CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Mkurugenzi wa Ubia nchi Bwana David Kafulila ameiambia ARIDHIO ya TBC kuwa sasa ni rasmi mtu au kikundi chochote chenye uwezo na nia ya kununua na kuendesha vichwa vya treni pamoja na mabehewa ya SGR wanakaribishwa kufanya hivyo Kwa sharti la Ubia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kafulila anasema, kama ilivyo kwa miundombinu mingine ya usafiri na usafirishaji ya Serikalí akitolea mfano wa barabara za Serikali kuna watu wamenunua Mabasi na wanayaendesha na Serikali inapata kodi lakini kubwa zaidi ni Wananchi kupata huduma bora na nzuri tena kwa wakati huku akitolea mfano wa mradi mkubwa kati ya DART na Mbia ambao kwa kiwango kikubwa uko tayari na mabasi zaidi 170 yataletwa kwa kuanzia divyo itakavyokuwa kwa SGR.
Kafulila anasema Serikali inafanya haya ili kuchachusha Uchumi wa nchi (economic stimulus) ambayo ndio hasa sera halisi na makini za Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na kwa sera hizi ndiyo zinaifanya Tanzania kuendelea kusalia kileleni kwa uchumi jumuishi kwenye nchi zote za maziwa makuu na baadhi ya nchi kusini mwa Jangwa la sahara.