Kafumaniwa

Kafumaniwa

Maty

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2010
Posts
2,167
Reaction score
727
Habari zenu wana Jf,

nimepata kisa cha kusikitisha muda si mrefu na nimeamua nikiweke hapa jamvini kinaweza kutusaidia katika kufanya maamuzi yakikukuta.

Kuna mkaka namfahamu yeye ni mume wa mtu na amefumaniwa na mke wa mtu. Inasemekana mume wa huyo mdada mwizi na mke wa mkaka mwizi walishagundua na kukaa pamoja kuelezana kwamba wenza wetu wanafanya uzinzi. Wakakubaliana kuwafumania na kweli siku ya siku fumanizi likafanikiwa walichofanya ni kumpiga yule mwanaume sana hasa hasa kichwani mpaka damu imevilia kichwani na habari nilizopata hivi punde ni kuwa huyo kaka anapumulia oxygen machine once ikitolewa roho na mwili vinaachana.

Tupeane mawazo ikitokea ukamfumania mkeo/mumeo uamuzi mzuri ni upi? au walichfanya hawa mke na mume waibiwa kumpiga huyu baba mpaka kuwa hivi ni sawa?
 
vipi kuhusu mama maana kuna watuhumiwa wawili hapo au mme tu ndo aliadhibiwa.
 
huyo mke nawe kichaa kweli........akapigwa mume wake then mke wa yule mume akaachwa......hahaha..........sasa mumewe anapumulia mashine na kama damu imevia ndani ana 0.000912% za kuishi.........

hawa wawili wanaweza kurudiana.....

kweli tamaa mbaya
 
mmmmh mbaya sana Mungu amsaidie apone ili afanye toba!!!!!!!!!
 
Wasijekuwa WAFUMANIZI nao wanatafuta opportunity ya KUCHAKACHUANA..............
 
Nakama walikubaliana kwa nini alipigwa mmoja??Kwanza jua mpaka wanakaa wanakubaliana na wao walishafanya uzinzi!!ila kupigwa huyu labda alikuwa mkaidi!!ila ukimfumania mke kama unakifua nenda kwani unawezakumpiga mtu akazima wewe ukaishia Segerea na mkeo wakaendelea kumtimba kamakawaida!!Faida ikowapi??Mwache aendezake ujue huyo ajakupenda japo mnaishi au mwambie nimekusamehe njoo tulee watoto!!
 
mume wa mwanamke mwizi na mke wa mwanaume mwizi wlipanga huu mtego kama nimekusoma vizuri, huyu mwanamke wa huyo mwanaume mwizi alipatia wapi muda wakupuuzi hivyo wa kupanga yote hayo badala ya ku deal na mume wake?...anyway...cku zote mie ya kwangu ni yangu, ningekuwa mie ni huyo dada hata kupanga mambinu ya kijinga hivi nicngekuwa na muda nayo, ninge deal na mhucka wangu mwenyewe....
 
Kwenye hii kesi kuna watuhumiwa wawili what about the other(Mwanamke). Iweje wakubaliane kumpiga huyu mwanaume mpaka yuko kwenye hati hati ya kupoteza maisha sasa ina maana huyo mwanamke mke wa mtu ambaye naye kafumaniwa hana kosa??.....There is something fishy here
 
Mwanamke naye alistahili kichapo. Fumanizi huwa silifagilii huwa nashangaa sana watu wanavyoandaa namna ya kumfumania mpenzi wako ili iweje, upige? kithibitisho?
 
Habari zenu wana Jf,

nimepata kisa cha kusikitisha muda si mrefu na nimeamua nikiweke hapa jamvini kinaweza kutusaidia katika kufanya maamuzi yakikukuta.

Kuna mkaka namfahamu yeye ni mume wa mtu na amefumaniwa na mke wa mtu. Inasemekana mume wa huyo mdada mwizi na mke wa mkaka mwizi walishagundua na kukaa pamoja kuelezana kwamba wenza wetu wanafanya uzinzi. Wakakubaliana kuwafumania na kweli siku ya siku fumanizi likafanikiwa walichofanya ni kumpiga yule mwanaume sana hasa hasa kichwani mpaka damu imevilia kichwani na habari nilizopata hivi punde ni kuwa huyo kaka anapumulia oxygen machine once ikitolewa roho na mwili vinaachana.

Tupeane mawazo ikitokea ukamfumania mkeo/mumeo uamuzi mzuri ni upi? au walichfanya hawa mke na mume waibiwa kumpiga huyu baba mpaka kuwa hivi ni sawa?

Namwombea huyo kaka afariki dunia ili sheria ichukue mkondo wake kwa hao walio mshushia kipigo
 
yani hao waliofumania nao hawajalana tu bado?? au ndio kunya anye kuku??:bored:
 
Mwanamke naye alistahili kichapo. Fumanizi huwa silifagilii huwa nashangaa sana watu wanavyoandaa namna ya kumfumania mpenzi wako ili iweje, upige? kithibitisho?

Lengo kubwa nikumdhalilisha tu hakuna jingine
 
Namwombea huyo kaka afariki dunia ili sheria ichukue mkondo wake kwa hao walio mshushia kipigo
yeah right, vipi kuhusu watoto kama wapo? wateseke bila wazazi sio?
 
Mwanamke naye alistahili kichapo. Fumanizi huwa silifagilii huwa nashangaa sana watu wanavyoandaa namna ya kumfumania mpenzi wako ili iweje, upige? kithibitisho?
fumanizi lina raha yake mazee.. ushaona sura za waliofumaniwa zinavyokua??? khe khe heheheheeeeeeeeee....:tape:
 
mume wa mwanamke mwizi na mke wa mwanaume mwizi wlipanga huu mtego kama nimekusoma vizuri, huyu mwanamke wa huyo mwanaume mwizi alipatia wapi muda wakupuuzi hivyo wa kupanga yote hayo badala ya ku deal na mume wake?...anyway...cku zote mie ya kwangu ni yangu, ningekuwa mie ni huyo dada hata kupanga mambinu ya kijinga hivi nicngekuwa na muda nayo, ninge deal na mhucka wangu mwenyewe....
Nyamayao hata mimi napatwa na wasiwasi dada yangu isije ikawa hawa nao wanakamchezo kao nyuma ya pazia
 
Huyo mwanamke wa huyo kaka aliyepigwa hana akili timamu,
Yani anaona mume wake anauliwa anashangalia? Na kusaidia kuua.....
Hiyo sio roho ya mwanamke bwana.

Sasa kama mume wake atakufa atabaki bila mume, na huyo mwanaume aliyemsaidia kuua atabaki na mke wake.
Kafanya nini sasa hapo?
 
Kwenye hii kesi kuna watuhumiwa wawili what about the other(Mwanamke). Iweje wakubaliane kumpiga huyu mwanaume mpaka yuko kwenye hati hati ya kupoteza maisha sasa ina maana huyo mwanamke mke wa mtu ambaye naye kafumaniwa hana kosa??.....There is something fishy here

mie nipo kwa huyu mwanamke aliemtwanga mumewe kihivyo? kweli kuna mwanamke ana akili ya kumchangia mume wake na mwanaume mwingine mpaka wamuumize kihivyo?...swali lingine labda Maty atuambie je huyo mwanamke aliefumaniwa alitimua au nae alikuwa anaangalia wrestling inavyoendelea?
 
yani hao waliofumania nao hawajalana tu bado?? au ndio kunya anye kuku??:bored:
Ahaaa ahaaa nina wasiwasi mpaka wamefikia hatua ya kupanga fumanizi si ajabu tayari hawa
 
Back
Top Bottom