Adrianinho
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 426
- 522
Huyu jamaa nimemshangaa sana nimeisoma sana historia ya Thomas Sankara jinsi alivosalitiwa mpaka kupinduliwa hatimae kuuwawa na rafiki yake kipenzi wa tangu utotoni Compaore.Burkina Faso na Rwanda wapi wapi wakati hata Kijiografia tu ziko mbali mno. Siku zingine hakikisheni mnapokuja Kuanzisha Mada hapa basi Vichwani mwenu ama Gongo au Bangi mlizotumia ziwe hazijawazidi Kipimo. Kuna Watu wengine huwa mnajidhalilisha na kuonyesha waziwazi jinsi mlivyo Watupu Vichwani.
Kwa kukusaidia tu hasa kwa nchi za Afrika zetu hizi Mipango mingi ya Kimapinduzi hufanywa na Watu ama walio ndani au walio nje ya nchi husika ila iliyo na ukaribu wa Kijiografia lakini ni ngumu leo hii Rais au Mwana Mapinduzi wa Botswana akasababisha Machafuko / Mapigano nchini Chad.
Vitu vingine wala havihitaji Akili Kubwa kuvijua ila najua dhamira yako Kuu hapa ni Kumdhalilisha na Kuzidi Kuonyesha na Kuwaaminisha Wana JamiiForums kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ni Mtu mbaya sana wakati hata hapa nchini Kwako una Watu / Viongozi pengine wabaya na makatili kuliko huyo Kagame. Na najua wapo Watu watakuamini kwa haya Madai yako japo najua baadhi wenye Akili timamu na zilizotukuka watakupuuza tu.
Sijui ni Mtanzania gani aliyewapeni Sumu hii Kali Watanzania ya Kumchukia hivi Rais wa Rwanda Paul Kagame na Wanyarwanda wote hasa hasa wa Kabila la Watutsi ( Tutsi ) wakati hakuna nchi na Watu wanaowapenda Watanzania na Kuwaheshimu kama Rwanda na Wanyarwanda. Na leo niwahakikishieni tu kuwa Rais Paul Kagame hayuko hivyo kama ambavyo Watanzania wengi ( siyo Wote ) mmelishwa ' Propaganda ' mbaya dhidi yake ambayo mmeiendeleza hadi kwa Wanyarwanda wenyewe. Watanzania mnapendwa na kuheshimiwa sana na Wanyarwanda kuliko ambavyo mnajua.
Sasa hii habari ya Kagame kuhusika sijui kaitoa wapi.
Inawezekana kachanganya majina na huyu Sankara aliejifanya anakaribia kupindua utawala wa Kagame, mwisho wa siku kakamatwa kama kuku huko Comoro.