Kaduguda: Simba inasajili wachezaji wa ndondo cup

Kaduguda: Simba inasajili wachezaji wa ndondo cup

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
KADUGUDA: SIMBA INA SAJILI WACHEZAJI WA NDONDO

Mwanachama Mwandamizi wa Simba SC na aliyewahi kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Simba Mhina Kaduguda ametoa maoni yake kuhusiana na namna Uongozi wa Simba SC ulivyopuyanga katika usajili ikiwemo kuwaacha Moses Phiri na Jean Baleke.

“Huwezi kumtoa Baleke, Phiri utuletee Jobe sijui Fred wanasimba wasiwe waoga kusema, hapa uongozi umeteleza hata kama wanataka kwenda nusu fainali au kuchukua ubingwa wa Afrika lakini ndio Center Foward Fred ? midfield Jobe? Sijui Babacar Sarr eeeh jamani?

“Hawa wachezaji hawa, ukienda Tandika, Mwananyamala watoto wa kihuni sisi ambao tumecheza mpira and katika level ndogo mashindano haya ya Ndondo wapo kama utitiri,” Mwina Kaduguda akizungumza katika kipindi cha Michezo na Wapo Radio.

NB: makolo haya mambo ya 10% mtaacha lini?

1710212894584.jpg
 
Asilimia kubwa ya viongozi wa zamani wa makolo wana mapenzi na timu basi tu wakati wa uongozi wao hawakua na financial muscles pamoja na connection/Information kama sasa hivi. Wanaumia sana kwa hiki wanachoona kinaendelea ndio maana yanawatoka maneno yote hayo.
Wanaumia kuona timu yao inaongozwa na makanjanja[emoji23]
 
Hizi kelele zitaongezeka tukitolewa na Al Ahly na kushika nafasi ya pili au ya 3 kwenye msimamo.

Zitajifia kifo cha mende iwapo mambo yatakuwa tofauti na niliyosema hapo juu.
[emoji23][emoji23]
Simba haijawahi ishiwa migawanyiko
 
Timu yetu ya Simba ingekuwa na viongozi aina ya Mwina Kaduguda na Mzee Kilomoni, hakika tusingekuwa tunashiriki haya mashindano ya Ligi ya Mabingwa huku tukiwa siyo Mabingwa kwenye nchi yetu!
Ni aibu sana mkuu [emoji23]
 
Back
Top Bottom