Mbalamwezi1
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 2,073
- 2,026
Wadau tupeane uzoefu wa utumiaji wa mafuta ktk magari tunayotumia! Mimi naendesha gari aina ya Toyota Succeed(TX G Package) ina CC 1496 ya mwaka 2003. Kiukweli haka kagari nimetokea kukapenda hasa ktk ubebaji wa mizigo na matumizi ya mafuta kulingana na shughuli zangu! Ujazo wa tank la mafuta ni lita 50 huwa nasafiri nayo sana dar-dom(kama km 450 hivi), sasa nikiweka full tank dar kwenda dom nakuta nafika dom na nusu tank inabaki!! Kwa mimi naona ni nafuu sn kwangu ukichukulia mwanzoni nilikuwa natumia gx100 MarkII Grande! Ebu tupeane uzoefu wa matumizi ya mafuta hasa kwa sisi wenye vigari vidogo(baby walker type)Nimeambatisha na picha ya geji ya mafuta!