CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
===
Hatimaye sera za mzee Hashimu Rungwe Sipunda wa chama cha CHAUMA zaanza kupata utetezi wa kisayansi polepole baada ya miaka kumi kupita ( 10 )
Leo tutamuangazia Mkurugenzi Mkuu wa kituo Ubia nchini PPPC Bw David KAFULILA katika moja ya tweete zake huko tweeter X.
Mkurugenzi Kafulila anasema kama Taifa katika mwelekeo wetu mpya wa miaka 25 ijayo ni vema tukaangalia uwezekano wa kuchukua sera nzuri ya Nutritional basics maarufu kama Sera ya UBWABWA mashuleni iliyoasisiwa na mgombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 toka Chama Cha Ukombozi wa Umma Wakili Msomi Hashimu Rungwe Sipunda.
Cde Kafulila anaonesha tatizo la Utapiamlo duniani na Tanzània ikiwemo ni kubwa pamoja na yote linaigharimu dunia mabilioni ya Shilingi katika kupambana nalo akitolea mfano kuwa mpaka mwaka 2025 zaidi ya $18bn ambazo ni zaidi ya TZS 45 Trilioni zitatumika kupambana na Utapiamlo duniani Tanzania yetu ikiwemo.
Bila kujali hoja hii imetoka Upinzani au chama rafiki bado ni hoja mtambuka kwa Ustawi wa Taifa letu na Watanzania wa leo na kesho kwenye hili nampa Kafulila kongole nyingi kwa wivu wake mkubwa juu ya maisha ya Watanzania hasa watoto wanaotoka kwenye familia duni.