Kufumania kunauma sana, lakin pia kumpiga huyo mwanaume siyo suluhisho la tatizo zaidi ni kuongeza tatizo kwa huyo mwenye mume. Ajue kuwa yeye anauguza mume (na bora apone,akifa unaambulia ujane), wakati wenzake wanaombana msamaha na maisha yanaendelea kwao.
Ukimfumania mke/mume usipigane na uliyemfumania nae, cha kufanya hakikisha kuwa wanakuona ili watambue kuwa unajua wanachofanya halafu rudi nyumbani . Atakaporudi mke /mume nyumbani ndipo umwuulize nini sababu ya yeye kufanya hivyo mtatafuta njia ya kumaliza tatizo lenu.
Mi naamini kupitia fumanizi unaweza kujifunza kitu au jambo laweza kuwa baya au zuri na likawa msaada ktk mahusiano yenu.
Narudia na nasisitiza kufumania kunauma sana sana sana sana sana. Ukiwa kwenye mahusiano na haujawahi kufumania mwambie mungu asante sana.
Binadamu tunaishi kwa kujifunza, haijalishi kama hilo jambo ni baya au zuri, lililo muhimu ni kujifunza.