Kagame asema kuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya amani DR Cong

Kagame asema kuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya amani DR Cong

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kuwa kuna fursa ya kufikia makubaliano ya amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kuongeza kuwa mzozo katika nchi hiyo unasababishwa na msukumo kutoka nje.

Akizungumza katika kikao na wanahabari, Kagame amesema kuwa hatua zozote za kutatua mzozo unaoendelea huko DR Congo ni lazima zijumuishe suala la FDLR.

Vile vile, Kagame aligusia juhudi za utafutaji amani za rais wa Marekani Donald Trump na kuongeza kuwa ni muhimu kwa kwa kila nchi kutekeleza wajibu wake kahakikisha ufikiaji wa amani.

"Rwanda inaunga mkono juhudi na maamuzi ya Trump kuhusu mgogoro wa DRC," alisema Kagame.

"Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo unahusisha pande tatu, kisiasa, kiuchumi na msukumo wa nje," Kagame alisema.

Kagame ametoa hakikisha la kutimiza wajibu wake katika makubaliano lakini akaongeza kuwa utekeleza wa makubaliano yoyote ni jukumu la serikali ya DR Congo.
 
Akizungumza katika kikao na wanahabari, Kagame amesema kuwa hatua zozote za kutatua mzozo unaoendelea huko DR Congo ni lazima zijumuishe suala la FDLR.
Jeshi la Rwanda limeshindwa kuwamaliza Fdlr huko Drc tangu mwaka 1996, kipi kinamuaminisha Kagame hilo litawezekana sasa kwa kuendelea kutumia nguvu huku akikataa kuzungumza nao?

zitto junior JokaKuu
 
Kama watamuwachia Kagame aendelee kupora mali ya DRC hapana shaka amani itapatikana.

Lakini ukweli Kagame ni clever sana aisay, anachukua mali kutoka nchi zingine anapeleka kwake. Sio hao viongozi wengine wajinga wanachukua kwao,kupeleka USA au Europe, afu badaye wanazichukua hao USA na Europe wakati wananchi wao wanakufa njaa
 
Jeshi la Rwanda limeshindwa kuwamaliza Fdlr huko Drc tangu mwaka 1996, kipi kinamuaminisha Kagame hilo litawezekana sasa kwa kuendelea kutumia nguvu huku akikataa kuzungumza nao?

zitto junior JokaKuu

..DRC ni shamba la bibi.

..Marekani, DRC, na Rwanda, wamekubaliana namna ya kugawana mali za DRC.
 
Back
Top Bottom