Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa

Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kwa mujibu wa simulizi za kidini, ulimwengu umewahi kuadhibiwa mara mbili na mwenyezi Mungu kwa mapigo mawili makubwa.

Pigo la kwanza wakati wa Nuhu, Pigo la gharika hili lilipozwa kwakuwa maji ni uhai na watu walipewa muda wa kujiandaa. Hili ni pigo takatifu lenye nafasi ya uhai ndani yake.

Pigo la pili lilikuwa kwenye miji ya Sodoma na Gomora. Pigo la moto, hili liliteketeza kila kitu watu na mali na viumbe hai. Waliosalimika ni watatu tu Lutu na mabinti zake wawili. Mke wake alivunja sharti la kugeuka nyuma hivyo akawa jiwe la chumvi.

Moto huteketeza vibaya kuliko maji. Shambulio la silaha za nyuklia kule Hiroshima Japan athari zake zinaonekana mpaka kesho.

Kwenye uchawi na ushirikina uchawi wa kuchoma kitu ni hatari na mbaya zaidi ya uchawi wa maji na udongo.

Mwenge wetu wa uhuru ukiachana na sababu zake za kishirikina. Ulifanywa kama alama muhimu ya kukumbukwa na ukawekwa juu ya mlima Kilimanjaro. Kwenye barafu!? Yani ukayeyushe barafu?

Dhana ya kukimbiza huu moto unaoitwa mwenge ni kafara la kutisha lenye tafsiri mbaya kiroho. Hebu fananisha mwenge wa olimpiki na huu wa kwetu.

Moto ule ukimbizwao hufisha, huchoma na kuharibu kabisa fikra yakinifu, mawazo chanya.. Maono ya taifa bora, ujasiri, uthubutu na kujiamini.

Ni kafara la kufanya upande mmoja uendelee kusimama na kutawala wengine. Bila uthubutu dhahiri wa kuhoji ama kuchukua maamuzi magumu. Jamiii huishia kulalama na kulalamika tu kisha husahau na maisha kuendelea.

Siri ya huu moto ukimbizwao inaisha... Hakuna kiongozi wake aliyewahi kumaliza miaka mitano akiwa hai baada ya kuukimbiza nchi nzima.

Mwaka ambao tutashindwa kufanya hili kafara la kukimbiza moto uwakao ndio mwaka taifa litajikomboa na kukombolewa!


Edwin Kagasheki.M

IJUE HISTORIA YA KUANZISHWA KWA MWENGE:

Mnamo miaka ya zamani hizo kabla na baada kidogo ya ukoloni watu waliamini sana katika Mazindiko, Uchawi na Kafara tofauti kidogo na miaka ya hivi leo(miaka ya utandawazi) ambapo watu huyapooza mambo hayo kwa kukemea mila potofu na pengine ni ukiukwawaji wa haki za binadamu. Naam basi tuitizame miaka ya 1900 ambapo walizaliwa watu mashuhuri na baadaye waliitwa "wataalamu" walioweza kusaidiana na viongozi wa nchi yetu kwenye mambo mbalimbali ya kitaifa na waliaminika sana kwenye tawala za ki-chief na jamii kwa ujumla.

Miongoni mwao alikuwepo mtaalamu aliye julikana kwa jina la Forojo Ganze, huyu alizaliwa mwaka 1902 na alikuwa na jopo la wafuasi wake/wazee wenzake wa nyakati hizo ambao walikwenda sambamba na Mwl.Nyerere katika kutoa mchango wao wa kitaalamu kwenye maswala nyeti ya kitaifa.

Forojo Ganze, alikuwa ni mchawi maarufu na ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo, walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani (Mwl.Nyerere) hapingwi na mtu yeyote. Zindiko hilo lilifanyika bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo, na zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake "ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee?".

Basi kiongozi wa msafara Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia kwenye hilo shimo mithili ya pango kwaajili ya kuuliza , alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wazee wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wengine wa Dar es salaam, kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi alikuwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika, wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno haya "Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau ".

Alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho.

Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani, baada ya hapo alimuagiza Yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115, kama kawaida ya Shekhe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "Utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38 ".

Hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na hii ndivyo ilivyokuwa, mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema.
Jiulize, mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa Bukoba ama wa Arusha jambo la kitaifa?
Jibu, Zindiko la bagamoyo linafanya kazi.

Safu iliyoagizwa kufanya zindiko ilikuwa ya watu watano(5) ambao ni.
1: Forojo Ganze mwenyewe,
2: Mzee Ramadhan, aliye zaliwa mwaka 1920,
3: Ally Tarazo, aliye zaliwa mwaka 1929,
4: Komwe wa Komwe, aliye zaliwa mwaka 1918 na
5: Shekhe Yahya Hussein, aliye zaliwa mwaka 1925
 
Kuna siku naangalia MIELEKA namsikia my best perfomer RANDY ORTON anasema "HOLLY HELL" anarudiarudia na watu wanashangilia

Kwangu ndo ilikua mwisho wa kufatilia mieleka, hio haikua sababu pekee ila kuna mambo mengi entertainment industry inatuingiza bila sisi kujua.

Ni mtizamo wangu
Unaruhusiwa kutofautiana nami
 
Tunazoeshwa motoni mkuu ndomana vijana wanasema

"MAMBO NI FIRE" wanaona kama kibwagizo flani NA WANAFURAHIA KABISA, bila kuelewa siri nyuma ya pazia
Mwenge sijaona umuhimu wake zaidi ya ngono zembe, magonjwa ya ngono mimba zisizo tarajiwa.

Umepumbaza watanzania wengi.
Bajeti ya kukimbiza moto nchi nzima ukiijua kwa hakika ni lazima utaona kuna kitu cha ziada
 
Je tafsiri ya kuulinda huu moto kwa kutumia askari wakakamu wenye silaha za moto ni nini?
tapatalk_1558707592899.jpeg
 
huwa natafakari sijawahi kuona faida za huu unaoitwa Mwenge wa Uhuru... mbali na kutafuna hela za walipa kodi.

Nakubaliana na mtoa hoja kwamba yawezekana upo upo kwa sababu za giza.
 
Kwanini mbio za mwenge bado zipo?
By france - April 20, 20160641

mwengeNIKIWA binti mdogo wakati nasoma shule ya msingi miaka ya 1980, nilizoea kusikia na kuimba wimbo mmoja ambao niliupenda sana mpangilio wake wa ala za muziki, na sauti zilizokuwa zikisikika. Huu si wimbo mwingine, bali ni wimbo ambao ulihusu alama kubwa sana ya Taifa letu: Mwenge wa Uhuru.

Wimbo ulikwenda namna hii: “Sisi tumekwisha uwasha Mwenge, tumekwisha uwasha Mwenge. Na kuuweka juu ya mlima, Mlima Kilimanjaro. Kuwasha Mwenge, Kuwasha Mwenge na kuuweka Kilimanjaro; Kuwasha Mwenge, Kuwasha Mwenge na kuuweka Kilimanjaro.”

Naam. Niliupenda mahadhi yake na nakumbuka hata tukiwa sekondari, tulitakiwa kuchangia shilingi tano za mafuta ya taa kwa ajili ya Mwenge huo. Tulijivunia Mwenge huu na tuliaminishwa pia kwamba una maana kubwa sana kwa Taifa letu.

Siku za hivi karibuni, hata hivyo, Watanzania wengi wanaonekana wameuchoka Mwenge. Imefikia hatua kwamba picha zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha Mwenge wa Uhuru na chini yake kukiwa na maneno: Mtumishi hewa namba moja. Picha hiyo imesambazwa sana na kuendelea kusambazwa kwake kunaweza kutafsiriwa kwamba watu wengi wanakubaliana na kauli hiyo ya kuwa kweli alama hii ya Taifa ni mtumishi hewa namba moja.

Wapo pia, nikiwamo mimi, ambao tulidhani kwamba baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, basi angeufutilia mbali Mwenge, kwa maana ya kufuta kabisa hizi mbio za Mwenge ambazo zimekuwa zikifanyika kila mwaka. Huenda wengi wetu tulifikiri hivi kutokana na sababu mbalimbali ambazo zinasababisha tudhani kwamba Mwenge huu wa Uhuru hauna faida.

Bahati nzuri, niliposikia kwamba Mwenge haujafutwa, bado upo na utaendelea kukimbizwa mwaka huu, nikaamua kujiuliza maswali kadhaa. Kwanini hasa mbio hizi za Mwenge wa Uhuru hazijafutwa?

Kwa kuanzia, naomba nitofautishe vitu viwili hapa: Kuna Mwenge wa Uhuru, halafu kuna Mbio za Mwenge wa Uhuru. Ni mambo mawili tofauti. Ili kuelewa tofauti ya mambo haya mawili, nadhani inatupasa kurudi kwenye historia.

Kwa ninavyoelewa, Mwenge wa Uhuru ulianza Disemba 9, 1961, siku ya Uhuru wa Tanganyika. Wakati bendera ya Malkia wa Uingereza ikishushwa Uwanja wa Taifa, bendera ya Tanganyika ilipandishwa, sambamba na Mwenge wa uhuru kuwashwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro. Hiyo inadhihirisha kwamba Mwenge wa Uhuru una maana kubwa sana kwa uhuru wa nchi hii.

Kwa mujibu wa tovuti ya Serikali ya Tanzania, Mwenge wa Uhuru huzunguka nchi nzima ukiwa na ujumbe wa matumaini, upendo, heshima na amani. Mwenge huo huanzia katika mkoa wowote utakaochaguliwa kila mwaka na mbio hizo hufika tamati Oktoba 14, siku ambayo Taifa huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vilevile, tovuti ya Serikali inaongeza kwamba Mwenge huwa na ujumbe tofauti kila mwaka, kulingana na vipaumbele vya maendeleo vya mwaka husika.

Historia pia inatueleza kwamba siku Mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukiwashwa juu ya Mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza, Mwalimu Nyerere alisema maneno yafuatayo: “Tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu; ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini; upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau.”

Mwenge huo uliwekwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na Luteni Kanali, Alexander Nyirenda. Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba Mwenge una umuhimu mkubwa katika kuijenga Tanzania yenye umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa watu wote.

Hiyo ilikuwa Disemba 9, 1961 na tangu mimi nilipokuwa na ufahamu wa kuweza kuwaza mwenyewe, nimekuwa nikisikia kila mwaka kukiwa na mbio za Mwenge. Nadhani lengo lake ni kujikumbusha kuhusu wajibu wetu kama wananchi kuwa na umoja, mshikamano, upendo na amani.

Leo hii, mwaka 2016, wananchi wengi sana wanaonekana hawana imani na mbio za Mwenge. Wana sababu zao za msingi kabisa, ambazo pengine zingefaa kuangaliwa. Sababu moja kubwa ni kwamba mbio za Mwenge zinamaliza tu hela kutokana na Mwenge huo kuwashwa kwa mafuta ya taa. Hela inayotumika kuzunguka nchi nzima ni kubwa sana, pamoja na posho na usafiri kwa wale wakimbiza Mwenge wote.

Sambamba na hilo, ni ukweli usiofichika kwamba Mwenge ukilala kwenye eneo fulani, basi eneo hilo usiku huo kutakuwa na kucheza ngoma usiku kucha, pamoja na vitendo vya wazi kabisa vya zinaa. Ukiwauliza wahudhuriaji, watakueleza kwamba ifikapo asubuhi, kondomu zilizotumika huokotwa kwa wingi na zinaweza kujaza ndoo kadhaa. Ikumbukwe kwamba hizo ni zilizotumika. Kuna uwezekano mkubwa kwamba wapo watu ambao hata hawakutumia kabisa kondomu. Ni alama mbaya sana, kwani mbio za Mwenge wakati mwingine hutumika kama upenyo wa kufanya zinaa isiyo salama.

Lakini vilevile, swali lingine ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza, ni: Hivi kweli wananchi wanafahamu maana na umuhimu wa Mwenge? Sisi tuliokwenda shule miaka ya 80 na 90, kabla ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, tulikuwa tukielezwa sana kuhusu Mwenge na kulazimika kuchangia. Lakini, watoto wetu wanaosoma sasa hivi wanaelewa chochote? Wanafahamu kuhusu historia ya Mwenge na Nyirenda kuuwasha juu ya Mlima Kilimanjaro? Wanajua kuhusu kauli ya amani, upendo, mshikamano na matumaini iliyotolewa na Baba wa Taifa? Wanamfahamu hata huyo Baba wa Taifa na umuhimu wa kuuzima Mwenge Oktoba 14?

Haya ni maswali ambayo nadhani ofisi husika inatakiwa kuyapatia si tu majibu, bali kuyafanyia mkakati ili Taifa lielewe maana ya Mwenge na umuhimu wake.

Hivi, watu wanajua kwamba Mwenge ni alama ya Taifa, na kwamba upo kwenye ngao ile ijulikanayo kama ‘Bibi na Bwana?’ Watu wanaelewa kwamba Mwenge ukifutwa, maana yake ni kwamba unakuwa umefuta historia ya nchi na huenda hata ile ngao ya Taifa itabidi ibadilishwe kwa kuwa imebeba alama za Taifa?

Kila siku nasema, kwanini hatuwi wabunifu? Kwani ni lazima kuukimbiza Mwenge kila mkoa, wilaya na kata kila mwaka? Hakuna njia nyingine mbadala ya kuelimisha watu juu ya Mwenge na maana yake kwa Taifa? Hakuna ubunifu wowote wa kusaidia hata watoto wetu kujua kuna kitu kinaitwa Mwenge wa Uhuru na umuhimu wake kwa Taifa? Ni lazima kukimbia tu kila mwaka? Yaani yale yaliyofanywa miaka ya 70 yaendelee kufanywa hadi leo?

Kama mbio hizi za Mwenge wa Uhuru zipo tu kufuata utaratibu wa kila mwaka bila ya wananchi kukumbushwa umuhimu wake na watoto kufundishwa maana yake, basi hakuna atakayekuwa na kosa atakayeuita Mwenge huo mtumishi hewa namba moja.

Mwisho…


copy n paste...
 
Back
Top Bottom