Kagame na Kenyatta kuongoza mkutano wa kibiashara EAC

Kagame na Kenyatta kuongoza mkutano wa kibiashara EAC

Ki Mun

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
3,442
Reaction score
4,388
Kigali. Rais Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya leo wataongoza mkutano wa kibiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaojumuisha wafanyabiashara maarufu katika jumuiya hiyo.

Mkutano huo wa siku mbili utafanyika Kigali nchini Rwanda na marais hao wanatarajiwa kutoa maoni yao jinsi gani serikali na wafanyabiashara wanaweza kuungana na kuleta maendeleo.

Maoni hayo watayatoa katika mjadala utakaoongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya KCB, Joshua Oigara.

"Kama ukiangalia uzito wa mabadiliko katika miundombinu, tehama, nishati, sera na ulinzi, viongozi hawa tayari wameshaweka mpango wa jinsi gani ya kuyafanikisha.

"Tunachotafuta ni njia rahisi ya kufanikisha malengo waliyoyaweka katika biashara na pia tungependa kuona jumuiko zuri la kufanikisha malengo haya," alisema Oigara.

Mkutano huo pia utazungumzia maendeleo ya biashara, kodi na sera mbalimbali katika jumuiya ikiwa ni pamoja na sera za kazi zitakazoruhusu kutengeneza nafasi za kazi katika jumuiya hiyo.

"Jumuiya imepata maendeleo makubwa katika eneo la uwekezaji mpya kwenye miundombinu ya nishati na usafirishaji ambayo itapunguza gharama ya ufanyaji biashara," alisema Linus Gitahi ambaye ni mwenyekiti wa mkutano huo na pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group, (NMG).

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Hawezi kumface kagame toka aongee vitu vya hovyo juu ya Rwanda. amebaki kukimbia kimbia tu.
 
Hahahahahaaaaaa! Watutsi utawajua tu kwa post zao. Hapo soon MAHORO atatinga mguu
 
Hili gazeti la Mwananchi ndilo linalotumiwa na akina Kagame kumchafua JK.
 
Hana hoja ya maana ya kiuchumi atakayoitoa katika mkutano huo, sasa wewe mtu hajui chanzo cha umaskini, yeye anaamini kuwa ana uwezo wa kutengeneza matajiri wakubwa nchini kwa kuwanyamazia waibe...poor presid.
 
Hivi wewe Brigedia huwa unashirikisha akili yako vema kabla ya kupost? Yaani nikisoma comments zako huwa napata kinyaa kweli!
 
Kama Mkutano unafanyikia kigali inawezekana ndo maana hajaenda,

Kagame hakaribishi wala rushwa kuitia najsi nchi yake.
 
Hao akina Kenyatta wanapiga soga tu. hakuna litakalowezekana kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki bila ya uwepo wa Tanzania
Nakubaliana na wewe dada. Uhai wa EAC unategemea ushiriki wa Tanzania
 
Kama Mkutano unafanyikia kigali inawezekana ndo maana hajaenda,

Kagame hakaribishi wala rushwa kuitia najsi nchi yake.
Kagame ndo mla Rushwa nambari moja Afrika. Tena ni muuaji wa upinzani. Tanzania tushukuru kuwa na kiongozi kama JK. Akina Slaa, Mbowe, Lissu nk wangekuwa Rwanda mpaka sasa tungekuwa tumewazika siku nyingi
 
Hivi wewe Brigedia huwa unashirikisha akili yako vema kabla ya kupost? Yaani nikisoma comments zako huwa napata kinyaa kweli!

Unapata kinyaa kwa sababu mimi natumia IQ kujibu na ku-comment...Tangu lini IQ ndogo ikaielewa IQ kubwa?
 
Kagame ndo mla Rushwa nambari moja Afrika. Tena ni muuaji wa upinzani. Tanzania tushukuru kuwa na kiongozi kama JK. Akina Slaa, Mbowe, Lissu nk wangekuwa Rwanda mpaka sasa tungekuwa tumewazika siku nyingi

Hivi mwangosi aliuliwa na nani?
 
Wacha waendelee bana. Sisi tujifariji na u sleeping giant wetu kila siku kujivunia milima,mito, mbuga, gesi sijui nini wakati wenzetu wanajipanga. Si tunajigamba na rasilimali lakini kutwa kuomba misaada.
Wenzetu wanaamua kujikwamua kwa nguvu zao sisi tunategemea za nje sababu hatuwezi na tunajiwekea vikwazo kuwa wawekezaji wakubwa ndani ya nchi yetu wenyewe.
Tunaendelea kujidanganya EAC haiwezi bila sisi, wakati sisi ndio waoga kufa kujiunga kwa sababu tunajijua mapungufu yetu ila hatuyakubali na hivyo kamwe hatuwezi kuyarekebisha.
Utasikia oo mbona makampuni ya nje yanaajiri wakenya tu sana sana. Ooo tukikubali EAC watakuja wakenya na warwanda kuvamia ardhi yetu! Sasa kama sisi tunashindwa kujiendeleza si ndio itakua matokeo yenyewe hayo.
Tunaendekeza siasa wenzetu wanakomalia elimu na maendeleo ya kiuchumi. Sisi tunaleta div 5, kufaulisha ambao hata hawapo darasani achana na ambao hawajui kusoma.

Badala ya kuona na kukubali mapungufu ili tujipange kama taifa tunafikiri kwa kukataa tu kwa nguvu basi itakua kweli. Dah nchi yangu aisee.
Rwanda huyo katoka juzi tu kwenye vita ila sasa hivi mrwanda atakua mtu wa maana na kuheshimika duniani kuliko mtanzania. Ila haina shida, kwanza hawana mbuga, gesi, mafuta mito na mabonde kama sisi!
 
Siasa za CCM zimetuharibu kuliko wengi tunavyotambua. Na hii 2015, bila kuweka siasa pembeni na kuchagua kiongozi anaefaa tutaula wachua kwa miaka 10 mengine. We only have 1 shot not to be left behind for good na kuendelea kujisifia rasilimali ambazo hata manyani waporini wanaweza kujisifia kuwa nayo kwasababu haihitaji akili yeyote kuwa na machimbo ya madini, gesi, mafuta, mbuga na milima. Kuendelea kujivunia hivyo vitu karne hii ya 21 na wakati havitupi faida wananchi ni kuwa na akili sawa na tumbili!
 
Hao akina Kenyatta wanapiga soga tu. hakuna litakalowezekana kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki bila ya uwepo wa Tanzania

Ndivo mnavofikiri siyo?Wenzetu wako serious na shughuli za uchumi wa nchi zao,mswahili wetu na wapambe wake wanapiga tu majungu ya urais 2015,PITY
 
Back
Top Bottom