Kagame Cup, Dar es Salaam-Tanzania 2015 Special thread!

83' Mins | Adama City 0 - Azam FC 5

Kipre Tchetche 7', 19' (Azam FC)
Mussa 33' (Azam FC)
Yahaya Mudathir 47' (Azam FC)
Ambrosse Pen 71' (Azam FC)
 
90' Mins | Adama City 0 - Azam FC 5

Kipre Tchetche 7', 19' (Azam FC)
Mussa 33' (Azam FC)
Yahaya Mudathir 47' (Azam FC)
Ambrosse Pen 71' (Azam FC)
 
FULL TIME | Adama City 0 - Azam FC 5

Kipre Tchetche 7', 19' (Azam FC)
Mussa 33' (Azam FC)
Yahaya Mudathir 47' (Azam FC)
Ambrosse Pen 71' (Azam FC)
 
Hatua ya makundi ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kukamilika leo jumapili kwa michezo miwili kupigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio ya wapenzi wa soka yakiwa katika mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya Khartoum ya Sudan.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10 kamili jioni, ambapo Yanga SC watashuka dimbani kusaka ushindi wake wa tatu mfululizo katika michuano hiyo, hali kadhalika timu ya Khartoum ikihitaji ushindi wake wa tatu katika mechi hiyo inayosuburiwa kwa hamu kubwa.

Kuelekea katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa vuta ni kuvute kufuatia timu ya Yanga SC kuhitaji ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuongoza kundi lake, huku pia Khartoum wakihitaji ushindi katika mchezo huo ili kuweza kuongoza kundi A.

Utamu wa mchezo huo unaletwa na makocha wa timu hizo mbili, Hans Van der Pluijm wa Yanga na James Kwesi Appiah wa Khartoum ambao wote wamewahi kufanya kazi nchini Ghana kwa vipindi tofauti.

Hans ambaye ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania msimu huu, anasifika kwa kucheza soka safi la kasi na kushambulia muda wote, huku akiwa na mafanikiko nchini Ghana baada ya kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ya Berekum Chelsea miaka miwili iliyopita.

Kwa upande wa James Appiah alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana, ambapo alikua kocha wa kwanza mwafrika kuipeleka timu ya Afrika katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Brazil mwaka 2014.

nifah, Makoye Matale, yahoo, b5-click, cnjona, Deo Corleone, youngsharo,
 
Last edited by a moderator:
Mpira umeanza kwa kasi sana. Hawa khartoum wazuri sana na dakika hizi za mwanzo wameonyesha makali yao.
 
Barthez anaokoa goli hapa. Dah tulikuwa tumeshalala. Dalili si nzuri upande wetu.
 
Another attempt kutoka kwa khartoum wanatukosa na attempt zote on target. Beki yetu ovyo sana.
 
Msuva gemu dakika hizi za kwanza mpira umemkataa sana. Tambwe anafanya madudu hapa
 
Kuna kituo chochote cha redio kinatangaza mtanange huu.
 
YANGA: Barthez, Zutta Joseph, Oscar Joshua, Kelvin, Pasco Ngonyani, mbuyu twite, msuva, niyonzima, tambwe, malimi busungu, coutinho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…