Kafulila aeleza siri tatu muhimu kufanikisha dira 2050

Kafulila aeleza siri tatu muhimu kufanikisha dira 2050

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila ametaja mambo matatu ya msingi yanayopaswa kupewa kipaumbele ili Tanzania ifanikishe Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa mahojiano na kituo cha habari cha ITV katika kipindi cha Kipima Joto, Kafulila amesema mafanikio ya Dira hiyo yanategemea rasilimali watu yenye maarifa, nafasi ya kijiografia ya nchi na diplomasia ya kiuchumi.

“Lazima tuwe na nguvu kazi yenye elimu na ujuzi wa kushindana na kuzalisha mali ili kujenga uchumi imara,” amesema Kafulila

Kafulila amesema jiografia ya Tanzania ni fursa kubwa inayoweza kubadilisha uchumi zaidi ya sekta nyingine yoyote kwani nchi inapakana na mataifa mengi yasiyo na bandari na hutegemea Tanzania kufanya biashara na dunia.

“Zaidi ya asilimia 80 ya biashara duniani hupitia baharini. Tanzania ikiwa na eneo kubwa la bahari na bandari zinazohudumia nchi jirani, tuna nafasi ya kipekee kunufaika kiuchumi. Hivyo uwekezaji katika sekta ya miundombinu, hususani bandari ni muhimu,” amesema.

Akizungumzia diplomasia ya kiuchumi, Kafulila amesema ni nyenzo isiyoonekana moja kwa moja lakini yenye matokeo makubwa kwa uchumi wa taifa.

“Tangu Serikali ya Awamu ya Sita ifungue milango ya diplomasia ya kiuchumi, biashara ya kimataifa ya Tanzania imeongezeka. Mwaka 2021 mauzo na manunuzi ya nje yalikuwa takribani dola milioni 17 lakini sasa yamepanda hadi zaidi ya dola milioni 34,” amesema.

Kwa mujibu wa Kafulila, ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi za kimkakati katika kukuza uhusiano wa kibiashara na mataifa mengine jambo linalochangia moja kwa moja ustawi wa uchumi wa nchi.

Credit:Jambo
 
Usitoe rushwa ili upige au usipige kura. Piga 113 kutoa taarifa za rushwa
 
Back
Top Bottom