Pamoja na kufahamu hayo ninafahamu pia kwa mlipa Kodi kuna mambo ambayo anatakiwa apate kutokana na kodi yake na sasa hivi Matozo yamekuwa mengi bila value for money zaidi ya kulishwa propaganda na watu kuwa madalali na machawa tu..., Busy Talking the Talk.....
Kwamba mpaka leo hatuna DIRA theoretically ? (Sababu practically hatuna ndio maana kila siku kila anayeamka anakuja na ngonjera zake na kuleta vitu abstract wala visivyoeleweka).., Issue sio kuwa na maandiko mazuri bali issue ni kufanyia kazi vilivyopo na kuvifanya...
Vilevile kwa nchi ambayo watunga Sera wamekuwa madalali unategemea wanaweza kufanya lolote zuri ambalo hawana faida nalo kifedha ? Case in Point nimekuletea hapo Juu, kuhusu nishati ya kupikia
- Misaada imetoka dunia nzima kwahio kuna fedha lukuki
- Badala ya kuhimiza umeme ambao tunao hawa jamaa wamekuwa madalali wa kupigia chapuo gesi ambayo ina gharama kwa watu wapikie na wanawakataza kuni ambazo wangetumia bure
- Mbaya zaidi wanakwenda kutafuta watoa mlungula kina Adani ili waje wasambaze umeme (ambao wanasema hautoshi) ili bei za umeme zizidi kupanda hivyo kumuumiza mwananchi
Unadhani hawa mchwa wasio na uchungu na taifa bali matumbo yao kama ndio tunawaachia wawe na tochi ya kumulika wapi tunakwenda watatupelekea wapi ?
Sheria ? Sheria ambazo zinavunjwa kila dakika (kwahio hata ukisema liwe kama sheria wakati kuna vitu vipo wazi hata kipofu anaona utagundua kwamba haya yote ya Michakato ni Miradi ya kuendelea kupiga Kodi zetu)
Hakuna jipya hapa bali kuendelea recycling maneno ambayo hayafanyiwi kazi zaidi ya kujilipa pesa za kuleta maandiko / mawazo na kufanya propaganda na maigizo yasiyofurahisha wala kumsaidia yoyote...; Badala ya kubwabwaja waanze kufanya kama wameona watu lishe ni mbovu na pesa kila siku tunazitoa kwanini wasipeleke hio lishe leo au jana ?