Kafulila: UNDP imetoa orodha ya nchi 54 duniani zilizoelemewa na deni la Taifa. 25 zinatoka Afrika Tanzania haipo, tukope zaidi tujenge Uchumi zaidi

Mkuu ili hoja yako iwe na mashiko ebu tutajie walau Nchi tatu zilizoendelea Duniani bila kukopa?
Zilikopa ili zifanye nn trillion 90+ tangu uhuru ebu ainisha vipau mbele vilivyotekelezwa

Nyerere tuliona maendelea viwanda, program ya azimio la arusha kuwezesha siasa ya ujamaa na kujitegemea

Awamu nyingine nn umeona barabara na fly over, maji shida, umeme shida mishahara kwa watumishi shida, pembejeo kwa wakulima zinepanda, bei za vyakula na maisha juu hiyo trillion 26 waliokopa iko wp

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Kafulila Ana tatizo mahali, kwanini asikubali kua Zama ke zimepita? Hivi hajifunzi kwa Akina Makonda na hapi? Wameamua kukaa kimya kuendelea na mambo yao
 
Kafulila ana shindwa kujua WB iko strategically,miradi yao mingi imeelekezwa huku watatuwekaje kwenye orodha hiyo!!!

Ukishaonja cake ya wachache lazima uharibikiwe akili,unadaiwa tillion 95 then unaropoka mropoko mkubwa kama huo, kweli!!!
 
Sasa kama wananchi wanalalamika umeme,ukaanzisha project kubwa ya umeme wa upepo eneo kama singida watu si wanalipa bill, ikatumika kulipa den na kufanya maintenance na watu wakapata ajira sasa apo kuna asara gani
Hasara ni kwamba huyo aliyekukopesha atakuendesha kama gari bovu,na atakufanya mfanyie vitu vingi at your disadvantage vya hasara hasara tu,wewe si mtumwa wake?Halafu mind you,hata ulichokopa kingi kitarudi kwake kimkakati!

Tunajua kwa kuwa tulikuwa huko.Unashangaa 60% ya mkopo imerudi kwake,na anayelipa ni wewe.Ninyi hamjui yanayoendelea,nia ya mikopo ni kufukarisha mkopaji in style.Mlioko nje ya mifumo ya serikali mnapewa lugha tamu tamu tu mkiamini ni kweli.Mikopo ni biashara,tena kwa mkopaji biashara kichaa,Tena kichaa kweli kweli.
 
Hakuna njia rahisi ya kufanikiwa kama Kwa kukopa kama utakuwa na strategies za maana, tatizo ni pale unapokopa unaenda kujenga shule afu unataka wanafunzi wasome bure, umekupa fanya vitu vitakavyoingizia taifa pesa nyingi Kwa muda mfupi kama bandari alafu serikali ipunguze vitu vya bure
 
Hivi chawa ana faida gani kwenye ecosystem kweli?!!
 
Uteuzi kuupata labda ahera. Time yako imeisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…