ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Ukimuona mtu wa miaka 35, 40 au 50 anasema mimi hizo club nilishaacha zamani usiamini haraka. Mara nyingi si kwamba hataki kwenda, bali mwili unagoma tu. Mimi tu mwenyewe nina miaka 30 tu, lakini mara nyingi huwa nakaa na madogo fulani wa Myanmar tunakunywa kunywa nao whiskey kuanzia saa 1 hv jioni kufikia saa 4 au 5 mimi tayari macho yanakuwa mazito, mwili umechoka, akili inataka kitanda. Lakini hawa madogo wa under 20 ndiyo wanaanza kupasha moto. Wanaendelea na gitaa, vaping, kucheza pooltable mpaka asubuhi.nikagundua kuwa kadri umri unavyoongezeka, stamina ya kukesha inapungua. Siyo kwamba ghafla unapenda kulala au unachukia starehe. Hapana. Tatizo ni mwili unaanza kudai haki zake. Ukiwa mdogo unaweza kulala saa 10 alfajiri na kuamka saa 12 unaendelea na maisha. so ukiwaona wazee wakisema acha niende nyumbani mapema msidhani wameokoka sana. Wengine mioyoni mwao bado wangependa kubaki kusikia muziki mpaka jogoo awike ila mwili unagoma.