Kaduma alikuwa the best Cartoonist. Hizi kazi zinaweza kuwa animated?

Hakukuwa na mazingira magumu! Bali yale ndio yalikuwa uhalisia wa maisha ya wakati ule.
Ukigundua kiberiti usijidanganye kuwa eti aliyekuwa anapekecha moto alikuwa anapata tabutabu.
 
Pimbi ni bingwa wa kutongoza lakini hajawahi kula mzigo hata siku moja.
 
Sijui nini kilitokea kwa Sani maana badae lilikuja kuibuka jarida la Bongo huko nako kulikua hatari riwaya km Msako wa hayawani; Msako wa Mr.X; Anga za wenyewe;Dunia gunia; zilikua moto wa kuotea mbali
Kwa Sani riwaya ya Ole na Linda ilinisisimua sana!
 
Kama mtu unajua kuchora bila shaka lazima uwatambue hao 'malegends'...
 
Ahahaa.....Jarida la sani lilikuwa noma....ukilinganisha na mingine kama tabasamu
 
Au pambano la Zena na Betina mi nilijua ni kweli wapo Dar hao wadada wawili enzi hizo.
Aisee acha tuu, nakumbuka kipindi hicho tunashindana kuwachora hao cartoon darasani mpaka mwenzetu alipata zawadi kiwilaya,
 
Hii nchi sijui ina laana! Hawa watu kwa kazi walizokuwa wakizifanya ingekuwa ni tunu kubwa sana kwa taifa hili kama wangetaka kuangalia kwa jicho la tatu. Teknolojia ilivyokuwa hivi sisi kwetu inatumika kwenye siasa tu. Upumbavu mkubwa huu, wakati hapa nchini kuna wigo mpana mno wa ajira ila wahusika hawana muda nao, wamekaa kufungia fungia tu kazi za wanaojituma
 
Hii avatar yako inabidi uniundie nami hilo begu jeusi hapo kwangu liwe linachezacheza pia
Hiyo ni mbegu ya mti unaofanana na mnazi unapatikana visiwa vya Shelisheli; Mbegu zinaumbile la kati la mwanamke (love seed)
 
Fortunatus Ndila yuko wapi siku hizi? Nakumbuka alikua na a.k.a yake akijiita mtaalamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…