Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Kwa wale wapenzi wa Bongo Fleva, mtakumbuka kuwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, staa wa muziki huo wakati huo, Hussein Machozi, alitoa wimbo uliogusa hisia za wengi ambao ndio umebeba Title ya thread hii “KAFIA GETTO.” Wimbo huu ulielezea kisa cha kweli kilichotokea kwa mmoja wa watu wa karibu wa Machozi, hali iliyompelekea kuandika wimbo huu wenye ujumbe mzito.
View: https://youtu.be/pqfYFzGARkI?si=gKrNkLF4_CzL6w59
Mbali na mkasa uliosimuliwa kwenye wimbo huo, pia kuna tukio la kweli lililotokea huko Mwanakwereke, Jitimai - Zanzibar, takribani miaka 6 iliyopita, mwaka 2018. Katika kisa hicho, bwana mmoja aitwaye Ibrahim Kibuyu alijikuta matatani baada ya mpenzi wake kufariki akiwa katika himaya yake walipokuwa wamekutana kwa ajili ya faragha zao. Tukio hili lilizua maswali mengi na kumuweka Ibrahim kwenye mtego wa kisheria, hali iliyoleta changamoto kubwa kwa pande zote mbili za familia na kwa jamii iliyoshuhudia tukio hilo.
View: https://youtu.be/5OOo4FtI4uw?si=JHGLSheceto76qka
Visa hivi viwili ndivyo vilichonivuta hapa kwenu wanajamvi na kuandika thread hii ni kutaka tu kupeana code iwapo situation ile ikitokea kwako mwana JF ni wapi utachomokea, je utetezi gani utatumia ili uonekane mkweli mbeli ya uso wa sheria?
Ni wazi kwamba katika hali za kawaida, watu wengi tumekuwa na mahusiano yasiyo rasmi (wanayo yajua marafiki zety tu, ndugu aaaaah - in Steve Mweusi’s Voice), na kama ilivyo ada, mahusiano bila mchezo hayanogi na raha ya mechi bao🥰. Waswahili wanasema ‘kichwa cha chini kikitaka jambo lake, cha juu huwa kina cease kufanya kazi kabisa’😂
Inawezekana 99.99% ya watanzania wote tumesha jihusisha na mahusiano yasiyo rasimi na kutumii maeneo tunayoishi (mageto) kama uwanja wa nyumbani na sometimes kwenda kwenye viwanja vya ugenini (mageto ya wenza wetu) bila familia au ndugu kujua chochote kuhusu mahusiano hayo.
Lakini hebu tujaribu kufikiria Ikiwa mpenzi wako huyu asiyejulikana na familia yako ama ndugu zako wala familia yao haikutambui akifariki ama kupata tatizo lolote kubwa akiwa katika himaya yako, utajibu nini mbele ya familia yake? Uta jibu nini mbele ya vyombo vya sheria? Au ndo tutaishia kuilaumu mahakama kuwa haitendi haki?🤷🏽♂️
Mbali na visa hivyo, pia ipo kesi iliyowahi kutokea huko kijiji cha Buturi, wilaya ya Butiama mkoani Mara, ambapo tukio hili liliwaacha watu wengi midomo wazi. Tukio lilitokea katika siku ya Valentine mnamo mwaka 2018, ambapo Bi. Mecklida Hassani alifariki ghafla alipokuwa akifanya mapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, Bwana Mashimba Silingi (can you imagine🧐).
Mwili wa Mecklida ulikutwa na majeraha shingoni, akiwa karibu na nyumba yake, huku kondomu zikiwa pembeni. Mashimba alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la mauaji, lakini aliieleza mahakama kuwa kifo hicho kilitokea bila ugomvi au nia mbaya bali kilitokewa walipokuwa wakifanya mapenzi huku akisisitiza kuwa hakuwa akifikiria kama binti alikua akikata roho bali alifikiri ni utamu tu bibiye anausikilizia, na mwishowe aliachiliwa kwa kukosekana ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kosa hilo.
Mjadala huu unalenga kuibua mitazamo tofauti kuhusu athari za mahusiano yasiyo rasmi, hasa pale linapotokea tukio baya. Je, umewahi kujiuliza maswali haya? Au umewahi kushuhudia hali kama hii na kuona wengine wakijinasua? Tupe uzoefu wako, mitazamo yako, na mawazo yako ili wengine nao wapate funzo na kuchukua tahadhari!✍️
N:B. YAKIKUKUTA NDO UTAELEWA