Kafulila: Mafanikio ya Kihistoria ya Bandari chini ya DP World na Vivuko vya Bakresa ni mwanzo tu wa matunda ya PPP kwenye kujenga Uchumi wa kisasa

Nahitaji mjadala wa.wazi na Kafulila
 
Mkataba wa DP world uliahidiwa kupelekwa bungeni kujadiliwa, Je tayari ushajadiliwa? Na kama bado haujapelekwa, nitaanzia wapi kusifia jambo hili hata kama limeleta matunda?

Yes! Rais Samia aweza kuwa yuko good sana lkn kwa nini yale ya kuwekwa wazi hataki yawe wazi?
 
Nijuavyo mimi ulipelekwa ila Kwakuwa ni Bunge hamlisikiliza ndio sababu ya swali lako
 
Kwenye bandari hata Mimi naungana na Kafulila
Palikuwa na urasimu sana pale ila Leo kwakweli acha Samia aongoze tu hata kama mpaka 2035 ni sawa tu
Ni kweli ila wasomi watanzania waliopewa walikuwa na tatizo gani?

Kwa sababu walishindwaje kufikia lengo ,au ndiyo Yale ya kufanya kazi kwa mazoea

Bakhresa ana timu ya watu wataalamu ni sehemu ya wafanyakazi wake ...Inawakuwaje serikali Ina watu lakini wanashindwa wanakuja kusifia private?
 
Tatizo la Watanzania sisi ni majizi kwa asili,
Zamani watu wa Bandari walikuwa na majina sana mjini lakini kumbe walikuwa wanashindana kwa kutuibia sisi Watanzania,

Acha Wageni watunyooshe tumezidi ujinga na wizi wa Mali zetu wenyewe
 
Tatizo la Watanzania sisi ni majizi kwa asili,
Zamani watu wa Bandari walikuwa na majina sana mjini lakini kumbe walikuwa wanashindana kwa kutuibia sisi Watanzania,

Acha Wageni watunyooshe tumezidi ujinga na wizi wa Mali zetu wenyewe
Sema baadhi ya Watanzania sio Watanzania wote ni wezi
 
Mkataba gani mwingine wowote umewahi pelekwa Bungeni kujadiliwa? Mkataba ni Siri
 
Hivo Vivuko Viko we wapi?
 
Kafulila anatufungua sana macho namwomba akagpmbee ubunge
 
Kafulila sio Raia
 
Kwenye Vivuko nampongeza sana Kafulila Sasa ni kama Ulaya
Mv Magogoni na Mv Kigamboni vimehujumiwa ili mzenji mwenzetu Bakhresa apige hela
Vivuko vyake ni 500/=
Wakati vivuko vyote vitatu vinafanya kazi hakukuwa na shida..
Pale feri ni ufisadi unaohitaji special audit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…