Kafulila: Uchumi wa dunia ni US$ 105trilion 97% ni deni kukopa na kujenga ndio mpango mzima Duniani

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
1,588
Reaction score
956
IMG-20240610-WA0013.jpg

David Kafulila, Mkurugenzi wa PPP TANZANIA katika ukurasa wake wa tweeter ( X ) amechambua haya kwa kifupi

Kafulila anasema, kukopa kwajili ya miradi ya maendeleo ndio njia sahihi na ndio mpango wa dunia nzima kwa sasa.

Kafulila anatufumbua macho kwamba nchi zote kubwa duniani tunazoziona zikimea zinajengwa kwa mikopo kwa wastani wa 97%

David anasema, wakati uchumi wa dunia umefikia US$ 105trilion, Deni lote la dunia ( serikali & private ) ni US$ 315 trilion.

Kwa lugha nyepesi, Sasa deni la serikali zote duniani ikiwemo ya Rais Samia limefikia US$ 97trilion sawa na 97% ya uchumi wa dunia,

Kafulila anazidi kufafanua kuwa deni lote la dunia kwa ujumla ni US$ 315 Trilioni ambalo ni zaidi ya 300% ya GDP ya dunia.

Vietnam ni nchi ya mfano duniani kwa muujiza wa kukuza uchumi ndani ya muda mfupi,

Mwaka 1990, uchumi wa Vietnam ulikuwa US$ 6.4bilion, mbele kidogo ya Tanzania iliyokuwa na US$ 4.5bilioni na nyuma ya Kenya iliyokuwa na US$ 8.4bilioni,

Lakini Leo miaka 30 baadae, uchumi wa Vietnam ni US$ 400bilion, karibu mara nne ya Kenya na mara tano ya Tanzania.

Hata hivyo, Mwaka 2007, wakati uchumi wa Vietnam ukiwa US$77bilion, sawa na Tanzania leo,

Mwaka huohuo wa 2007 uwiano wa deni kwa uchumi Vietinum ulikuwa asilimia 43% karibu sawa na uwiano wa deni kwa uchumi wetu Tanzania Leo.

Kukopa kujenga uchumi ndio njia na ndio Afya yenyewe ya nchi anasema David Kafulila.
 
Samia awe makini na PPP za Kafulia, naona zinamgeuza kuwa dalali, kwa hiyo muda mwingi mali za nchi anazipigia debe "kariakoo mia kariako mia......". (Sehemu ya kariakoo chagua raslimali ya taifa, sehemu ya mia, jaza fedha ambayo kafulia anaitia hao pipi (PPP)wake)
 
mama akizid kumsikiliza huyu mtu tunatumbukia kwenye madeni makubwa
 
Samia awe makini na PPP za Kafulia, naona zinamgeuza kuwa dalali, kwa hiyo muda mwingi mali za nchi anazipigia debe "kariakoo mia kariako mia......". (Sehemu ya kariakoo chagua raslimali ya taifa, sehemu ya mia, jaza fedha ambayo kafulia anaitia hao pipi (PPP)wake)
Dalali ndio nini? How?
 
Kukopa kwa sjili ya uwekezaji wa mindumbinu inayozalisha Tena Kwa interest kidogo haina shida kabisa Wasiwasi wa wengi ni kuwa wasimamizi wengi ni weI hivyo wasiwasi kuwa fedha zinakopwa harafu zinaishia pabaya badala ya kufanya kazi iliyokusudiwa.
 
Dalali ndio nini? How?
Hivi unatafuta muwekezaji katika barabara ya Moro-Dar wakati asilimia kubwa ya mkoa wa morogoro ni pori la serikali? Ni suala la serikali kuita idara ya misitu kuwaambia tunapanua barabara, eti unaita PPP ya trilioni nzima. Moro Dar kilometa 190, ukijenga kila kilometa kwa bilioni moja,.njia mbili, bilioni mia tatu au mia nne hivi na ushee. Hizi ndio za kuitia muwekezaji? Hata ukijenga kwa awamu, mwaka huu kilometa 200, unaofata kilometa 200.

Sehemu za mkoa wa Pwani zenye maendelezo barabarani zikafidiwa. Nazo zikajengwa njia nne
 
===
David Kafulila, Mkurugenzi PPP TANZANIA katika ukurasa wake wa tweeter ( X ) amechambua haya,

Kafulila anasema, kukopa kwajili ya miradi ya maendeleo ndio njia.

Nchi zote kubwa duniani mnazoziona zikimea zinajengwa kwa mikopo kwa wastani wa 97%

David anasema, wakati uchumi wa dunia umefikia US$ 105trilion, Deni lote la dunia ( serikali & private ) ni US$97.

Kwa lugha nyepesi,deni la serikali zote duniani limefikia US$ 97trilion sawa na 97% ya uchumi wa dunia,

Kafulila anasema deni lote la dunia kwa ujumla ni US$ 315 Trilioni zaidi ya 300% ya GDP ya dunia.

Vietnam ni nchi ya mfano duniani kwa muujiza wa kukuza uchumi ndani ya muda mfupi,

Mwaka 1990, uchumi wa Vietnam ulikuwa US$ 6.4bilion, mbele kidogo ya Tanzania iliyokuwa na US$ 4.5bilioni na nyuma ya Kenya iliyokuwa na US$ 8.4bilioni,

Lakini Leo miaka 30 baadae, uchumi wa Vietnam ni US$ 400bilion, karibu mara nne ya Kenya na mara tano ya Tanzania.

Hata hivyo, Mwaka 2007, wakati uchumi wa Vietnam ukiwa US$77bilion, sawa na Tanzania leo,

Mwaka huohuo wa 2007 uwiano wa deni kwa uchumi ulikuwa asilimia 43% karibu sawa na uwiano wa deni kwa uchumi wetu Tanzania.

Kukopa kujenga uchumi ndio njia anasema David Kafulila.

View attachment 3011554
Kafulila Yuko mbele yenu sana ila bado kidogo mtamuelewa tu
 
Hivi unatafuta muwekezaji katika barabara ya Moro-Dar wakati asilimia kubwa ya mkoa wa morogoro ni pori la serikali? Ni suala la serikali kuita idara ya misitu kuwaambia tunapanua barabara, eti unaita PPP ya trilioni nzima. Moro Dar kilometa 190, ukijenga kila kilometa kwa bilioni moja,.njia mbili, bilioni mia tatu au mia nne hivi na ushee. Hizi ndio za kuitia muwekezaji? Hata ukijenga kwa awamu, mwaka huu kilometa 200, unaofata kilometa 200.

Sehemu za mkoa wa Pwani zenye maendelezo barabarani zikafidiwa. Nazo zikajengwa njia nne
Hayo uliyoeleza yanahusianaje na PPP? Kwani kuliwa na msitu ndio inakuaje? Barabara si ni ya kulipia au? Mbona hueleweki.

Mwisho PPP kampuni zinajilipa Kulingana na Watumishi sio Mkopo wa Serikali
 
Samia awe makini na PPP za Kafulia, naona zinamgeuza kuwa dalali, kwa hiyo muda mwingi mali za nchi anazipigia debe "kariakoo mia kariako mia......". (Sehemu ya kariakoo chagua raslimali ya taifa, sehemu ya mia, jaza fedha ambayo kafulia anaitia hao pipi (PPP)wake)
Unataka kumfundisha kazi Rais?

Jenga hoja acha maneno maneno,

Kama Dunia nzima inakopa sisi kelele za nini?

Kwani sisi ni akina nani?

Au mnataka tuuze rasilimali za nchi ili kujenga miradi?

Watanzania hatujulikani tunataka nini?

Kodi hatutaki kulipa Mikopo hatutaki Sasa nchi ijiendeshe kwa malikauli?
 
Hayo uliyoeleza yanahusianaje na PPP? Kwani kuliwa na msitu ndio inakuaje? Barabara si ni ya kulipia au? Mbona hueleweki.

Mwisho PPP kampuni zinajilipa Kulingana na Watumishi sio Mkopo wa Serikali
Very good PPP, Ni uwekezaji,

Na sio lazima kupita kwenye hizo njia,

Ila zitawasaidia hasa wenzetu wa nchi za Uganda, Rwanda, Kongo etc
 
Hayo uliyoeleza yanahusianaje na PPP? Kwani kuliwa na msitu ndio inakuaje? Barabara si ni ya kulipia au? Mbona hueleweki.

Mwisho PPP kampuni zinajilipa Kulingana na Watumishi sio Mkopo wa Serikali
Usitumie kichwa kubebea kamasi, hiyo barabara ya Dar Moro ijengwe na serikali yenyewe bila PPP, PPP ichukue miradi mikubwa ya kiuchumi. Haizidi bilioni 500 kuifanya iwe ya kisasa
 
Atafaa sana akipewa ukurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu.kwa sababu anafahamu vyema Dunia inakwendaje na ni mtu anayesoma na kujisomea sana na hivyo kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali.jambo ambalo ni la muhimu sana kwa mtu anayekuwa kwenye nafasi ya ukurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu.
 
Back
Top Bottom