Kafanya kosa kuoa house girl?

Kafanya kosa kuoa house girl?

Kama nafsi yake inamkubali na anaona ndio sababu tosha kumuoa huyo mdada sio mbaya kwanza ni vizuri sababu watoto wamesha mzowea kama house girl watakua na wakati mgumu kwa mda kubadili kwamba sasa ni MAMA lakini watazowea,ndugu hausiki kwenye hili
akiwa kama mwanamme afanye mamuzi yalo sahihi na isijekua alikua anamrandia ndio mana ndugu wanakata asemekweli...
 
Beware of name calling.............haya majina tunayowapa wasaidizi zimegeuka kuwa label za kuwasakama hawa watu kiasi tunasau msingi wa kwnza wa ubinadamu..........kuwa WOTE TUKO SAWA TU!
 
Juzi nilikwenda mapumziko Tanga baada ya kuchoshwa na shughuli zangu za kikazi za wikii nzima na foleni za hapa Bongo zisizo na tija! Nikiwa TA nilipata wasaa wa kumtembelea kwa mara nyingine rafiki yangu mpendwa ambaye mwaka juzi alifiwa na mkewe.

Kabla ya kufariki kwa mkewe, kaka huyu alikuwa akiishi na mdada wa kazi ambaye ki umri hakupishana kabisa na mkewe. Dada huyu ambaye nilifanikiwa kumuona mara kadhaa kila nimtembeleapo rafiki yangu ni mpole mtaratibu na mwenye tabia njema.

Katika mazungumzo yake, mkuu alinidokeza kuwa ameamua kufunga ndoa na msichana huyu kwa sababu amemsaidia sana tangu mkewe alipofarikia na hata watoto wawili walioachwa na marehemu, amekuwa akiwatunza na kuwahudumia kana kwamba ni watoto wa kuzaa mwenyewe.

Nilipomuuliza kama alikuwa na mahusiano hapo kabla ya mkewe kufariki, alikana kabisa kuwa hakuwahi kufanya hako kamchezo ila kwa sasa focus yake ni nani hasa anafaa kuwatunza watoto wake. Ndugu zake wamekuja juu kupinga uamuzi wake na sasa ameamu kuomba ushauri kutoka kwangu.

Wadau naomba ushauri nimshauri nini kaka huyu.

Wenu,

HP

Mwambie kama mahari haitoshi anitafute.Wandugu mapenzi yanapaswa kuwa na bima (sio nyumba ndogo) kama mnavyokata bima kwa ishu nyingine. Kifupi bima ni kurudisha back to normal situation.Kufa kupo hakuombwi,je umejiuliza mwenzio akitutoka leo nani atashika nafasi? Je si yule unayefahamu kuwa unamuelewa na anakuelewa, potelea mbali hata kama ni huyo hausigeli? Mwambie a-go ahead amuoe huyo binti na ndugu wote wanonko waufyate. Yuko safi kwa yeye, yuko safi kwa watoto, unataka nini tena na hasa kama hizi tabia anashuhudia mwenyewe na si kusimuliwa? TRUE LOVE ,does not count on background. Wewe na rafiki yako mmenikera sana tena sana!
 
Mke mwema ni nani awezaye kumjua? wasifu wa nje inasemekana ni mtaratibu,mstaarabu mpenda na mlezi mzuri wa watoto na hapo mwanzo hakuwahi kutia doa ndoa ya hiyo familia,wakapime waendelee na maisha .Ni heri huyo h/gal mwanamke mwingine atakuwa stranger total kwa watoto na si wote wenye mapenz toka moyoni na watoto wa mume,ila aombe Mungu huyo mdada akizaa wangine asibague wa mwanzo (hiyo ni kwa mwanamke yeyote simaanishi h/gal pekee mara nyingi tunakua na spirit ya selfish)
 
Remember and keep this,

Anayekaribisha ni babu...Kwa hiyo hakuna ubishoo au ushalobaro!!...He will take of you all!!

Wewe ukuje tu....na wambie na wadogo zako pia!
Kheeee...ubishoo kwenye kula babu?Hiyo bado mimi kujaribu.
 
Ni mtihani mgumu. Anahofu watoto kulelewa na mama wa kambo hivyo inampelekea kumuoa house girl kisa kawazoea watoto! Isiwe tatizo kama kweli anampenda HG its fine ila HG apewe nafasi ya kuchagua. Vinginevyo huyo jamaa atafute mwanamke mwingine na HG abakie hapo hapo maana watoto wamemzoea. Aweke wazi kwa huyo mwanamke kuhusu watoto na awe tayari kuishi nao kama wanawe.
 
Hivi Lizzy, DC na Bishanga nini tatizo?

Mie niingie timu ya nani?
 
Back
Top Bottom