Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Hujui unachokisema, ngoja nikupe shule kidogo, ndio utaelewa.Ukimaliza form 4 inafaa uanze kusomea taaluma mapema, kuna advantages nyingi kuliko kusomea form 6 ikiwemo kuwa na uwanja mpana wa ajira unaweza kuomba ajira zote diploma na degree, kuwa na cv ndefu ya kusomea taaluma, kufanya trainings za kazi kwa vitendo zaidi, kuweza kubadili taaluma ukiingia degree, n.k.
Huna point kabisa unaposema advance inakomaza akili, kwa experience yangu nilivyosoma form 6.
- Wanachapwa viboko kama watoto wadogo
- wanachungwa kama form 1 kuanzia muda wa kuamka, kulala, kunyoa ndevu, n.k.
- Ni watu wazima wasioruhusiwa kuwa na mahusiano
- Hawaruhusiwi kumiliki simu
- wanasubiria mtihani moja wa taifa kupima uwezo wao miaka miwili shuleni.
- n.k.
Leo hii mtoto anayemaliza form four mara nyingi utakuta hata miaka 18 hajafika, kumkimbiza kwenye maisha ya kichuo ni kumbemenda tu kiakili na kimaadili, chuo kinaishia kumuharibu tu na sio kumtengeneza. Chunguza hilo, utagundua kitu.
Pili, mtoto akishakwenda kusoma diploma ya fani fulani maana yake huko mbeleni hawezi tena kuja kusomea fani nyingine kwa msingi wa hiyo diploma. Je, watoto wetu wamejiandaa au kuandaliwa vyema kujua ni fani ipi wataishi nayo maishani?
Tatu, fahamu tu, kusoma ili kuja kuajiriwa kwa kutumia hiyo diploma kwa zama hizi hakupo kabisa, na ikitokea basi itakuwa ni kwa mshahara mdogo sana.
Mwisho, kwa mtoto aliyefaulu vizuri O-level (division one au two) halafu kwenda kusoma diploma ili mwisho wa siku kuja kusoma degree ni kupoteza muda zaidi na kubahatisha.