Kafulila: Wawekezaji si wageni tu tumeni maombi yenu PPP-Centre kama unautaka mradi wowote wenye sura ya kibiashara popote kituo Cha Ubia kitawasaidia

Kafulila: Wawekezaji si wageni tu tumeni maombi yenu PPP-Centre kama unautaka mradi wowote wenye sura ya kibiashara popote kituo Cha Ubia kitawasaidia

TWELVE12

Senior Member
Joined
Jun 5, 2024
Posts
135
Reaction score
133
IMG-20240918-WA0072.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi - (PPP) David Kafulila
awataka wananchi kutosubiri tangazo la zabuni za Serikali.

Mkurugenzi Kafulila ameeleza njia nne Sekta ya Umma, Binafsi zanavyofanya kazi pamoja

••••••••••••
Mkurugenzi Mtendaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi - (PPP) David Kafulila amewashauri wafanyabiashara na wawekezaji nchini wasisubiri zabuni za Serikali zitangazwe ili waweze kupata fursa za kazi na badala yake wenyewe waanzishe fursa hizo.

Ushauri huo Kafulila aliutoa katika mahojiano maalumu na Kituo Cha Wasafi Media Cha jijini Dar es Salaam akieleza namna Sekta ya Umma na Sekta Binafsi zinavyoweza kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya kila mmoja.

Kamishna Kafulila alieleza kuwa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ina maeneo manne ambayo yanatoa nafasi kwa pande hizo mbili kuweza kufanya kazi kwa pamoja.

Alisema kuwa njia ya kwanza ni ile ambayo Serikali inahitaji kufanya mradi kwa utaratibu wa ubia, hivyo inauanda mradi husika kwa maana ya kufanya upembuzi yakinifu ambapo itaonesha sifa za mradi za kibiashara, kiuchumi na sifa nyingine.

Kwamba upembuzi huo ukishafanyika, mradi unapelekwa sokoni kwa maana ya kuutangaza ili kampuni binafsi zishindane na kuchukua fursa hiyo, ambapo alieleza kuwa njia hiyo Serikali inaanzisha yenyewe mradi na kuuweka sokoni.

“Njia ya pili ni ile ambayo Sekta Binafsi inaona fursa, kwa mfano inaweza kuwa jinsi ambavyo Serikali inaendesha Reli ya SGR labda kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma, mwekezaji anaweza kusema, ningepewa mimi kampuni binafsi ningeweza kufanya vizuri zaidi ya inavyofanya kwa faida yangu na kwa faida ya Serikali na kwa faida ya umma. Kwa hiyo hii ni ile ambayo Sekta Binafsi yenyewe imeichungulia fursa. Kimsingi fursa inakuwepo,” alitoa mfano Kamishna Kafulila na kuongeza,

“Na huu ni ujumbe kwa Watanzania ambao wapo katika masuara ya biashara na uwekezaji kwamba kwenye masuala ya ubia hauhitaji kusubiri zabuni ya Serikali itangazwe ili uweze kupata fursa na badala yake wewe mwenyewe unaweza kuanzisha fursa. Kimsingi fursa inakuwepo,”.

Alieleza kuwa ili kuanzisha fursa hiyo ni kupeleka kusudio la kuwekeza katika eneo kulani ambalo mamlaka ya Serikali inaendesha tofauti na maono yako kwa lengo la kuleta ufanisi au ubora zaidi katika mradi husika.

“Kimsingi unaleta sasa kusudio la kuwekeza katika hilo eneo ambalo wewe umeona kwamba mamlaka fulani ya Serikali inavyoendesha jambo fulani, mimi ningeweza kuendesha vizuri zaidi kwa faida yangu kibiashara, kwa faida ya Serikali kwa maana ya kutoa huduma. Hivyo sasa unaleta kusudio la kuwekeza kwenye kituo cha Ubia, ukishaleta kituo kinaita Mamlaka ya Serikali pamoja na wewe na kisha unawasilisha dhana yako hiyo ambayo unataka kuileta kwenye eneo husika. Basi mchakato kutokea pale ukiwekwa sawa sawa na kuonekana inafaa unapata fursa ya kuwekeza kwa utaratibu huo wa ubia ambao umetokana na wewe kuanzisha fursa,” aliongeza Kamishna Kafulila.

Hivyo alibainisha kuwa Sekta Binafsi inaweza kuangalia maeneo mbalimbali, ambayo inaweza kuwekeza kwa ubia ana Serikali ikiwemo Sekta za elimu, maji, miundombinu ya barabara, afya na maeneo kadha wa kadha ambayo Sekta binafsi inaona kuna fursa ya kibiashara kama ikisimamia na kuleta faida kibiashara kwa msalhi yake yenyewe pamoja na Serikali.

Kafulila alibainisha njia ya tatu kuwa ni ile ambayo Mamlaka ya Serikali inahitaji huduma kwa haraka, ufumbuzi wa jambo fulani kwa haraka huku taratibu za kibajeti na za kimanunuzi zitachukua muda mrefu, hivyo mamlaka ya Serikali inaweza kuzungumza moja kwa moja na mwekezaji mwenye uwezo na wakaingia mkataba kutekeleza mradi husika.

“Kwahiyo Mamlaka ya Serikali inaleta tu taarifa kwa Kituo cha Ubia, kwa mfano inasema tuna shida labda ya majosho ya kuogeshea ng’ombe na tunaona bajeti inachelewa kutekeleza jambo hili na tunahitaji pengine ndani ya miezi michache ijayo tuwe tunakamilisha hili jambo na mahitaji haya ni ya haraka. Kwahiyo hii ni sifa ya mradi ambao unaweza kukafanywa kwa mazungumzo ya moja kwa moja kwa sababu kuna muwekezaji ambaye anauwezo wa kufanya kazi hii,” alifafanua Kafulila na kueleza,

“Huo ni mfano tu, lakini kila eneo ambalo mamlaka ya Serikali ina uhitaji wa huduma fulani kwa haraka inaweza mamlaka hiyo kuomba kufanya majadiliano na mwekezaji mwenye uwezo moja kwa moja bila utaratibu huu ambao unatumika kwa maana ya ule utaratibu wa upembuzi,”.

Alisema njia ya nne ni ile ambayo inaitwa ‘special arrangement’, kwa maana ya makubaliano maalumu au utaratibu maalumu ambao unafayika kama kuna aina fulani ya uwekezaji ambao Serikali inauhitaji huku kukiwa na kampuni binafsi yenye uwezo wa kuufanya, lakini utekelezaji wake unakwamishwa na taratibu za kisheria.

“Kwahiyo aina hiyo ya uwekezaji ina ruhusu kampuni binafsi na Mamlaka ya Serikali kutengeneza makubaliano nje ya sheria inayosimamia ubia. Hata hivyo utaratibu huo hufanikiwa baada ya Tume ya Mipango kuridhia kwamba mradi huo ni wa kimakakati na una mazingira maalumu, lakini pia ni lazima Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiridhishe na zaidi Baraza la Mawaziri liridhie,” alieleza Kamishna Kafulila.

Hata hivyo Kafulila alisema kuwa utaratibu huo hufanyika kwa miradi mikubwa na yenye unyeti wake kiasi cha kukubaliana kufumua baadhi ya vifungu vya kisheria ili kuuruhusu mradi kutekelezwa.

Kafulila alieleza kuwa mfumo huu wa ubia ni kwa faida ya pande tatu, faida kwa mwekezaji kwa maana ya kwamba anapata biashara, faida kwa Serikali kwa maana ya kwamba inafanikisha upatikanaji wa mradi bila kutumia kodi, kukopa, kwahiyo inaipa fursa Serikali kufanikisha mradi husika bila presha ya kodi na mkopo, lakini pia ni faida kwa umma kwani huduma inapatikana kwa wakati bila kusubiri utaratibu wa Serikali kukopa na kutumia kodi.

Aliongeza kuwa, zaidi mradi wa ubia unaendeshwa na kampuni binafsi ambayo inatengeneza faida na kulipa kodi.
IMG-20240917-WA0036(1).jpg
 
Kafulila namwona kama kiongozi anayetaka Uchumi wa Watanzania umilikiwe na wazawa japo sioni huo mwamko wa Watanzania,

Watanzania ni waoga,
Watanzania ni wabishi
Watanzania ni wajuaji,
Watanzania ni walalamishi

Sijui kama watajitokeza kuwekeza
 
Wakati tunaendelea na hizi so called PPP ni bora pia tukaangalia manufaa yake kwa marefu na mapana kwa manufaa ya mlipa Kodi...

Watanzania wanaweza kuwekeza kwenye majungu na kulalamika kama akina Mbowe na Tundu Lissu
 
Wakati tunaendelea na hizi so called PPP ni bora pia tukaangalia manufaa yake kwa marefu na mapana kwa manufaa ya mlipa Kodi...

Kila option ina challenges.

You just need to weigh.

Tunashauriwa kufanya wanachofanya wengine na sio wanachoandika au kushauri.

PPP is all about structuring.

Ukipatia structuring uta balance private vs public interest.
 
Kila option ina challenges.
We need to know the challenges na loopholes za upigaji hususan nchi ambayo imegubikwa na upigaji
You just need to weigh.
We need to weigh in...., something which we are not, tumegeuka madalali na wapiga promo bila kuelezea matatizo
Tunashauriwa kufanya wanachofanya wengine na sio wanachoandika au kushauri.
Ana kushauri nani ? Mtu mwenye busara anahitaji kuangalia kabla hajaenda anaangalia pro and cons sio sababu fulani kafanya na watu wanaoandika hawaandiki sababu tu kwamba wanashauri bali msomaji inabidi kuangalia kama kuna vivid evidences na precedence na kama vyote hivyo vipo utakuwa chizi kuacha kufuatilia
PPP is all about structuring.

Ukipatia structuring uta balance private vs public interest.
ndio hapo nimeweka article ya the other side of the story ya yaliyotokea
 
We need to know the challenges na loopholes za upigaji hususan nchi ambayo imegubikwa na upigaji

We need to weigh in something which we are not tumegeuka madalali na wapiga promo bila kuelezea matatizo

Ana kushauri nani ? Mtu mwenye busara anahitaji kuangalia kabla hajaenda anaangalia pro and cons sio sababu fulani kafanya na watu wanaonandika sababu sio tu kwamba wanashauri kama kuna vivid evidences na precedence utakuwa chizi kuacha kufuatilia

ndio hapo nimeweka article ya the other side of the story ya yaliyotokea
Public-private partnerships are arrangements between the public and private sectors that undertake and deliver projects to serve the public interest.

They aim to leverage the strengths and expertise of both sectors to achieve mutual benefits, combining public resources and the efficiency of the private sector.

These partnerships can vary, but they typically involve the financing, construction, operation, and maintenance of public infrastructure or the delivery of public services.

The public sector retains the responsibility for setting the policy objectives and ensuring the project's compliance with public interest considerations.

The private sector partner brings its specialized skills, technological capabilities, and financial resources to design, build, and manage the project. The risks and rewards of the project are shared between the two parties, often through a long-term contractual agreement.

PPPs can be applied to various types of projects. Some examples are transportation infrastructure, utilities, social infrastructure such as schools and prisons, and information technology systems.

PPP projects are contingent upon many factors that include the need for the expertise of the private sector, cost savings, potential revenue generation, and the complexity of the project.

The duration of PPP contracts can vary significantly and is contingent upon the nature of the project. Projects can be as short as two years but can span as long as several decades.

The lengthy contract periods are necessary because they provide the private sector partner with the opportunity to recoup their investments and generate reasonable returns.

The duration also allows the public sector to benefit from the private sector's expertise over an extended period and ensure the quality and sustainability of the infrastructure or services provided.

👆👆👆
Hebu pitia hii
 
===
Katika ukurasa wake wa X zamani tweeter Mkurugenzi mkuu wa Ubia nchini Bwana David Kafulila amewataka Watanzania hasa wazawa kuchangamkia fursa za uwekezaji kwa njia ya Ubia kati yao na Serikali.

Kafulila ametoa fursa hiyo ya watu kutuma maombi ya kuitaka miradi yoyote inayoendeshwa na Serikali kibiashara kama Stendi, Masoko, Chanjo kwa watu na mifugo, Vyoo vya kulipia, Maegesho ya magari, Viwanja vya michezo, Usafirishaji, Ujenzi wa shule, Hosteli, hospitali au miundombinu ya Barbara pamoja na miradi mingine mingi kulingana na halimshauri husika.

View attachment 3098218
View attachment 3098219
Kafulila namwona kama kiongozi anayetaka Uchumi wa Watanzania umilikiwe na wazawa japo sioni huo mwamko wa Watanzania,

Watanzania ni waoga,
Watanzania ni wabishi
Watanzania ni wajuaji,
Watanzania ni walalamishi

Sijui kama watajitokeza kuwekeza
Kuwekeza kwenye nchi Kama Tanzania ni risk Sana.
Uncertainty ni nyingi sana, watawala wengi wa Afrika hawatabiriki, Wala haijulikani kesho kitatokea Nini!

Risks ni nyingi Sana kwenye kuwekeza Tanzania
 
Public-private partnerships are arrangements between the public and private sectors that undertake and deliver projects to serve the public interest.

They aim to leverage the strengths and expertise of both sectors to achieve mutual benefits, combining public resources and the efficiency of the private sector.

These partnerships can vary, but they typically involve the financing, construction, operation, and maintenance of public infrastructure or the delivery of public services.

The public sector retains the responsibility for setting the policy objectives and ensuring the project's compliance with public interest considerations.

The private sector partner brings its specialized skills, technological capabilities, and financial resources to design, build, and manage the project. The risks and rewards of the project are shared between the two parties, often through a long-term contractual agreement.

PPPs can be applied to various types of projects. Some examples are transportation infrastructure, utilities, social infrastructure such as schools and prisons, and information technology systems.

PPP projects are contingent upon many factors that include the need for the expertise of the private sector, cost savings, potential revenue generation, and the complexity of the project.

The duration of PPP contracts can vary significantly and is contingent upon the nature of the project. Projects can be as short as two years but can span as long as several decades.

The lengthy contract periods are necessary because they provide the private sector partner with the opportunity to recoup their investments and generate reasonable returns.

The duration also allows the public sector to benefit from the private sector's expertise over an extended period and ensure the quality and sustainability of the infrastructure or services provided.

👆👆👆
Hebu pitia hii
Sasa wewe unaleta story za what it is theoretically mimi nimekupa article what has been going on all over the globe kwa kupitia mgongo wa PPP's na mwisho wa siku mlipa kodi kuingia mkenge..., ngoja nikupe dondoo
  • Although PPPs are often promoted as a solution for countries under fiscal constraints, the evidence suggests rather that they worsen fiscal problems. According to the EIB, the six countries which have made the greatest use of PPPs in recent years are Cyprus, Greece, Ireland, Portugal, Spain and the UK. Four of these are subject to ‘Troika’ rescue packages, and the other two – Spain and the UK – both face large fiscal problems. In both Portugal and Cyprus, the IMF/EU ‘troika’ packages have identified PPPs as a contributory cause of the countries’ fiscal problems, and required an audit and renegotiation of existing PPPs and a freeze on new PPPs. 11 (see case study) In Latin America, PPPs are also concentrated in very few countries. Brazil and Mexico account for 65 per cent of all PPPs; Colombia, Peru, and Chile account for a further 15 per cent.
  • A further danger is the recent effort by the World Bank,the G20, OECD and others to ‘financialize’ PPPs in order to access the trillions of dollars held by pension funds,insurance companies and other institutional investors.
  • PPPs originated as an accounting trick, a way round the government’s own constraints on public borrowing. This remains the overwhelming attraction for governments and international institutions. Just as companies like Enron had tried to conceal their true liabilities by moving them‘off-balance-sheet’, so governments started using PPPs as “tricks…. whereby public accounts imitate the creative accounting of some companies in the past.”
  • “In developing countries, the development banks and multinational companies encouraged the spread of PPPs in the 1990s, especially in the water and energy sectors, as part of the general promotion of privatisation – and as a way around the fiscal limits which the same IFIs were imposing on developing countries. The main form of privatisation in water was concessions or lease contracts, which are a classic form of PPP.”
  • Governments have also started providing subsidies for PPPs, mainly by lending public money at low rates of interest that the private sector could not otherwise obtain – despite the obvious intrinsic contradiction of using public finance to finance PPPs.
 
Kuwekeza kwenye nchi Kama Tanzania ni risk Sana.
Uncertainty ni nyingi sana, watawala wengi wa Afrika hawatabiriki, Wala haijulikani kesho kitatokea Nini!

Risks ni nyingi Sana kwenye kuwekeza Tanzania
Ukipewa option ya PPP wala wewe mwekezaji hauna shida mkuu hii ni serikali mambo yakienda belly up serikali itakomboa through mlipa kodi (na hapo kumbuka ruzuku nje nje)
 
Ukipewa option ya PPPT wala wewe mwekezaji hauna shida mkuu hii ni serikali mambo yakienda belly up serikali itakomboa through mlipa kodi (na hapo kumbuka ruzuku nje nje)
Mimi nadhani tusikatishane tamaa, Nchi Kibao zimefanikiwa kujenga chumi imara kupitia PPP,
 
Mimi nadhani tusikatishane tamaa, Nchi Kibao zimefanikiwa kujenga chumi imara kupitia PPP,
Katika pesa za UMMA hatuhitaji kubahatisha na ukweli ni kwamba PPP's kuna loopholes nyingi za upigaji na mara nyingi anayefaidika without loss ni mwekezaji na mlipa kodi ndio anayebeba mzigo..., ni rahisi sana cheki hio article nchi ngapi zimeingia mkenge..., Kama kweli kitu kinalipa kwanini wawekezaji wasiingie mazima mazima kwa pesa zao 100 percent..., kwenye mambo mengine sawa sio mbaya ikifanyika partnership ila ndio hivyo kuna loopholes za upigaji
 
Siwamesema Sheria imewekwa sawa?
Wewe kama mwekezaji its the best opportunity nenda tu mkuu una back up ya serikali (kodi za mwananchi) nothing to lose... hata mambo yakienda ndivyo sivyo partner wako atatoa pesa.., Ila kama mlipa Kodi inabidi tufanye uchunguzi zaidi na kuwe na transparency 100 percent (jambo ambalo huwa sio, kuna a lot of kufichaficha)
 
Kwa Nini unajikita zaidi kwenye neno "kama mambo yatakwenda sawa"

Swali, Kwanini yasiende sawa?
 
Kwa Nini unajikita zaidi kwenye neno "kama mambo yatakwenda sawa"

Swali, Kwanini yasiende sawa?
It's the law of nature Shit Happens..., na kila ukifanya kitu huwa kuna percentage ya mambo kwenda ndivyo sivyo..., sasa nimekwambia kabia achana tu na mambo kutokwenda sawa PPPs inaleta loopholes za pesa ya mlipa kodi kuliwa soma tu hio article niliyokuwekea uone the other side of the coin..., hata unapochuma Roses sio vibaya ukajua pia kwamba kuna miba hivyo kujitayarisha kwa kuvaa gloves (unless wewe ni mwekezaji na sio mlipa kodi) basi hizi precautions hazikuhusu....
 
Back
Top Bottom