Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,442
- 4,388
Kigali. Rais Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya leo wataongoza mkutano wa kibiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaojumuisha wafanyabiashara maarufu katika jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa siku mbili utafanyika Kigali nchini Rwanda na marais hao wanatarajiwa kutoa maoni yao jinsi gani serikali na wafanyabiashara wanaweza kuungana na kuleta maendeleo.
Maoni hayo watayatoa katika mjadala utakaoongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya KCB, Joshua Oigara.
"Kama ukiangalia uzito wa mabadiliko katika miundombinu, tehama, nishati, sera na ulinzi, viongozi hawa tayari wameshaweka mpango wa jinsi gani ya kuyafanikisha.
"Tunachotafuta ni njia rahisi ya kufanikisha malengo waliyoyaweka katika biashara na pia tungependa kuona jumuiko zuri la kufanikisha malengo haya," alisema Oigara.
Mkutano huo pia utazungumzia maendeleo ya biashara, kodi na sera mbalimbali katika jumuiya ikiwa ni pamoja na sera za kazi zitakazoruhusu kutengeneza nafasi za kazi katika jumuiya hiyo.
"Jumuiya imepata maendeleo makubwa katika eneo la uwekezaji mpya kwenye miundombinu ya nishati na usafirishaji ambayo itapunguza gharama ya ufanyaji biashara," alisema Linus Gitahi ambaye ni mwenyekiti wa mkutano huo na pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group, (NMG).
Chanzo: Gazeti la Mwananchi