Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre), David Kafulila, amesema mafanikio ya taifa hayawezi kupimwa kwa ukubwa wa miradi ya miundombinu pekee, bali kwa uwezo wa wananchi kutumia fursa hizo kuzalisha, kubuni na kuboresha maisha yao.
Kafulila amesema uwekezaji wenye thamani zaidi kwa taifa ni ule unaomjenga mwananchi kuwa rasilimali yenye uwezo wa kuchochea uzalishaji na kuleta suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa.
Kafulila alitoa kauli hiyo jana, Agosti 14, 2026, wakati akizungumza mbele ya mamia ya wakufunzi na wanafunzi katika Mhadhara wa Umma uliofanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), jijini Arusha.
Katika mhadhara huo, Kafulila alirejea misingi ya falsafa ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akisema Tanzania ilianza safari yake ya maendeleo kwa kuweka mwananchi katikati ya mapambano ya kujenga taifa.
Kwa mujibu wa Kafulila, mtazamo huo ulionekana wazi katika hotuba ya Mwalimu Nyerere ya mwaka 1958 mbele ya Baraza la Umoja wa Mataifa (UN), ambapo alieleza kuwa harakati za Watanganyika kudai uhuru hazikutokana na chuki dhidi ya Waingereza, bali zilichochewa na haja ya kuondokana na matatizo yaliyokuwa yakikwamisha maendeleo ya watu.
Alisema matatizo hayo yalijumuisha ujinga, maradhi na umaskini, ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kama vikwazo vikubwa vya maendeleo ya jamii.
Kafulila alisema falsafa hiyo ya kumweka mwananchi mbele imeendelea kuwa sehemu muhimu ya mjadala wa maendeleo duniani, ikiwemo katika mabadiliko kutoka Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) kwenda Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Akizungumzia nafasi ya miradi ya miundombinu inayotekelezwa kupitia ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP), Kafulila alisema miradi hiyo haipaswi kuangaliwa kama majengo au miundombinu pekee, bali kama nyenzo zinazolenga kuongeza uwezo wa wananchi kushiriki katika shughuli za kiuchumi.
Alisema barabara, madaraja, vituo vya usafiri na miundombinu mingine ya kijamii vinapojengwa kwa ufanisi, huondoa vikwazo vya uzalishaji, kurahisisha usafirishaji na kuongeza fursa kwa wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi.
“Maendeleo ya kweli yana maana pale ambapo miundombinu na uwekezaji vinabadilisha maisha ya watu na kuongeza uwezo wao wa kuzalisha,” alisema Kafulila.
Aidha, Kafulila alisema misingi ya maendeleo iliyowekwa na Mwalimu Nyerere imeendelea kuwa rejea katika safari ya Tanzania, huku awamu mbalimbali za uongozi zikiendelea kusisitiza umuhimu wa kukuza uchumi na kuhakikisha matokeo ya ukuaji huo yanawafikia wananchi wengi.
Katika uchambuzi wake, Kafulila alitaja maeneo matatu anayoyaona kuwa nguzo muhimu katika kujenga rasilimali watu yenye tija katika dunia ya sasa; lishe bora, huduma bora za afya na maarifa.
Alisema taifa lenye wananchi wenye afya, lishe inayokidhi mahitaji ya mwili na akili pamoja na maarifa ya kutosha linakuwa na msingi imara wa kujenga uchumi unaoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Kafulila alisisitiza kuwa mwananchi mwenye uwezo huo si mzalishaji pekee, bali pia ni chanzo cha ubunifu na suluhisho katika mazingira ambayo yanaweza kuonekana kuwa hayana matumaini.
Kwa msingi huo, alisema mjadala wa maendeleo ya Tanzania unapaswa kwenda sambamba na uwekezaji katika watu, kwa sababu miundombinu na rasilimali nyingine za taifa hupata maana kubwa zaidi pale zinapotumiwa na watu wenye uwezo wa kuzalisha na kubadilisha fursa kuwa matokeo.
Mhadhara huo ulikuwa sehemu ya mijadala inayolenga kuwajengea washiriki uelewa mpana kuhusu maendeleo, uchumi, ubia kati ya Serikali na sekta binafsi pamoja na nafasi ya rasilimali watu katika kufikia malengo ya taifa.