Kagame Cup, Dar es Salaam-Tanzania 2015 Special thread!

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Donald Ngoma amelambwa kadi nyekundu.Ngoma amepigwa kadi hiyo baada ya kumsukuma beki wa Gor Mahia ambaye alipanda kwenye mguu wake katika dakika ya 24 ya mchezo.



Mechi hiyo ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame inaendelea sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Tukio hilo lilionyesha kumuudhi Ngoma raia wa Zimbabwe aliyekuwa na kadi ya njano tayari, akamsukuma na mwamuzi akampa kadi nyingine ya njano na kuwa nyekundu.

Ngoma alijikuta akiangua kilio baada ya kutolewa nje . Hadi sasa Yanga ina bao moja kama ilivyo kwa Gor Mahia ambayo ilisawazisha katika dakika ya 24 kupitia Shakava.
 
Timu hizo zinakwenda mapumziko baada ya Yanga kutangulia kupata bao baada ya beki wa Gor kujifunga lakini wakasawazisha kupitia Harun Shakava katika dakika ya 16.
 
Baada ya kuondoa timu za mchangani, mashindano yatakuwa na ushindani mwaka huu
 
Wakuu hii mechi hakuna station inayoonyesha.!
 
Inaonyesha Ngoma anapanikishwa kirahisi uwanjani
 
Magufuli kaogopa kuzomewa, hajatokea uwanjani badala yake kaja raila odinga...,.ukawa wamemtishia nyau na kaogopa kweli hahahahaha

Bila shaka amewashitukia TFF kuwa kuna kundi la wadandia lift tu wanaotafuta jinsi ya kunyoosha mambo yao kiulanilaini.

Vv
 
Yani mimi Nataka yangu ishinde Lakini sioni uwezekano tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…