BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,869
- 13,137
Ushawahi kumsikiliza mtu na ikatokea ukasikia kitu ambacho hukutarajia kabisa kukisikia kutoka kwake bila ya kujali ni kizuri au kibaya pengine ulikuwa unamsikiliza mtu ambaye unamheshimu ila ghafla akaongea maneno ambayo yakakufanya uhisi aibu kwa niaba yake na kubaki kutoamini kuwa yametoka kinywani mwake kitu kilichopelekea kupunguza imani na heshima kwake.?
Katika hali ya kawaida binadamu anapenda sana kusikilizwa kwani kupitia kusikilizwa uona kama anapewa thamani, heshima na kujiona mwenye nguvu ya ushawishi dhidi ya wengine ndio maana kwenye mijadala wahusika upambania Kupata nafasi ya kuwasilisha hoja zao huku wakiwa na imani kila mmoja kwa upande wake kuwa asemacho ni bora na kina mantiki kulinganisha na cha mwengine.
Kuna hatari ya mtu kukosa control anapoongea muda mrefu kwa maana ya kuongea vitu visivyo na mantiki au kuongea vitu ambavyo hakupaswa kuviongea kwa wakati uliopo na kwa hadhira iliyopo na ubaya wa kinywa ni kuwa kitu kikishatamkwa hakiwezekani tena kurudishwa mdomoni ndo maana watu wenye hekima ufikiri mara mbili kabla ya kuongea.
Njia nzuri ya kumfahamu mtu mnapokuwa kwenye maongezi ni kumpa fursa ya yeye kuwa muongeaji kwa muda mrefu huku ukionyesha kuwa upo makini na unavutiwa na mazungumzo yake na unapokuwa hujaelewa unauliza maswali katika namna ambayo ni ya kirafiki zaidi niamini mimi Baba Morgan utayasikia yale ambayo hukutarajia kuyasikia kutoka kwa mtu huyo.
Watangazaji wenye uweledi wanafahamu kuhusiana na hili, katika vipindi vya mahojiano vinavyofanywa na mtangazaji anayejua saikolojia ya mwanadamu hususani ya kumpatia mtu fursa kubwa ya kuongea ufanya vipindi vyao kuwa bora na kuibua issues mpya kuhusiana na mhusika, kwa Tanzania yawezekana watangazaji wa namna hii wapo wengi ila kwa haraka haraka naweza mtaja kijana Millard Ayo afanyapo mahojiano anakuwa mtulivu na kumuachia mgeni wake kipaza sauti na uhuru wa kuongea.
Kulianza kuongea sana kukafuatia kuropoka wengi wameponzwa kwa kuwa waongeaji sana kitu kilichopelekea kukosa control kwa kile wasemacho na kuibua sintofahamu na hisia mseto.
Ni vizuri mtu kuwa msikilizaji mzuri kwani kupitia kusikiliza kuna mengi unajifunza na jambo la msingi ni kuwa makini na unachoongea ili kuepuka kuzua hali ya sintofahamu.
Wahanga wakubwa wa hii hali ni watu maarufu sababu ni kusikilizwa na hadhira kubwa yenye watu wa aina tofauti kuanzia wazee mpaka watoto na wanaoishi mijini au vijijini kwa vyovyote vile kisemacho hakitakiwi kuegemea upande wowote wala kudhihaki kundi lolote lile na njia pekee ya kulifanikisha hilo ni kujiandaa na kufikiri kwa kina kabla ya kuongea na kwa usilolijua ni vyema kutoliongelea kabisa.
Speech is silver, silence is golden.