Kafulila: Serikali inakopa T-bills kwa 5% wakati Msumbiji 17%, Kenya 16%, Malawi 16%, Zambia 10%, Namibia 9%, Uganda 9%, SA 8%. Uelekeo wetu ni sahihi

Unazungumzia nini T-bills ndio Mdudu gani mboni tunachanganyana?
Kwani ujasoma kichwa cha habari kinazungumzia nini.

T-Bills (Treasury Bills) ni short loans za serikali malipo yake ndani mwaka.

Usichanganye na treasury bonds and notes hizo zina time frames tofauti usually 2 years plus.
 
Kwani ujasoma kichwa cha habari kinazungumzia nini.

T-Bills (Treasury Bills) ni short loans za serikali malipo yake ndani mwaka.

Usichanganye na treasury bonds and notes hizo zina time frames tofauti usually 2 years plus.
Hapo sasa nimeelewa nikajua TTCL Bills
 
Hapo sasa nimeelewa nikajua TTCL Bills
Wewe unaweza amini hiyo variation ya Kafulila kwenye huo upuuzi alioandika.

Yaani SA yenye credit rating ya A1 (low default risk) itoe riba kubwa kushinda Tanzania B1 (Junk bond). Nani ataacha kwenda kununua SA.

Uoni kama huyo mtu ujinga wake unapitiliza sasa anaanza kujiandika mambo asiyoyaelewa.
 
Ni ruksa kwa CPA hapa kutoa maoni. Wengine tunapita tu na kushangaa.
Nimeshindwa hata kuweka like au mshangao maana kwangu maoni haya ni kama hadithi za Abunuas.
 
Hapa nimeshindwa kuvumilia. Jibu langu rahisi: Msikilize mama hotuba yake alipokuwa anapokea Gawio Juzi.
Alisema: Walitupandisha daraja (uchumi wa kati), mwakani watakuja tena kufuatilia kama bado tupo ktk viwango. Kama wakituthibitisha katika daraja hilo HII MIKOPO KWA MASHARTI RAHISI NA RIBA NDOGO HAITAKUWEPO TENA.

Iko hivi- hata wewe unaweza ukamchangia bureee masikini au omba omba buku 5 au zaidi. Lakini mwalimu mkuu akikuomba buku tano, pengine utamuuliza- utalipa lini pengine utaweka na riba juu.
 
Tumbili wewe ni mnufaika wa moja kwa moja wa mikopo hii ya serikali! Msitutie ujinga huo, serikali kwa sasa haina uwezo wowote tena wa kutoa huduma za kijamii kwa wananchi kama ilivyokuwa hapo awali, kilakitu ni wananchi tu kujilipia! Fedha yote ya serikali kwa sasa inaelekezwa kwenye kulipia madeni, nyinyi Ndo mnazidi kuyashambikiahsyo madeni! Na kwanini kila anayetetea deni la taifa lazima apate uteuzi? Nani sasa ataiambia ukweli serikali?
 
Shida yao ni kupenda kusema uongo, na njia ya mtu muongo uwa ni fupi ndio maana maelezo yake hayakuwa consistent.

Nchi kwa sasa ipo uchumi daraja la chini, yeye mwanzo alitaka kutuaminisha tupo kwenye middle income.

Baadae akaanza kujichanganya kwenye maelezo kwa sasa tunapata mikopo rahisi kwa sababu ni least developed nation (maana yake hatupo kwenye middle income).

Mwakani kuna tathmini nyingine hiko mbeke tunaweza panda kuwa middle income, hizi fursa za sasa zitapotea (mikopo rahisi) ya maendeleo ya jamii.

Ashukuru nchi anayoongoza ni Tanzania ingekuwa hata Kenya tu hapo, hiyo inconsistent yake media wasingeacha ipite raisi anaongea story isiyo make sense vile.
 
Wewe ndio umejichanganya. Ni hivi- unapoanza kazi kuna kipindi cha kutazamiwa kabla hujathibitishwa. Hivyo TZ sasa hivi tupo kwenye middle income lakini bado hatujathibitishwa, hivyo bado tunachukuliwa katika daraja lile tulilokuwa nalo kabla.
Habari ya kupandishwa katika daraja la middle income ilitolewa na IMF, sio na Samia. Samia ananukuu tu maneno ya hiyo taasisi kubwa duniani. Google utaipata.
 
Sasa kwanini alisema tukifanyiwa tathmini mwakani tukapandishwa daraja kuwa middle-income hizi fursa za mikopo ya least developed nations itapotea?

Halafu sioni ata huo uhusiano wa alichosema ‘bi-tozo’ na hii hoja ya Kafulila kwenye hii mada. Yeye alikuwa anaongelea mambo ya misaada, Kafulila anaongelea money market instruments; vitu viwili tofauti hata sijui kwanini unavifananisha.
 
Acha mawazo mgando, kama wewe ni mmoja wa viongozi huko serikalini, inabidi upishe wengine wenye uelewa wa namna bora ya kutukwamua na kausha damu bila kukinga bakuri kila sehemu ( Ni fedheha). Waachieni wengine walete mawazo mbadala, mnangangania kuwemo tu huki ili hali akili zenu zimedumaa na kusinyaa tayari. Tuko zaidi ya million 60 na hamuwezi kuwa na monopoly ua ideas kwamba mo lazima kukopa... uwezo wetu wa kuilipa hiyo mikopo upoje au ndio yale yale ya kukabidhi maliasili zetu kwa wageni kama collateral? acheni hizi mambo ya kushabikia mikopo. Binafsi, sijui hata kama wewe umeisha wahi kuwa na credit card na ukajua ivyofanya kazi.. mikopo ni utumwa ndugu yangu.
 
Tatizo la sio ukopaji tatizo ni vipaumbele ya hiyo mikopo na usimamizi wa hizo fedha asilimia kubwa fedha za mikopo zinafanyiwa ufisadi na nchi inabebeshwa zigo la deni
 
Sio Sifa ila hata familia yako kama unataka kuwa tajiri kuwazidi wengine lazima ukope, Bakresa pia analoan kibao kwenye mabenki
Sikatai ila kopa ukiwa na watu wenye uchungu na huo mkopo ..sasa ww kila siku utasikia kuna wilaya wamepiga billions kadhaaa na huyo huyo mwizi adhabu yake ni kuhamishwa kituo cha kazi ama kupangiwa kazi nyingine.
 
Ni Tz tu mtu kama Kafulila anaweza kupayuka payuka mambo asiyoyafahamu undani wake na watu wakaamini anajua..ana tabia ya kusoma soma magazeti na taarifa za mitandaoni na kudhani vinampa ujuzi wa kueleza kama anavyosoma..ni vitu vya kukariri tu, hajawahi kufanya analysis yoyote ya kiuchumi au mambo ya fedha inavyotakiwa, kupitia maandiko(makala)..issue ya mikopo kupitia hati fungani huwezi itenganisha na kiwango cha mfumuko wa bei na hata kiwango cha ubadilishaji fedha za kigeni kwa nchi husika dhidi ya nchi nyingine..bei ya hati fungani Kenya au Mauritius haiwezi kufanana au kulingana, na si kweli kwamba ukiona bei ya hati fungani Mauritius iko juu kwa maana ya tarakimu, haimaanishi kwamba bei ya hati fungani Kenya iko chini..tafsiri yake inaweza kuwa bei ya hati fungani Mauritius ni ya chini zaidi ya ile ya Kenya pamoja na kwamba ki-tarakimu inaonekana iko juu zaidi ya ile ya Kenya..ni kwa sababu viwango vya mfumuko wa bei na ubadilishaji fedha za kigeni unatofautiana kati ya nchi hizi mbili.
 
Hiyo nafasi anayoivizia ya mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu inataka cool headed.

Anaropoka na kujaza machawa humu mpaka anaanza kuonekana mtu wa hovyo sasa.
Inaonyesha wewe una chuki binafsi . Maana kila mtu anafahamu vyema kabisa namna Mh Kafulila alivyo mtulivu,mwenye uwezo mkubwa wa kujenga na kutetea hoja pamoja na uchapakazi uliotukuka. Lakini vilevile Mh Kafulila ni kiongozi mbunifu na mwenye uelewa na ufahamu wa masuala mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…