John kaduma(r.i.p) gwiji la michoro afrika mashariki na kati. Yeye mwenyewe akiijita 'fogastar'. Alikuwa moto wa kuotea mbali. Hii ilinifanya nipende kuchora pia. Alichora kiuhalisia, hadithi na michoro yake vilizungumza. Yamkini, alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia hiyo. Palikuwa vilevile, na kina Dikwe ndoto, fortunatus ndilla, willy kisangas, chriss katembo, ibra radi washokera, maggie, N.k. Lakini kaduma kwa maoni yangu aliwakuwa the best. Sijui vipaji hivi vinathaminiwaje, sijui watu hawa wanakumbukwaje, sijui wamenufaikaje pia na vipaji vyao. Wizara yenye dhamana, ina wajibu wa kuwaangalia wasanii wachoraji. Binafsi, nilikuwa najichorea na kutunga kwa ajili ya burudani tu enzi nikiwa primary na secondary. Ifikie pahala, sanaa(fani) iwe ni maisha. Na sio kuburudisha, kuelimisha na kuonya tu. Nakumbuka hadithi zao, murua za Kistoni ninja,pablo zungu , (mchoraji kaduma), mlinzi wa zamu(fortunatus ndilla), pwani yawanyonge(mchoraji chris katembo). Mlikuwa na mchango na hakika kazi zenu mlizifanya kattika mazingira magumu ya teknolojia.