“Kafiti hatoshi Ilemela?”kauli ya Rc Mwanza kwa Kafiti “Kukalia kiti nunusu”

“Kafiti hatoshi Ilemela?”kauli ya Rc Mwanza kwa Kafiti “Kukalia kiti nunusu”

Oneonone

Member
Joined
May 5, 2026
Posts
17
Reaction score
17
“KAFITI HATOSHI ILEMELA?”KAULI YA RC MWANZA KWA KAFITI “KUKALIA KITI NUNUSU”.


Siku chache zilizopita Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, alitoa kauli yenye mashaka na utata ndani yake kuhusu Mbunge wa Ilemela Kafiti William.

Kauli ya mkuu wa mkoa ilikuwa hivi, nanukuu maneno yake,” wewe sasa ni wakati wa kuchapa kazi wewe ndo Mbunge wa Ilemela kalia kiti ipasavyo usikae nusunusu”. kauli hii imeleta maswali kwa wananchi.

Kitendo cha Mkuu wa mkoa kutoa kauli hiyo, kumeibu maswali mengi moja wapo ni kwamba Mbunge huyo anafanya kazi kwa hofu ya mtangulizi wake, kutojuamini na kile anachokifanya, mgogoro wa uongozi ndani ya jimbo la Ilemela baada ya uchaguzi bado lipo fukuto, Mbunge huyo kutokuwa karibu na wananchi wake.

Baada ya kauli hiyo, mwandishi wa andiko hili alifanya Uchunguzi na kubaini kuwa, katika jimbo la Ilemela baada ya uchaguzi, makundi yaliyokuwepo wakati wa uchaguzi bado yanaendelea kusigana vikali.

Makundi mengine yanaona kuwa, likianza kundi la aliyekuwa Mbunge aliyemaliza muda wake, Angelina Mabula, kuwa wao ndo walipaswa kutumikia wananchi kitendo hicho kinatajwa kumfanya Mbunge huyo kukosa nguvu ya kutumikia wananchi na kukalia kiti nusunusu kama kauli ya Mkuu wa mkoa.

Kundi lingine ni la Manguzo, ambalo lenyewe nalo linaamini pia wao ndo walipaswa kuwa watawala wa jimbo hilo kwa awamu hii kutokana na nguvu na ushawishi ambao walikuwa nao kwa wananchi.

Kundi hilo la Manguzo, limeendelea na harakati za kutaka kumuangusha Mbunge huyo ambaye pia hana ushawishi kwa wananchi kwa kuwa tangu achaguliwe hakuna mipango na mikakati mipya ya maendeleo Ilemela.

Uchunguzi wa mwandishi wa andiko hili, baada ya kuzungumza na wananchi wake Ilemela wanadai kuwa, wanaona na itakuwa, Mbunge huyo atakuwa ni wa awamu moja.

Sababu zao wao Mbunge huyo kuwa wa awamu moja ni kwa sababu moja, katika kipindi cha kura za maoni ndani ya chama hakuwa mshindi na hakuwa chaguo la wanaccm.

Wanasema Mbunge huyo sio chaguo la wanaccm walio wengi kwani yeye aliteuliwa na wala hakuchaguliwa na wanachama wa Ilemela, kutokana na hali hiyo ubunge wake wana mashaka nao na utakuwa wa awamu moja.

Hivyo, kauli ya Mkuu wa mkoa kwenda kwa Kafiti kukalia kiti cha ubunge nusunusu, inalenga moja ya makundi hayo kuendelea kuwa karibu na wananchi wa Ilemela.

Wilaya ya Ilemela kwa muda mrefu, ni miongoni mwa wilaya ambayo ina uhaba wa maji kwa wananchi wake, wananchi wengi Ilemela wanatumia maji ya visima ambayo sio safi na salama.
 
Back
Top Bottom