Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa

Je tafsiri ya kuulinda huu moto kwa kutumia askari wakakamu wenye silaha za moto ni nini? View attachment 1106605

Wewe una agenda zako binafsi..
Mwege upo na utaendelea kuwepo..hizo story zako za gomora/sodoma ni vistory vyamakaburu vyakusadikika..

Mwenge unafaida sawasawa kabisa na hasara zake. Hivyo jifunze kubalance takwimu zako na achana na mifano hewa
 
Yaani umeandika hivi tu na unataka wenye akili wakuamini? Kwa nini mnapenda kudharau akili za members humu ndani? Umekaa ukaandika hiyo figure halafu na sisi tukuunge mkono. Just like that?

Hiyu jamaa ana Upumbavu mwingi kichwani..
Mpuuze tuu..
 
Kuna siku naangalia MIELEKA namsikia my best perfomer RANDY ORTON anasema "HOLLY HELLY" anarudiarudia na watu wanashangilia

Kwangu ndo ilikua mwisho wa kufatilia mieleka, hio haikua sababu pekee ila kuna mambo mengi entertainment industry inatuingiza bila sisi kujua.

Ni mtizamo wangu
Unaruhusiwa kutofautiana nami
WWE ni seat ya shetani. Kwa mfano ikitokea kuna mtu kasign up na wwe utasikia watangazaji wakisema, "he's just signed a deal with the devil himself"

John cena, randy orton, aj styles, bray wyatt etc wote ni occultists. Binafsi nimeacha pia kufuatilia wwe
 
Nimefuatilia sana WWE kuanzia Smackdown, RAW Mpaka zile pigano za Westelmenia...
Hii ni more than Devil's arena guys....
 
Mtoa hoja MOTO pia unatumika hadi leo kiroho.

Kumbuka Yohana Mbatizaji alibatiza kwa Maji huku akisema " Mimi nawabatiza kwa maji ila ajaye baada yangu yeye atawabatiza kwa MOTO."

Roho mtakatifu ni MOTO..
Alikuwa anamzungumzia Jiwe nini 😂😂😂
 
Je tafsiri ya kuulinda huu moto kwa kutumia askari wakakamu wenye silaha za moto ni nini? View attachment 1106605
Kwa mujibu wa maelezo yako ya awali,mimi nahisi/huenda ikawa
Mwenge unaangaza Taifa kupitia Mizimu ya Bagamoyo na ile ya Mlima Kilimanjaro..unapougusa pasipo ridhaa ya mila na desturi ya waliopewa dhamana ya kuukimbiza au kuupokea pia ukijaribu kuufata hadi usawa wa askari "you are shot on spot"
Tambiko lolote ukilivunja gharama yake ni nzito.
NB: Kama Mungu yupo pia Shetani yupo
 
Hivi watu mnaoamini uchawi na madude ya mazindiko mnaishije?
Na iq zenu sijui zikoje..yaani vitu havina logic wala havimake sense na bado mtu anakomaa kuamini..

Maajabu ni kwamba unakuta wanawashangaa wasioamini kama vile wao wana iq kubwa kwamba kina kitu wamegundua kumbe ni delusion tu (ugonjwa wa akili)
 
Sababu mbili tu unafukuzwa kazi Barua inafata baadae kwa watumishi wa Umma ni MWENGE na MITIHANI haoa hakuna mchakato wa nidhamu.

Ndo ujue Mwenge unavyosujudiwa[emoji35][emoji35]
Soma tena ulichoandika, hueleweki!
 
Kwa mujibu wa simulizi za kidini, ulimwengu umewahi kuadhibiwa mara mbili na mwenyezi Mungu kwa mapigo mawili makubwa.

Pigo la kwanza wakati wa Nuhu, Pigo la gharika hili lilipozwa kwakuwa maji ni uhai na watu walipewa muda wa kujiandaa. Hili ni pigo takatifu lenye nafasi ya uhai ndani yake.

Pigo la pili lilikuwa kwenye miji ya Sodoma na Gomora. Pigo la moto, hili liliteketeza kila kitu watu na mali na viumbe hai. Waliosalimika ni watatu tu Lutu na mabinti zake wawili. Mke wake alivunja sharti la kugeuka nyuma hivyo akawa jiwe la chumvi.

Moto huteketeza vibaya kuliko maji. Shambulio la silaha za nyuklia kule Hiroshima Japan athari zake zinaonekana mpaka kesho.

Kwenye uchawi na ushirikina uchawi wa kuchoma kitu ni hatari na mbaya zaidi ya uchawi wa maji na udongo.

Mwenge wetu wa uhuru ukiachana na sababu zake za kishirikina. Ulifanywa kama alama muhimu ya kukumbukwa na ukawekwa juu ya mlima Kilimanjaro. Kwenye barafu!? Yani ukayeyushe barafu?

Dhana ya kukimbiza huu moto unaoitwa mwenge ni kafara la kutisha lenye tafsiri mbaya kiroho. Hebu fananisha mwenge wa olimpiki na huu wa kwetu.

Moto ule ukimbizwao hufisha, huchoma na kuharibu kabisa fikra yakinifu, mawazo chanya.. Maono ya taifa bora, ujasiri, uthubutu na kujiamini.

Ni kafara la kufanya upande mmoja uendelee kusimama na kutawala wengine. Bila uthubutu dhahiri wa kuhoji ama kuchukua maamuzi magumu. Jamiii huishia kulalama na kulalamika tu kisha husahau na maisha kuendelea.

Siri ya huu moto ukimbizwao inaisha... Hakuna kiongozi wake aliyewahi kumaliza miaka mitano akiwa hai baada ya kuukimbiza nchi nzima.

Mwaka ambao tutashindwa kufanya hili kafara la kukimbiza moto uwakao ndio mwaka taifa litajikomboa na kukombolewa!

Edwin Kagasheki.M

IJUE HISTORIA YA KUANZISHWA KWA MWENGE:

Mnamo miaka ya zamani hizo kabla na baada kidogo ya ukoloni watu waliamini sana katika Mazindiko, Uchawi na Kafara tofauti kidogo na miaka ya hivi leo(miaka ya utandawazi) ambapo watu huyapooza mambo hayo kwa kukemea mila potofu na pengine ni ukiukwawaji wa haki za binadamu. Naam basi tuitizame miaka ya 1900 ambapo walizaliwa watu mashuhuri na baadaye waliitwa "wataalamu" walioweza kusaidiana na viongozi wa nchi yetu kwenye mambo mbalimbali ya kitaifa na waliaminika sana kwenye tawala za ki-chief na jamii kwa ujumla.

Miongoni mwao alikuwepo mtaalamu aliye julikana kwa jina la Forojo Ganze, huyu alizaliwa mwaka 1902 na alikuwa na jopo la wafuasi wake/wazee wenzake wa nyakati hizo ambao walikwenda sambamba na Mwl.Nyerere katika kutoa mchango wao wa kitaalamu kwenye maswala nyeti ya kitaifa.

Forojo Ganze, alikuwa ni mchawi maarufu na ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo, walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani (Mwl.Nyerere) hapingwi na mtu yeyote. Zindiko hilo lilifanyika bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo, na zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake "ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee?".

Basi kiongozi wa msafara Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia kwenye hilo shimo mithili ya pango kwaajili ya kuuliza , alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wazee wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wengine wa Dar es salaam, kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi alikuwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika, wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno haya "Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau ".

Alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho.

Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani, baada ya hapo alimuagiza Yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115, kama kawaida ya Shekhe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "Utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38 ".

Hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na hii ndivyo ilivyokuwa, mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema.
Jiulize, mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa Bukoba ama wa Arusha jambo la kitaifa?
Jibu, Zindiko la bagamoyo linafanya kazi.

Safu iliyoagizwa kufanya zindiko ilikuwa ya watu watano(5) ambao ni.
1: Forojo Ganze mwenyewe,
2: Mzee Ramadhan, aliye zaliwa mwaka 1920,
3: Ally Tarazo, aliye zaliwa mwaka 1929,
4: Komwe wa Komwe, aliye zaliwa mwaka 1918 na
5: Shekhe Yahya Hussein, aliye zaliwa mwaka 1925
Hata malikia wa ana mwenge wake,ambao huwa unakimbizwa mataifa yote ya jumuiya ya madola.
Lengo la kuanzishwa kwa mwenge ni zuri,ni la kihistoria.Kuna mapungufu kidogo katika ukimbizwaji mwenge,matumizi ya pesa nyingi,ngono zembe,yakiboreshwa bado ni jambo zuri.
Sio lazima tuache kila kitu chetu,kwa vile tu wakubwa wetu wazungu hawafanyi.
Umeishawahi kujiuliza Familia ya kifalme ya UK inafaida gani kwa nchi yao.?wanatunzwa na kodi za wananchi,hata wasipofsnya kazi,watakula bule mpaka wave,lakini kitendo cha kusema tuondoe ufalme,utaonekana wewe ni muhaini kule UK.
Tutunze vyetu tuviboreshe,tusibeze kila kitu,tuhoji,na tuje na njia mbadala ya kufanya mambo,sisi ni weusi,abadani hatuwezi kuwa wazungu,hata tuongee English kama royal family members.
 
Kwa mujibu wa simulizi za kidini, ulimwengu umewahi kuadhibiwa mara mbili na mwenyezi Mungu kwa mapigo mawili makubwa.

Pigo la kwanza wakati wa Nuhu, Pigo la gharika hili lilipozwa kwakuwa maji ni uhai na watu walipewa muda wa kujiandaa. Hili ni pigo takatifu lenye nafasi ya uhai ndani yake.

Pigo la pili lilikuwa kwenye miji ya Sodoma na Gomora. Pigo la moto, hili liliteketeza kila kitu watu na mali na viumbe hai. Waliosalimika ni watatu tu Lutu na mabinti zake wawili. Mke wake alivunja sharti la kugeuka nyuma hivyo akawa jiwe la chumvi.

Moto huteketeza vibaya kuliko maji. Shambulio la silaha za nyuklia kule Hiroshima Japan athari zake zinaonekana mpaka kesho.

Kwenye uchawi na ushirikina uchawi wa kuchoma kitu ni hatari na mbaya zaidi ya uchawi wa maji na udongo.

Mwenge wetu wa uhuru ukiachana na sababu zake za kishirikina. Ulifanywa kama alama muhimu ya kukumbukwa na ukawekwa juu ya mlima Kilimanjaro. Kwenye barafu!? Yani ukayeyushe barafu?

Dhana ya kukimbiza huu moto unaoitwa mwenge ni kafara la kutisha lenye tafsiri mbaya kiroho. Hebu fananisha mwenge wa olimpiki na huu wa kwetu.

Moto ule ukimbizwao hufisha, huchoma na kuharibu kabisa fikra yakinifu, mawazo chanya.. Maono ya taifa bora, ujasiri, uthubutu na kujiamini.

Ni kafara la kufanya upande mmoja uendelee kusimama na kutawala wengine. Bila uthubutu dhahiri wa kuhoji ama kuchukua maamuzi magumu. Jamiii huishia kulalama na kulalamika tu kisha husahau na maisha kuendelea.

Siri ya huu moto ukimbizwao inaisha... Hakuna kiongozi wake aliyewahi kumaliza miaka mitano akiwa hai baada ya kuukimbiza nchi nzima.

Mwaka ambao tutashindwa kufanya hili kafara la kukimbiza moto uwakao ndio mwaka taifa litajikomboa na kukombolewa!

Edwin Kagasheki.M

IJUE HISTORIA YA KUANZISHWA KWA MWENGE:

Mnamo miaka ya zamani hizo kabla na baada kidogo ya ukoloni watu waliamini sana katika Mazindiko, Uchawi na Kafara tofauti kidogo na miaka ya hivi leo(miaka ya utandawazi) ambapo watu huyapooza mambo hayo kwa kukemea mila potofu na pengine ni ukiukwawaji wa haki za binadamu. Naam basi tuitizame miaka ya 1900 ambapo walizaliwa watu mashuhuri na baadaye waliitwa "wataalamu" walioweza kusaidiana na viongozi wa nchi yetu kwenye mambo mbalimbali ya kitaifa na waliaminika sana kwenye tawala za ki-chief na jamii kwa ujumla.

Miongoni mwao alikuwepo mtaalamu aliye julikana kwa jina la Forojo Ganze, huyu alizaliwa mwaka 1902 na alikuwa na jopo la wafuasi wake/wazee wenzake wa nyakati hizo ambao walikwenda sambamba na Mwl.Nyerere katika kutoa mchango wao wa kitaalamu kwenye maswala nyeti ya kitaifa.

Forojo Ganze, alikuwa ni mchawi maarufu na ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo, walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani (Mwl.Nyerere) hapingwi na mtu yeyote. Zindiko hilo lilifanyika bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo, na zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake "ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee?".

Basi kiongozi wa msafara Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia kwenye hilo shimo mithili ya pango kwaajili ya kuuliza , alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wazee wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wengine wa Dar es salaam, kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi alikuwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika, wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno haya "Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau ".

Alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho.

Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani, baada ya hapo alimuagiza Yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115, kama kawaida ya Shekhe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "Utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38 ".

Hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na hii ndivyo ilivyokuwa, mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema.
Jiulize, mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa Bukoba ama wa Arusha jambo la kitaifa?
Jibu, Zindiko la bagamoyo linafanya kazi.

Safu iliyoagizwa kufanya zindiko ilikuwa ya watu watano(5) ambao ni.
1: Forojo Ganze mwenyewe,
2: Mzee Ramadhan, aliye zaliwa mwaka 1920,
3: Ally Tarazo, aliye zaliwa mwaka 1929,
4: Komwe wa Komwe, aliye zaliwa mwaka 1918 na
5: Shekhe Yahya Hussein, aliye zaliwa mwaka 1925
Mkuu tukumbushe mazindiko/makafara mengine ya kitaifa
 
Mwenge sijaona umuhimu wake zaidi ya ngono zembe, magonjwa ya ngono mimba zisizo tarajiwa.

Umepumbaza watanzania wengi.
UK kule kuna mfumo wa kifalme,hiyo familia,inakula bure,inalipwa mishahara bure,hawazalishi chochote,
Lakini huwezi kumsikia RAIA wa UK anapiga kelele kwamba huo ni unyonyaji.Vyetu sio vibaya kwasababu tu hakuna wazungu wanaofsnya kama sisi.Hata malikia wa UK anakifimbo chake,na huwa kinakimbizwa nchi zote zilizotawaliwa na Uingereza.
USA kuna utamaduni ambao raisi hufsnya kitendo cha kumuweka huru Turkey,"setting the turkey free"
Hufanyika kila mwaka.
Huyu turkey ni ndege jamii ya kuku,Mwaka Jana,Trump alionekana akisema"in the name of ....iam setting you free/.
Wewe unaweza kuona huu utamaduni ni wa kipuuzi,lakini kwa wa America ni symbol kubwa sana.
Usidharau na kubeza vya kwako kwa sababu tu mabwana wakubwa wazungu,hawavifanyi,au wamesema ni vya kishenzi.
Fanya tafakuri kubwa,njoo na njia mbadala ya kuweka mambo.
Vitu visivyo na tija ni kama kuwa na Mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya,mkurugenzi,katibu tawala wa mkoa,katibu tawala wa wilaya.Au kila wakati kuongeza idadi ya wilaya na mikoa.wakati ukubwa wa eneo la kijiografia upo pale pale.
Majimbo ya US yapo Yale Yale,sijawahi kusikia jimbo limegawanywa kutengeneza jimbo lingine,kwa sababu ya idadi ya watu
 
Ndo maana ukiwa huelewki tunasema wewe ni mtoto wa mwenge " yaani umetungwa kwenye mkesha wa mwenge".maana pale ni full zindiko
 
nyie mnao taka matambiko yafe....mmewaza kwa kutumia akili gani...? serikali haina dini lakini ina imani sana juu ya kutambika....iacheni kabisa serikali ifanye matambiko....😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mwenge wafipa huita Ichaka,kweli mwenge Sumbawanga enzi hizo ilikuwa ikitokea kuna jambo baya limetekea basi kila nyumba ilitoa majani toka kwenye paa la nyumba ulitengenezwa mwenge (ichaka)na wazee waliwasha moto yale majani na kuanza kuzunguka kijiji huku wakisema maneno sijui yapi.sitaki kusema mengi kwani haya ni ya huko.lakini mambo haya mmmmh.
 
Alafu wote walioleta ma kuanzisha haya matambiko juu ya nchi ni waislam. Nafikiri waislam wanakitu cha kujibu juu ya Matambiko.
 
WWE ni seat ya shetani. Kwa mfano ikitokea kuna mtu kasign up na wwe utasikia watangazaji wakisema, "he's just signed a deal with the devil himself"

John cena, randy orton, aj styles, bray wyatt etc wote ni occultists. Binafsi nimeacha pia kufuatilia wwe
Kumbe tupo wengi.... Kuna ufalme wanawakilisha
 
Kwa mujibu wa maelezo yako ya awali,mimi nahisi/huenda ikawa
Mwenge unaangaza Taifa kupitia Mizimu ya Bagamoyo na ile ya Mlima Kilimanjaro..unapougusa pasipo ridhaa ya mila na desturi ya waliopewa dhamana ya kuukimbiza au kuupokea pia ukijaribu kuufata hadi usawa wa askari "you are shot on spot"
Tambiko lolote ukilivunja gharama yake ni nzito.
NB: Kama Mungu yupo pia Shetani yupo
Thinking great way... Kila kitu kina pande mbili
 
Ndo maana ukiwa huelewki tunasema wewe ni mtoto wa mwenge " yaani umetungwa kwenye mkesha wa mwenge".maana pale ni full zindiko
[emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom