Kafulila: Uchumi wa dunia ni US$ 105trilion 97% ni deni kukopa na kujenga ndio mpango mzima Duniani

Kafulila: Uchumi wa dunia ni US$ 105trilion 97% ni deni kukopa na kujenga ndio mpango mzima Duniani

Namna ipo ila wafanya maamuzi ndo viziwi hawataki kusikia wanaona njia pekee ni mikopo wakati wangeweza kupunguza matumizi yao mfano posho na mishahara ya wanasiasa (bunge) manunuzi ya magari ya kifahali kila mwaka kuziba mianya ya ufisadi kwa kuweka sheria kali kwa atakayebainika kujihusisha na rushwa na matumizi mabqyq ya mali za umma
Na ndio wizi wenyewe huu; kuhalisha matumizi ya ovyo.
 
View attachment 3012355
David Kafulila, Mkurugenzi wa PPP TANZANIA katika ukurasa wake wa tweeter ( X ) amechambua haya kwa kifupi

Kafulila anasema, kukopa kwajili ya miradi ya maendeleo ndio njia sahihi na ndio mpango wa dunia nzima kwa sasa.

Kafulila anatufumbua macho kwamba nchi zote kubwa duniani tunazoziona zikimea zinajengwa kwa mikopo kwa wastani wa 97%

David anasema, wakati uchumi wa dunia umefikia US$ 105trilion, Deni lote la dunia ( serikali & private ) ni US$ 315 trilion.

Kwa lugha nyepesi, Sasa deni la serikali zote duniani ikiwemo ya Rais Samia limefikia US$ 97trilion sawa na 97% ya uchumi wa dunia,

Kafulila anazidi kufafanua kuwa deni lote la dunia kwa ujumla ni US$ 315 Trilioni ambalo ni zaidi ya 300% ya GDP ya dunia.

Vietnam ni nchi ya mfano duniani kwa muujiza wa kukuza uchumi ndani ya muda mfupi,

Mwaka 1990, uchumi wa Vietnam ulikuwa US$ 6.4bilion, mbele kidogo ya Tanzania iliyokuwa na US$ 4.5bilioni na nyuma ya Kenya iliyokuwa na US$ 8.4bilioni,

Lakini Leo miaka 30 baadae, uchumi wa Vietnam ni US$ 400bilion, karibu mara nne ya Kenya na mara tano ya Tanzania.

Hata hivyo, Mwaka 2007, wakati uchumi wa Vietnam ukiwa US$77bilion, sawa na Tanzania leo,

Mwaka huohuo wa 2007 uwiano wa deni kwa uchumi Vietinum ulikuwa asilimia 43% karibu sawa na uwiano wa deni kwa uchumi wetu Tanzania Leo.

Kukopa kujenga uchumi ndio njia na ndio Afya yenyewe ya nchi anasema David Kafulila.
View attachment 3011554
Jambo moja kubwa Kafulila ananifurahisha ni kuwachana watu ukweli black and white kwamba Mikopo ndio mpango mzima
 
Jambo moja kubwa Kafulila ananifurahisha ni kuwachana watu ukweli black and white kwamba Mikopo ndio mpango mzima
Unamwona shujaa kwa uwakala wake huo?
Kwani hiyo mikopo unaona kasi ya ongezeko lake na maendeleo viko sawa kama wakati wa jiwe?
 
Unamwona shujaa Wakati wa jiwe ilikuwa ni hatari zaidi kwani hata yeye alikuwa anakusanya pesa kwake Kwa maelezo ya Lissu. uwakala wake huo?
Kwani hiyo mikopo unaona kasi ya ongezeko lake na maendeleo viko sawa kama wakati wa jiwe?
Wakati wa jiwe ilikuwa ni hatari zaidi kwani hata yeye alikuwa anakusanya pesa kwake Kwa maelezo ya Lissu.
 
Back
Top Bottom