Kafulila: Kwanini utekelezaji mradi wa LNG Tanzania umechelewa?

Hongera David kwa kujitwisha mzigo na kazi ya kutolea maelezo mradi huu wa LNG. Mimi ni mmoja kati ya watu waliosomeshwa sana na kitendo cha kuuweka pembeni mradi huu na kuanza mipya ukiwemo wa bwawa la Nyerere. Tuliambiwa enzi ya JK kuwa nchi yetu ingekuwa ya uchumi wa gas. Kupitia mradi huu tulitegemea kupata umeme, ajira na uwekezaji mkubwa toka nje. Vyombo vya usafiri vingetumia gas badala ya mafuta ya petrol ama diesel kwa kiwango kikubwa na hivyo kuokoa matumizi ya hela za kigeni. Tusingelazimika kutumia hela zetu za ndani au za nje na kujilimbikizia madeni makubwa ili kujitosheleza kwa umeme. Kwa bahati mbaya serikali ilipoamua kuibadilisha gia angani haikutoa maelezo ya kujitosheleza. Ingekuwa jambo la busara sana kama wakati wa mabadiliko tungeelrzwa yaliyotokea kama bwana Kafulila anavyojaribu kufanya sasa hivi. Tukumbuke kuwa suala hili la gas liligharimu maisha ya ndugu zetu wa Mtwara. Katika kupoza hali hiyo serikali ilitoa ahadi na maelezo yaliyosaidia kupoza hali. Kwa hiyo halikuwa jambo la busara kuuacha huu mradi bila maelezo. Ilivyotokea ndugu zetu hawa wamehisi kudanganywa na uharibifu wote kukosa maana.
 
Unajua mkuu gspain, haya mambo tunayajadili hapa kivyepesivyepesi hivi lakini ni mambo ya msingi sana kwa taifa lolote kujitambua na kutafuta maendeleo kwa dhati.

Hebu jaribu kutazama serikali zetu zote, kasoro ile ya Mwalimu Nyerere. Utaona kwamba viongozi wetu wakuu wanajipigia tu kwenda mbele bila ya kutafakari kwa kina tunakwenda mbele kivipi, na matokeo ndiyo haya tunayoyaona kama ya vuruguvurugu tu.

Tokea tupate uhuru, ni wataalam wangapi tumewasomesha, Wamefanya nini, na wapo wapi sasa? Wengi wa madarasa ya akina Kikwete ndio hao sasa wamestaafu, bila ya kuweka msingi wowote wa utaalam wao ili taifa lipandie hapo kwenda mbele na hawa wanaoingia sasa!
What a waste?

Kuna ma-engineer wangapi wamesomeshwa ndani na nje ya taifa hili..., wapo wapi na wamefanya nini ambacho watarithisha wenzao wanaoingia na kuendelea?
Tuna wanasayansi wabobezi wangapi katuika nyanja mbali mbali..., madawa, kemia, biologia,n.k. Wapo wapi, na wamefanya nini?

Kwa mfano: chukulia hao wa madawa, pale Muhimbili. Chuo kile kilianzishwa kwa maksudi mazima ili nchi ipate wataalam wake wenye uwezo wa kuendesha viwanda vya madawa hapa nchini. UNDP ikatoa mwongozo pale wizarani (Afya), bila shaka mafaili bado yapo pale yamejaa mavumbi.
Watu wakasoma na wengine wakapelekwa nje ya nchi kwa utaalam zaidi.
Viwanda vichache vilijengwa, Keko na hata kule Arusha, vikafa kwa sababu mbalimbali (sio kwa sababu ya kukosa waendeshaji.)

Lakini wazo langu ni hili: chuo kile pale Muhimbili, na vingine kadhaa sasa hapa nchini, vimekuwa vya kuzalisha wauza maduka wenye digrii ya juu kabisa!

Nchi hii ingeshindwa nini, kwa mfano hata leo hii ikaweka mkakati kwamba ni lazima tuzalishe sehemu kubwa ya madawa yetu hapahapanchini. Ikaweka taratibu za kuwakusanya wataalam hawa na kuwapa mwongozo ni nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani.

Kama ni viwanda binafsi, au vya ushirikiano na serikali, hilo silizungumzii hapa, lakini la muhimu ni lengo lililowekwa...

Viinchi, kama Taiwan, Israel ni mashuhuri sana kwa utengenezaji wa kemikali ghafi za utengenezaji madawa, hata kampuni kubwa zinaagiza toka kwao. Wao waliamua iwe hivyo, na wakaweza. Sisi hapa tunazo malighafi tele za viwanda vya kemikali, tutashindwaje tukiamua kuwatumia kwa ushirikiano wataalam wetu wakatumia mali hizi?

Mara zote tunarudi palepale, ni swala la uongozi wetu. Kupata viongozi wenye dira ya kujua tunataka kwenda wapi.

Sasa hivi naona tumempata anayeamini usalama wetu na maendeleo yetu yatatokana na kuegemea zaidi kwa watu wengine toka nje, kuliko hawa waliopo ndani ya nchi.
 
Huu mradi utafanikiwa endapo tu ile sheria kandamizi kwa wawekezaji ya mwaka 2017 itafanyiwa marekebisho ya kina
 
Ni kweli mkuu Kalamu1, haya ni mambo mazito sana kwa taifa.

Ni ukweli kwamba hizi tawala zote baada ya Nyerere kwa maoni yangu zilijikita/zimejikita katika kuhakikisha zinadumu madarakani na vizazi vyao hivyo havigusii kabisa ujenzi wa taasisi bora kwa kuwa taasisi bora zinatupa nje hawa 'walafi' wote wa madaraka.

Nyerere katika makosa makubwa aliyowahi kufanya ambayo kwangu me huwa namuona hana maana ni kitendo chake cha kuacha taifa likiwa na mifumo na miundo mibovu na hasa katiba. Yaani issue ya utawala ni ya utashi wa rais aliye madarakani., tena Nyerere anatamla wazi wazi kuwa tatizo hilo alilijua vema na hakuchukua hatua kurekebisha.

Ndio maana utaona kila kiongozi akiingia anaingia na maono yake na ikibidi anatupilia mbali yale aliyokuta tena mara nyingi kwa sababu za 'ulafi' binafsi naye apige % zake.

Kitendo cha taifa lenye umri wa Tanzania kutokuwa na 'National Mission and Vision' zinazo tamkwa kikatiba ni kosa la karne.

Hadi sasa tunaimba sisi ni wajamaa ila ukitazama tunavyo endesha mambo yetu unajiuliza hawa watu kwa akili zao wanafikiri wanamhadaa nani labda zaidi ya kujiongopea wenyewe?

Maana kwenye ujamaa hatupo na huku hatuutaki upebari ila kudeclare sisi tunafuata mixed economy hatutaki, ndio yale ya Prof. Kezilahabi...Kaptula la Marx na shati la Mao.

Utaona tumeleta ujinga hadi kwenye mambo sensitive, hivi leo sifa ya ubunge ni kujua kusoma na kuandika kweli?! Kisha unatuambia waziri ni lazma atokane na mbunge... vichekesho na wasomi wote wamekaa kimya wanakenua tu. Sheria zitungwe na std 7, hao hao wajadili mikataba na zile lugha za sheria zilivyo, kisha waishauri na kuisimamia serikali...

Umegusia kidogo namna sekta ya afya ilivyo 'chochora' baada ya wahusika kuacha plan za kitaifa na kuanza kujiingiza kwenye biashara za kuiuzia serikali madawa na hivyo kuua ubunifu na ugunduzi wa wataalam wetu wa ndani.

Sekta za kilimo, biashara, elimu, siasa na utawala nk nk zoote hizo zinapitia the same challenge, hakuna succession plan, hakuna accountability, hakuna professionalism, hakuna integrity... yan kila kitu ni hovyo hovyo.

Hadi tutapo amua kwa dhati kuondokana na huu upuuzi uliopo ndipo tutaanza kupiga hatua, na kwa hekima za kitanzania nadhani hadi tukwame kabisa ifike sehemu kuongoza nchi iwe mzigo wa kukimbiwa na sio ulaji tena.
 
Tatizo letu ni hapo, na ninashukuru sana umelieleza kwa ufasaha kabisa katika mistari miwili tu. Hongera sana.
 
Huu mradi utafanikiwa endapo tu ile sheria kandamizi kwa wawekezaji ya mwaka 2017 itafanyiwa marekebisho ya kina
Sheria ambayo serikali yenyewe uliivunja wakati iliposaini mkataba mpya na Barrik na kuanzisha kampuni ya Twiga. Tuliambiwa mikataba itapitishwa na kuhakikiwa na bunge haikufanyika. Tuliambiwa kesi zitasikilizwa kwenye mahakama za Tanzania haiko hivyo na mengine ya kwenye sheria yamekikwa na serikali yenyewe. Serikali inatumia sheria pale inapoona ni convenient.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…