Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,904
- 1,064
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Bukoba mjini jana amewaijia juu wale wanaolalamikia kupanda kwa bei za vitu na kupanda kwa gharama za maisha katika miaka mitano.
Akihutubia katika mkutano wa kampeni katika kata ya Kagondo na huku akisikika moja kwa moja katika redio ya Kasibante FM anayoimiliki, Kagasheki aliwaambia wananchi wa kata hiyo wakati akimnadi mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya ccm Amani kuwa wasiwasikilize wanaolalamikia upandaji wa bei vitu wala gharama za maisha.
Kagasheki aliwambia wananchi waliokuwa wakimsikiliza kuwa kupanda bei kwa vitu ni kitu cha kawaida na si kitu cha ajabu kwa kuwa vitu haviwezi kubaki katika bei ile ile miaka yote na upandaji wa vitu bei unatokana na mfumuko wa bei.
Aliwataka watu wawadharau watu wote wanaolamikia upandaji wa bei na upandaji mkubwa wa gharama za maisha kama watu wasio kuwa na hoja na wawanyime kura kwa sababu hilo si suala la maana.