isee hii Nchi kweli imeuzwa.
Hivi mashindano makubwa kama haya Nchi ina Tv Stations kibaoo zenye uwezo mkubwa tu wanaenda kuwauzia mashindano wa South Africa?
TFF kweli wao ni Pesa tu na sio kuendeleza soka.
TFF ifaham kwamba Team Zetu zinawapenzi weengi saana mikoani,na wengine hata ukiwatajia DSTV ndio nini hawajui,wao wanajua Station za ndani tu.
Angalua wangeonyeshwa mechi hizi zingefunika machungu ya Team yetu kibonde ya Taifa.
TFF walivyo wanafiki ila kwenye hela wanakuwa waungwana.Kabla ya AZAM kudhamini Ligi Kuu,Supersport miaka mingi walikuwa wanaomba kuionyesha ila wakawa wanabania,na hii inaoneakana kwamba mkono wa AZAM ulikuwa unatambaa chinichini wanajua wao.
Leo hii Mechi hii inachezwa ndani ya Nchi na wananchi hao hao ndio Tunalipia Kodi TBC ili hadi vijijini watu waone mashindano makubwa kama haya eti wanawauzia Makaburu Supersport.
Na mbaya zaidi Supersport wakichukua haki miliki ni wao tu,wanapiga hela wanasepa.Halafu TFF mnasema mnataka kukuza Soka.
Maana vilabu imekuwa ni chaka na Watu kupiga hela,TFF nao kumeingia genge la wapiga helaa.
SIMBA OYEEEEE,bora mlivyojitoa,maana najua hao TFF na Super Sport walijua watapiga hela ndefu mkiwepo nyie
Subirini mechi zinazofuata kama wataona watu uwanjani