Kafulila: Uchumi wa dunia ni US$ 105trilion 97% ni deni kukopa na kujenga ndio mpango mzima Duniani

Ufafanuzi mzuri sana David, Tuendelee kuipigania nchi yetu
 
Uchambuzi mzuri sana huu, Nimefurahi,
 
Kama deni la dunia ni $315 trillion na katika hilo madeni ya serikali $97 trillion; kwa asilimia madeni ya serikali ni 30.8% na private debt 69.2%. Maana yake nini private sector ndio inakuza uchumi sio serikali.

Tanzania kwenye deni la taifa $77 billion kwa mgawanyo wa asilimia kwa mujibu wa imf private debt ni 12.5% na government 87.5% na serikali aizalishi kwa ratio hiyo uchumi sijui unakuwa vipi kwa kasi.

Mbaya zaidi jukumu kubwa la serikali za third world ni kujenga key infrastructure za kuchochea uzalishaji (kama vile kuweka umeme wa uhakika) na kujenga network infrastructure za usafirishaji mainly barabara na railway. Kama nchi Tanzanian tuna struggle huko.

Asilimia kubwa ya mikopo yetu ni kwa seminar za maendeleo au tunakopa kuvunja Hospitali ilikujenga mpya (you hope hawapo serious kutaka kuivunja muhimbili) katika nchi ambayo ina uhaba wa makazi hayo majengo yanaweza geuzwa apartments na hiyo hospitali ikatafutiwa eneo lingine.

Muhimbili interms of bed capacity si ajabu ikawa katika top 10 ya hospitali kubwa kwenye bara la Africa, viongozi watanzania wapo tayari kuivunja. Akili zetu watanzania zinatutosha wenyewe.
 
Ndio maana Kafulila anasisitiza UBIA
 
Issue hata sio kukopa, suala ni je hiyo pesa inayokopwa inapelekwa kwenye mtumizi yaliyokusudiwa kwa usahihi? Na kingine cha muhimu zaidi kuna mikakati thabiti iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha hiyo pesa inajizalisha hili kulipa deni pasipo kutuingiza kwenye hatari yoyote huko mbeleni?

Isije ikawa tunakopa kopa tu pasipokuwa na mikakati maalumu kama wale wamama wa uswahilini ambao kila siku wanakopa kausha damu kisha hela wanazipeleka kwenye shughuli au kufanyia birthday party watoto wao, halafu ukifika wakati wa marejesho wanaanza kusumbuana na maafisa mikopo na hatimae kubebewa vitu vyao.
 
Ni sahihi kabisa Mikopo lazima ipelekwe kwenye imekusudiwa
 
Naunga mkono mikopo ichukuliwe kulingana na mahitaji husika
 
Kuwa makini na comment zako pia
 
Halafu huyu na mahesabu yake hayo anamchanganya huyu mama tutalia ohoo
 
Wengi sana wanakubali ukweli kuwa Mheshimiwa Kafulila ni jembe.

Kwa haraka haraka unaweza kudhani ameongea mambo muhimu, lakini ni siasa na upotoshaji

Hakuna anayekataa kukopa! hoja ni kwamba kwanini tunakopa, ili iweje na kwa faida gani.

Mwaka 1961 tulikuwa sawa na Korea kusini
Miaka ya 1980 kukatokea akina Asian Tiger wakiwemo hao Viet Nam
Mwaka 1977 tulikuwa na China katika mkutano Arusha wa ' group 77''

Tanzania ni nchi iliyonufaika na misaada ya nchi za Magharibi kwa miaka zaidi ya 50
Tanzania ina arable land, ina madini , uoto wa asili, utalii, mito maziwa na bahari
Tanzania imekopa kuanzia Uhuru hadi iliposaemehewa ''HIPC''

Ukitazama hapo juu utajiuliza tunakwama wapi ukilinganisha na wenzetu? Kwanini tunahitaji mikopo ikiwa hatukuweza kutumia misaada na mikopo ya awali kujikwamua?

Kafulila aeleze umma haya
1. Bajeti ya Bunge kwa mwaka mmoja ni kiasi gani.
2. Mbunge wa Viet Nam anakipato gani ukimlinganisha na wa Tanzania katika chumi mbili tofauti
3. Bajeti ya kununua V8 , 500 inatoka wapi? v8 hizo zinachangia vipi kuinua uchumi wa nchi
4. Inawezekanaje nchi yenye kila mamlaka ipoteze zaidi ya Trilioni 1 kwa mwaka (CAG)
5. Tunatumia kiasi gani cha bajeti kuhudumia Wastaafu, na kwanini UK, Sweden na kwingine hawana gharamza hizo
6.Kwanini Waziri wa Uingereza atumie Taxi sisi tukiwa na V8 hata kwa Wakurugenzi tu wa idara?
7. Tuliwezaje kutumia Bilioni zaidi ya 200 kwa jambo lililoshindikana kama mchakato wa Katiba! ikiwa pesa hizo ni za mkopo tumezirudisha kwa utaratibu gani
8. Kwa miaka 10 iliyopita ni kiasi gani kimepotea kwa wizi kutokana na taarifa ya CAG


JokaKuu
 
Kazi kwelikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…