Tatizo Kafulila hajui kitu chochote kile kuhusu masuala haya ya Miradi ya PPP hapa Tanzania. Mpaka Sasa, Serikali ya Tanzania tayari imeingia Mikataba mingi tu ya Miradi ya PPP kabla hata Rais Magufuli na Samia waingie madarakani, Je, huyo Kafulila ameshawahi kujiuliza kwamba nchi hii imekuwa ikinufaika Nini na hiyo Miradi ya PPP???
Tayari kuna Mikataba mingi ya Miradi ya PPP kati ya Tz na Makampuni mbalimbali kutoka nchini China, Je, Tanzania mpaka Sasa inanufaika nini kutokana na kuwepo kwa Miradi hiyo ya Ubia Kati ya Tz na China?? Kwanza huyo Kafulila mpaka Sasa anaijua Miradi hiyo ya Ubia ambayo tayari ipo kwenye utekelezaji tangu miaka mingi iliyopita??
Kafulila aache kupiga Domo na kupiga Propaganda za Siasa kuhusu suala hili la Miradi ya Ubia Kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kwani hili ni suala gumu ambalo liko nje ya uwezo wake wa akili, na hata kwenye hii Serikali iliyopo Hakuna Watu ambao wako competent enough wa kuweza kuli-handle suala hili la Ubia. Wengi waliopo hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na masuala haya ya Ubia na jinsi Miradi ya Ubia inavyoweza kutekelezwa kwa kuzalisha faida.