Kafulila: UNDP imetoa orodha ya nchi 54 duniani zilizoelemewa na deni la Taifa. 25 zinatoka Afrika Tanzania haipo, tukope zaidi tujenge Uchumi zaidi

Mara nyingi na kwa uzoefu wangu Pesa nyingi zinazopotea Ni Pesa za makusanyo ya ndani..

Pesa ya mkopo hata ikipoyea Ni kwenye utekelezaji wa mradi aidha ku overprice au kujenga chini ya kiwango.

Mbona kwa Sasa tunalipa mishahara kwa mikopo?. Hakuna issue hapo.
 
Kumbe Japan 40% ya bajeti yake ni deni Daaah,

Asante Sana Mkuu Kafulila kutufumbua macho,
Hivi Bakhresa akiwa na 40% ya bajeti yake kuwa deni, wewe kapuku utatumia hiyo taarifa kujipa moyo juu ya madeni unayodaiwa dukani na Mangi?

Vv
 
Huyu atakuwa anaumwa ugonjwa wa akili ama anajitoa ufahamu kwa sababu anazozijua mwenyewe. Kudaiwa ni utumwa sio sifa
Acha kuzungumzia hivi videni vya kwa Mangi, Hivi mtu anakukopesha kwa riba ya 1% kwa miaka 20 unakataaje hiyo pesa?
 
Kafulila atakuwa amefulia kweli kweli 😂
Kukopa sio sifa na hasa kama mikopo hiyo inanufaisha ukoo wa panya, mchwa na mafisadi!.

Kwamba hatukuorodheshwa hivyo tukope tu eti deni letu ni stahimilivu? 🤔
 
Kafulila atakuwa amefulia kweli kweli 😂
Kukopa sio sifa na hasa kama mikopo hiyo inanufaisha ukoo wa panya, mchwa na mafisadi!.

Kwamba hatukuorodheshwa hivyo tukope tu eti deni letu ni stahimilivu? 🤔
Kafulia kweli kweli !! Vita vya Ukraine sio mchezo !!
 
Kwamba tuingie kwenye hiyo list sio?
 
Ninachomkubali Kafulila huwa tukikutana naye rafiki zake, wakati tunapiga stori huwa anamponda sana mama, ila huku mitandaoni anajikosha kuwa anampenda. Siku moja nitam record nilete hapa.
 
Naona Jamaa anajitahidi sana kuchonga mizinga nyuki waingie aanze kulamba asali lakini inaonekana mizinga yake ina moshi nyuki hawawezi kuingia, Labda sasa apambane Kutoa moshi ndani ya mizinga yake nyuki waweze kuingia. Kazana sana atimaye nyuki wataona mizinga.
 
Ukope kujenga uchumi gani?. Uchumi haujengwi kwa mikopo Bali kwa mipango madhubuti na makubaliano ya pamoja Kama taifa.
Acha porojo za kijinga,unaelewa maana ya kujenga njia za Uchumi au unapayuka tuu?

Mipango madhubuti bila nyenzo utakusaidia Nini?
 
Huyu atakuwa anaumwa ugonjwa wa akili ama anajitoa ufahamu kwa sababu anazozijua mwenyewe. Kudaiwa ni utumwa sio sifa
Kwa mafukara wasio na shughuli za kuingiza kipato,kudaiwa ni utumwa,lakini tz hakuna anayemzidi mo dewji kudaiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…