais anasema ovyo zaidi, Polisi wanajinadi kuwa ni wa chama tawala wazi zaidi. Yani mambo yamebadilika sana against upinzani.

Sasa kama upinzani ulishindwa kujipanga kuzuia upepo wa mwaka 2015, utaweza kuzuia tsunami ya CCM kutaka kushinda "by hooks and crooks" 2020?

Kama upinzani ulishindwa kuzuia ushindi wa CCM wakati mikutano iliporuhusiwa, na rais alipokuwa muungwana Kikwete, utaweza kuzuia ushindi wa CCM muda huu mikutano imepigwa marufuku na rais ni gubegube barubaru Magufuli?

Yani huu upinzani ulioshindwa kufanya maandamano mwaka wa uchaguzi ndiyo unategemea uweze kumzuia Magufuli na CCM yake kufanya anachotaka?

Kwa kipi cha zaidi?

Mimi siandiki haya kama mtetezi wa CCM au Magufuli, kwa kweli wananichefua sana.

Ila, kama realist, inabidi nikubali ukweli tu.

Ikiwa - nasisitiza neno ikiwa, Magufuli anaweza "kushinda" kihalali kwa muktadha finyu isiwe-, lakini ikiwa Magufuli kashindwa kura, akalazimisha ushindi, upinzani utafanya nini?
Huo ndo ukweli hata mimi naamini hivyo upinzani hauwezi ingia Ikulu hata sekunde moja hat Watanzania wote wawape kura ya ndiyo. Bila njia mbadala CCM haiwezi toka madarakani kwa box la kura.
 
Back
Top Bottom