Kafulila: Rais Samia Suluhu kusuka upya mfumo wa Elimu ya Tanzania ni zaidi ya Uamuzi muhimu wowote uliowahi kufanyika baada ya Uhuru

Alikuwa hatari zamani sio Sasa hivi. Amejishusha Kama akina kangi lugola kwa kuwaabudu wanadamu na mwishowe wakapotea. Nafurahi kujisimamia mwenyewe.
Tatizo lenu Chadema sasa kama mtu ameona kitu kizuri asiseme Rais Samia Suluhu amefanya kazi kubwa sana sekta ya elimu ametoa ajira za walimu amejenga madarasa pia amegfanikisha elimu bure
 
#HUU NI USHAHIDI YA ANACHOTAKA KUKIFANYA RAIS,

Ukiona post ya akili lkn kati ya michango 10, wenye akili 1 maanake tatizo ni 90% hivyo kusuka elimu kuokoa taifa sio jambo la kusubiri tena😂

..tatizo wanaokwenda kusuka elimu ya Tanzania wako ktk hiyo 90% uliyosema kwamba wana matatizo / ujinga.🤣
 
😂😂 ndio maana ni muhimu kusuka upya mfumo wa elimu maana hata quality ya mijadala ni kielelezo cha ukubwa wa tatizo. Mtu anaweka researched facts , badala ya kumjibu kwa facts unakuja na matusi ndio uwezo wako unapoishia
"62% ya utajiri wao ni nguvu kazi."

Nguvu kazi imefanya nini? Maana yake nini?

Wana waajiriwa wengi, au wanapiga sana kazi za msuli au ni ufanisi au ni nini ?
 

..tatizo baada ya yote hayo ni ukosefu wa AJIRA kwa vijana wanaohitimu.
 
Kwa Nini iwe hivyo?

..Kafulila alitakiwa atueleze ni asilimia ngapi ya wahitimu hapa Tz wanapata ajira mara baada ya kumaliza masomo.

..kwa maoni yangu Kafulila amekusanya takwimu na anazutumia kujenga hoja ambayo haiendani na uhalisia wa Tanzania.

..asilimia 60++ ya NGUVU KAZI ya Tanzania wako kwenye KILIMO. Kwa hiyo Kafulila alitakiwa ajenge hoja yake akizingatia ukweli / uhalisia huo.

..Badala yake Kafulila anajenga hoja kwa data zinazoelezea mazingira ya nchi zilizoko ktk hatua tofauti ya kimaendeleo na Tanzania.

..Huyu bwana nimemfuatilia ana tabia ya kusomba takwimu / data na kuzitumia ktk hoja zake bila kuzingatia uhalisia na mazingira ya Tanzania.

..Kunukuu data / takwimu ni jambo moja, na mara nyingi huwa ni jambo jepesi. Tatizo liko ktk kuelewa takwimu zinaeleza nini, na namna sahihi ya kuzitumia.

Cc Mwananchi Huru
 
Umeeleza vizuri Sana mkuu Ila out of topic,

Kafulila anaelezea furaha yake dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan kuufumua mfumo wa Elimu nchini na kuupanga upya,

Lakini amekazia faida ya anachokwenda kufanya Rais kwa mifano toka Mataifa yaliyoendelea,

Sasa hayo mambo ya takwimu za wenye ajira sio Mada hii mkuu,
 
Ajira ni shida ya dunia nzima

..Ni shida ya dunia nzima lakini kwa hapa Tz kiwango cha wasio na ajira ni kikubwa na cha kutisha kuliko mataifa mengi.

..Na serikali ya CCM imeshindwa kuja na mkakati wa kupunguza tatizo hilo, na badala yake imeacha tatizo liongezeke toka awamu moja ya uongozi mpaka nyingine.
 
Hebu lete takwimu za hayo Maeneo mengine
 

..unapozunguzia nguvu kazi ktk muktadha wa elimu bila shaka utakuwa unazungumzia wahitimu wetu ktk soko la ajira.

..halafu "kufumua" mfumo wetu wa elimu na "kuupanga upya" maana yake ni nini?

..Hebu tutolee mfano mmoja wa kitakachofumuliwa, jinsi kitakavyopangwa upya, halafu utueleze malengo na matarajio ni nini.
 
Mfano,

Watoto wote watasoma Mpaka kipato cha nne kwa lazima, Then atakayefauli ndio ataendelea na masomo
 
Je huo Mfumo wa Elimu inasukwqje?
Nasoma mipasho tu huku, mbali zaidi hata seniors wanaandika ngongera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…