Kafulila: Kwanini utekelezaji mradi wa LNG Tanzania umechelewa?

Kafulila: Kwanini utekelezaji mradi wa LNG Tanzania umechelewa?

Na David KAFULILA

KUNA sababu nyingi za kuchelewa kwa LNG yetu kulinganisha pengine na tulivotarajia kama nchi lakn pia kulinganisha na washindani wetu eneo hilo kama Mozambique.

Sababu kubwa kwa maoni yangu mimi ni anguko la bei ya gas duniani kwa karibu muongo mzima. Tathimini ilofanywa na taasisi ya kimataifa ya Natural Resources Governance Institute ( NRGI) kwenye report yao mwaka 2014 ilionesha kwamba kwa mazingira ya kuzalisha LNG Tanzania bei inatakiwa walau iwe $14 kwa 1mmmBtu( kufikia Break even point ). Kitu ambacho hakijatokea kwa muda sasa.

Sio kiwango cha juu sana kwani kuna miaka ilifika hata 18/mmmBtu. Hata hivyo bei ya gas iliendelea kuanguka mpaka $7/mmmBtu na hata $3.5/mmmBtu. Anguko hili la bei ya gas linawapa sababu makampuni haya( IOCs) kwanza kufikiria upya uwekezaji wao kama waendelee lkn zaidi kama wanaendelea wanalazimika kuja na terms mpya zenye mabadiliko makubwa kutokana na tofauti kubwa ya anguko la bei.

Lakn wapo wanaoweza hoji kwann Mozambique tulianza nao miaka ya 2012/13 lakn wao wakafikia muafaka kwajili ya uwekezaji( Investment Decision) kabla yetu wakati sababu za anguko la bei ni dunia nzima?

Kunaweza kuwa na sababu za ziada , lakn kwa maoni yangu moja ya sababu kubwa ni kwamba gas yao ni rahisi kuivuna kwa gharama nafuu kuliko Tanzania na hivyo wanakuwa na faida ya kuishindan. Asilimia 85% ya gas ya Mozambique ipo kinakifupi(shallow water) ambapo wastani wa kuchimba kisima ni kati ya $50m-$70m kulinganisha na Tanzania ambapo asilimia 90% ya Gas ipo kinakirefu(deepsea) ambapo wastani wa bei ya kuchimba kisima kimoja ni $100m-$120m. ( hii kwa takwimu za mwaka 2015).

Kwa mazingira hayo ni wazi kwamba ilikuwa rahisi kwa IOCs kuanza Mozambique hasa ukizingatia anguko hili kubwa la bei. Sababu nyingine ni uwezo wetu wa ndani kwenye eneo la gas ambalo mkataba mkubwa kama huu wa $30bn, unahusisha taaluma nyingi kuanzia Sayansi za gas, biashara, uchumi, sheria na zote zinahitaji uzoefu mkubwa na sio tu suala la Dr au Profesa kwani mnaenda mezani kukaa na kampuni zenye uzoefu wa zaidi ya karne eneo hilo.

Katika hali ya kawaida tunahitaji kuhusisha wazoefu wakubwa eneo hilo hata kama wanatoka nje. Tusijilazimishe kutumia wataalamu wa ndani kwenye maeneo ambayo hatujajiandaa. Kwenye dunia ya ushindani unaangalia tu unataka nn haijalishi anaekusaidia anatoka wapi.

Ndio sababu Uingereza baada ya mtiksiko wa uchumi duniani wa mwaka 2008 waliajiri Gavana wa Bank Kuu ambae ni raia wa Canada ambae amewahi kuwa Gavana wa Bank Kuu Canada.( sijiulizi kama Tz tunaweza bali nchi ngapi duniani zimefika huko? Chache mno na sio kosa).Tuangalie uwezo na tunachokitaka.

Maana yangu ni kwamba kwa mabadiliko makubwa katika eneo la gas yaliyojitokeza katika muongo mmoja ni wazi yatalazimisha fikra tofauti majadiliano ya mikataba tofauti na mazoea ya hapo kabla. Hii maanake inahitaji team yenye uwezo na mauzoefu ya kutosha eneo hili ili kutosumbuana kwenye majadiliano.

Tunawezakupata mshauri mwelekezi kutoka popote duniani sio kuamua bali kusaidia team yetu ikiwemo kujengeana ufahamu wa ziada. Nasema hili kwasababu lazma na muhimu tuamue kwa usahihi haijalishi kwa bei gani muhimu ndio bei sahihi.

Nasema haya kwasababu huko mbeleni jambo hili linaweza kuleta siasa za kwann tumekubali terms hizi wakati kwingine walifanya kwa terms nzuri zaidi bila kujua biashara hii ni complex na inategema mambo mengi ikiwemo mazingira yenu kama nilivoeleza hapo juu na zaidi muda mnaoingia mkataba kwa maana soko linazungumza nini na matarajio yapoje( market projections), impact ya COVID-19 kwenye FDI duniani na zaidi Africa ambayo itaongoza kwa anguko la FDI, pia masuala ya usalama ambapo washindani ktk biashara hizo usikute terrorism ni sehemu ya business strategy.

Nasema hili kwakuzingatia kilichotokea Mozambique juzi ambapo kampuni ya TOTAL imeahirisha uwekezaji mkubwa wa LNG ya $20bn kwa hofu za usalama kutokana na masuala ya ugaidi.sisemi kwamba tufurahie kushindwa kwa Mozambique ni fursa kwetu maana Rais wetu sio muumini wa 'zero sum game' kwamba ufaidike kwa mwenzako kuumia! Bali nachosema ni lesson tunapojipanga.

Huu ni uwekezaji mkubwa kupata kutokea kwenye ukanda wote wa africa mashariki. Ni nusu ya uchumi wa Tz, ni theluthi ya uchumi wa Kenya na ni sawa na uchumi wa Uganda au mara mbili ya uchumi wa Rwanda.

Nihitimishe kwa kusema tusiogope kutafuta mshauri popote duniani kusaidiana na wataalamu wetu kufikia mkataba bora. Sio aibu! Uingereza wakati inachakata kujitoa umoja wa Ulaya- BREXIT , ilikodi mtaalamu mshauri ( consultant) kutoka Newzland kuongoza team ya Uingereza kufikia mikataba mipya ya kibiashara na mataifa mengine dunian.

Alipohojiwa waziri Mkuu wa Uingereza kwann atafute mtaalamu nje wakati Uingereza ina heshima kubwa kwa kuwa na vyuo bora duniani alijibu kwamba Uingereza imepoteza uzoefu wake ktk kuingia mikataba ya aina hiyo kama nchi kwani kwa miaka mingi ilifanywa Brussels chini ya Umoja wa Ulaya( EU).

Zaidi, nikweli tumechelewa, lakn hatujachelewa sana kwa kuzingatia uzoefu wetu kisera na kitaasisi eneo hilo. Nakumbuka Canada, Taifa kubwa, lenye sera imara na wataalamu wakubwa na wenye uzoefu mkubwa eneo la gas kuliko sisi walifikia makubaliano na IOCs kwa mradi mmoja wa Kitimat wa $31bn( karibu sawa na wetu wa $30bn) Mwaka 2018 baada ya miaka7 ya majadiliano, na walikuwa na miradi 20, mingine 19 wakakubaliana kutokubaliana ! Yote ni makubaliano, muhimu iwe hivyo kama ni lazma sana.

Wasalaam.

MUHIMU: Haya ni maoni yangu kama David Kafulila.
Hongera David kwa kujitwisha mzigo na kazi ya kutolea maelezo mradi huu wa LNG. Mimi ni mmoja kati ya watu waliosomeshwa sana na kitendo cha kuuweka pembeni mradi huu na kuanza mipya ukiwemo wa bwawa la Nyerere. Tuliambiwa enzi ya JK kuwa nchi yetu ingekuwa ya uchumi wa gas. Kupitia mradi huu tulitegemea kupata umeme, ajira na uwekezaji mkubwa toka nje. Vyombo vya usafiri vingetumia gas badala ya mafuta ya petrol ama diesel kwa kiwango kikubwa na hivyo kuokoa matumizi ya hela za kigeni. Tusingelazimika kutumia hela zetu za ndani au za nje na kujilimbikizia madeni makubwa ili kujitosheleza kwa umeme. Kwa bahati mbaya serikali ilipoamua kuibadilisha gia angani haikutoa maelezo ya kujitosheleza. Ingekuwa jambo la busara sana kama wakati wa mabadiliko tungeelrzwa yaliyotokea kama bwana Kafulila anavyojaribu kufanya sasa hivi. Tukumbuke kuwa suala hili la gas liligharimu maisha ya ndugu zetu wa Mtwara. Katika kupoza hali hiyo serikali ilitoa ahadi na maelezo yaliyosaidia kupoza hali. Kwa hiyo halikuwa jambo la busara kuuacha huu mradi bila maelezo. Ilivyotokea ndugu zetu hawa wamehisi kudanganywa na uharibifu wote kukosa maana.
 
Uko sahihi, nadhani tunahitaji kujenga taasisi imara zisizo athiriwa na maslahi binafsi ya wanasiasa ili tuweza kuwa monitor wasomi wetu watuletee tija tarajiwa.

Hata pale wanasiasa wanapo jaribu kutuaminisha kuwa wanatekeleza ushauri wa wataalam/wasomi, deep down wasomi hao tunao ambiwa huwa wanashauri kwa kufuata maslahi ya wanasiasa pengine kulinda 'ugali' wao.

Wanasiasa wanatuambia tuwasikilize wataalam wakati wataalam wana wasikiliza wanasiasa, yaan wasomi wetu wamegeuzwa speaker za wanasiasa.
Unajua mkuu gspain, haya mambo tunayajadili hapa kivyepesivyepesi hivi lakini ni mambo ya msingi sana kwa taifa lolote kujitambua na kutafuta maendeleo kwa dhati.

Hebu jaribu kutazama serikali zetu zote, kasoro ile ya Mwalimu Nyerere. Utaona kwamba viongozi wetu wakuu wanajipigia tu kwenda mbele bila ya kutafakari kwa kina tunakwenda mbele kivipi, na matokeo ndiyo haya tunayoyaona kama ya vuruguvurugu tu.

Tokea tupate uhuru, ni wataalam wangapi tumewasomesha, Wamefanya nini, na wapo wapi sasa? Wengi wa madarasa ya akina Kikwete ndio hao sasa wamestaafu, bila ya kuweka msingi wowote wa utaalam wao ili taifa lipandie hapo kwenda mbele na hawa wanaoingia sasa!
What a waste?

Kuna ma-engineer wangapi wamesomeshwa ndani na nje ya taifa hili..., wapo wapi na wamefanya nini ambacho watarithisha wenzao wanaoingia na kuendelea?
Tuna wanasayansi wabobezi wangapi katuika nyanja mbali mbali..., madawa, kemia, biologia,n.k. Wapo wapi, na wamefanya nini?

Kwa mfano: chukulia hao wa madawa, pale Muhimbili. Chuo kile kilianzishwa kwa maksudi mazima ili nchi ipate wataalam wake wenye uwezo wa kuendesha viwanda vya madawa hapa nchini. UNDP ikatoa mwongozo pale wizarani (Afya), bila shaka mafaili bado yapo pale yamejaa mavumbi.
Watu wakasoma na wengine wakapelekwa nje ya nchi kwa utaalam zaidi.
Viwanda vichache vilijengwa, Keko na hata kule Arusha, vikafa kwa sababu mbalimbali (sio kwa sababu ya kukosa waendeshaji.)

Lakini wazo langu ni hili: chuo kile pale Muhimbili, na vingine kadhaa sasa hapa nchini, vimekuwa vya kuzalisha wauza maduka wenye digrii ya juu kabisa!

Nchi hii ingeshindwa nini, kwa mfano hata leo hii ikaweka mkakati kwamba ni lazima tuzalishe sehemu kubwa ya madawa yetu hapahapanchini. Ikaweka taratibu za kuwakusanya wataalam hawa na kuwapa mwongozo ni nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani.

Kama ni viwanda binafsi, au vya ushirikiano na serikali, hilo silizungumzii hapa, lakini la muhimu ni lengo lililowekwa...

Viinchi, kama Taiwan, Israel ni mashuhuri sana kwa utengenezaji wa kemikali ghafi za utengenezaji madawa, hata kampuni kubwa zinaagiza toka kwao. Wao waliamua iwe hivyo, na wakaweza. Sisi hapa tunazo malighafi tele za viwanda vya kemikali, tutashindwaje tukiamua kuwatumia kwa ushirikiano wataalam wetu wakatumia mali hizi?

Mara zote tunarudi palepale, ni swala la uongozi wetu. Kupata viongozi wenye dira ya kujua tunataka kwenda wapi.

Sasa hivi naona tumempata anayeamini usalama wetu na maendeleo yetu yatatokana na kuegemea zaidi kwa watu wengine toka nje, kuliko hawa waliopo ndani ya nchi.
 
Hongera David kwa kujitwisha mzigo na kazi ya kutolea maelezo mradi huu wa LNG. Mimi ni mmoja kati ya watu waliosomeshwa sana na kitendo cha kuuweka pembeni mradi huu na kuanza mipya ukiwemo wa bwawa la Nyerere. Tuliambiwa enzi ya JK kuwa nchi yetu ingekuwa ya uchumi wa gas. Kupitia mradi huu tulitegemea kupata umeme, ajira na uwekezaji mkubwa toka nje. Vyombo vya usafiri vingetumia gas badala ya mafuta ya petrol ama diesel kwa kiwango kikubwa na hivyo kuokoa matumizi ya hela za kigeni. Tusingelazimika kutumia hela zetu za ndani au za nje na kujilimbikizia madeni makubwa ili kujitosheleza kwa umeme. Kwa bahati mbaya serikali ilipoamua kuibadilisha gia angani haikutoa maelezo ya kujitosheleza. Ingekuwa jambo la busara sana kama wakati wa mabadiliko tungeelrzwa yaliyotokea kama bwana Kafulila anavyojaribu kufanya sasa hivi. Tukumbuke kuwa suala hili la gas liligharimu maisha ya ndugu zetu wa Mtwara. Katika kupoza hali hiyo serikali ilitoa ahadi na maelezo yaliyosaidia kupoza hali. Kwa hiyo halikuwa jambo la busara kuuacha huu mradi bila maelezo. Ilivyotokea ndugu zetu hawa wamehisi kudanganywa na uharibifu wote kukosa maana.
Huu mradi utafanikiwa endapo tu ile sheria kandamizi kwa wawekezaji ya mwaka 2017 itafanyiwa marekebisho ya kina
 
Unajua mkuu gspain, haya mambo tunayajadili hapa kivyepesivyepesi hivi lakini ni mambo ya msingi sana kwa taifa lolote kujitambua na kutafuta maendeleo kwa dhati.

Hebu jaribu kutazama serikali zetu zote, kasoro ile ya Mwalimu Nyerere. Utaona kwamba viongozi wetu wakuu wanajipigia tu kwenda mbele bila ya kutafakari kwa kina tunakwenda mbele kivipi, na matokeo ndiyo haya tunayoyaona kama ya vuruguvurugu tu.

Tokea tupate uhuru, ni wataalam wangapi tumewasomesha, Wamefanya nini, na wapo wapi sasa? Wengi wa madarasa ya akina Kikwete ndio hao sasa wamestaafu, bila ya kuweka msingi wowote wa utaalam wao ili taifa lipandie hapo kwenda mbele na hawa wanaoingia sasa!
What a waste?

Kuna ma-engineer wangapi wamesomeshwa ndani na nje ya taifa hili..., wapo wapi na wamefanya nini ambacho watarithisha wenzao wanaoingia na kuendelea?
Tuna wanasayansi wabobezi wangapi katuika nyanja mbali mbali..., madawa, kemia, biologia,n.k. Wapo wapi, na wamefanya nini?

Kwa mfano: chukulia hao wa madawa, pale Muhimbili. Chuo kile kilianzishwa kwa maksudi mazima ili nchi ipate wataalam wake wenye uwezo wa kuendesha viwanda vya madawa hapa nchini. UNDP ikatoa mwongozo pale wizarani (Afya), bila shaka mafaili bado yapo pale yamejaa mavumbi.
Watu wakasoma na wengine wakapelekwa nje ya nchi kwa utaalam zaidi.
Viwanda vichache vilijengwa, Keko na hata kule Arusha, vikafa kwa sababu mbalimbali (sio kwa sababu ya kukosa waendeshaji.)

Lakini wazo langu ni hili: chuo kile pale Muhimbili, na vingine kadhaa sasa hapa nchini, vimekuwa vya kuzalisha wauza maduka wenye digrii ya juu kabisa!

Nchi hii ingeshindwa nini, kwa mfano hata leo hii ikaweka mkakati kwamba ni lazima tuzalishe sehemu kubwa ya madawa yetu hapahapanchini. Ikaweka taratibu za kuwakusanya wataalam hawa na kuwapa mwongozo ni nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani.

Kama ni viwanda binafsi, au vya ushirikiano na serikali, hilo silizungumzii hapa, lakini la muhimu ni lengo lililowekwa...

Viinchi, kama Taiwan, Israel ni mashuhuri sana kwa utengenezaji wa kemikali ghafi za utengenezaji madawa, hata kampuni kubwa zinaagiza toka kwao. Wao waliamua iwe hivyo, na wakaweza. Sisi hapa tunazo malighafi tele za viwanda vya kemikali, tutashindwaje tukiamua kuwatumia kwa ushirikiano wataalam wetu wakatumia mali hizi?

Mara zote tunarudi palepale, ni swala la uongozi wetu. Kupata viongozi wenye dira ya kujua tunataka kwenda wapi.

Sasa hivi naona tumempata anayeamini usalama wetu na maendeleo yetu yatatokana na kuegemea zaidi kwa watu wengine toka nje, kuliko hawa waliopo ndani ya nchi.
Ni kweli mkuu Kalamu1, haya ni mambo mazito sana kwa taifa.

Ni ukweli kwamba hizi tawala zote baada ya Nyerere kwa maoni yangu zilijikita/zimejikita katika kuhakikisha zinadumu madarakani na vizazi vyao hivyo havigusii kabisa ujenzi wa taasisi bora kwa kuwa taasisi bora zinatupa nje hawa 'walafi' wote wa madaraka.

Nyerere katika makosa makubwa aliyowahi kufanya ambayo kwangu me huwa namuona hana maana ni kitendo chake cha kuacha taifa likiwa na mifumo na miundo mibovu na hasa katiba. Yaani issue ya utawala ni ya utashi wa rais aliye madarakani., tena Nyerere anatamla wazi wazi kuwa tatizo hilo alilijua vema na hakuchukua hatua kurekebisha.

Ndio maana utaona kila kiongozi akiingia anaingia na maono yake na ikibidi anatupilia mbali yale aliyokuta tena mara nyingi kwa sababu za 'ulafi' binafsi naye apige % zake.

Kitendo cha taifa lenye umri wa Tanzania kutokuwa na 'National Mission and Vision' zinazo tamkwa kikatiba ni kosa la karne.

Hadi sasa tunaimba sisi ni wajamaa ila ukitazama tunavyo endesha mambo yetu unajiuliza hawa watu kwa akili zao wanafikiri wanamhadaa nani labda zaidi ya kujiongopea wenyewe?

Maana kwenye ujamaa hatupo na huku hatuutaki upebari ila kudeclare sisi tunafuata mixed economy hatutaki, ndio yale ya Prof. Kezilahabi...Kaptula la Marx na shati la Mao.

Utaona tumeleta ujinga hadi kwenye mambo sensitive, hivi leo sifa ya ubunge ni kujua kusoma na kuandika kweli?! Kisha unatuambia waziri ni lazma atokane na mbunge... vichekesho na wasomi wote wamekaa kimya wanakenua tu. Sheria zitungwe na std 7, hao hao wajadili mikataba na zile lugha za sheria zilivyo, kisha waishauri na kuisimamia serikali...

Umegusia kidogo namna sekta ya afya ilivyo 'chochora' baada ya wahusika kuacha plan za kitaifa na kuanza kujiingiza kwenye biashara za kuiuzia serikali madawa na hivyo kuua ubunifu na ugunduzi wa wataalam wetu wa ndani.

Sekta za kilimo, biashara, elimu, siasa na utawala nk nk zoote hizo zinapitia the same challenge, hakuna succession plan, hakuna accountability, hakuna professionalism, hakuna integrity... yan kila kitu ni hovyo hovyo.

Hadi tutapo amua kwa dhati kuondokana na huu upuuzi uliopo ndipo tutaanza kupiga hatua, na kwa hekima za kitanzania nadhani hadi tukwame kabisa ifike sehemu kuongoza nchi iwe mzigo wa kukimbiwa na sio ulaji tena.
 
Ni ukweli kwamba hizi tawala zote baada ya Nyerere kwa maoni yangu zilijikita/zimejikita katika kuhakikisha zinadumu madarakani na vizazi vyao hivyo havigusii kabisa ujenzi wa taasisi bora kwa kuwa taasisi bora zinatupa nje hawa 'walafi' wote wa madaraka.
Tatizo letu ni hapo, na ninashukuru sana umelieleza kwa ufasaha kabisa katika mistari miwili tu. Hongera sana.
 
Huu mradi utafanikiwa endapo tu ile sheria kandamizi kwa wawekezaji ya mwaka 2017 itafanyiwa marekebisho ya kina
Sheria ambayo serikali yenyewe uliivunja wakati iliposaini mkataba mpya na Barrik na kuanzisha kampuni ya Twiga. Tuliambiwa mikataba itapitishwa na kuhakikiwa na bunge haikufanyika. Tuliambiwa kesi zitasikilizwa kwenye mahakama za Tanzania haiko hivyo na mengine ya kwenye sheria yamekikwa na serikali yenyewe. Serikali inatumia sheria pale inapoona ni convenient.
 
Back
Top Bottom