Rutunga,
Mko sahihi kabisa kuwa na mashaka ya uwepo wa Bagenda kwenye jukwaa la kagasheki. Binafsi nafahamu kwa undani urafiki ambao hivi karibuni uliingia kwenye hali ya uadui baada ya Prof. Tibaijuka kuombwa na kisha kutaka kutangaza nia kupitia jimbo la BK-Mjini. Jambo hili si kwamba lilimwewesesha kagasheki bali lilienda mbali zaidi na kujenga chuki dhidi yake na Prof na timu yake yote akiwemo Bagenda. kagasheki alikwenda mbali zaidi kuimarisha chuki hii hata baada ya Prof kuhamishia majeshi Muleba kwa Masilingi. Imethibitika kwamba kagasheki alichangia kwa mali na fedha lukuki kuhakikisha Masilingi anambwaga Prof. Na engine ya Prof; Bagenda ikalishinda hilo. Hivyo, uhusiano uliopo kati yao wote ni wa kinafki