Elections 2010 Kagasheki kugombea au kutogombea tena 2010?



Hivi haya maneno ya "wananchi" bado tunaridhika naye au ni "wewe" as individua unaridhika nayel! Dont generalize and reach a conclusion on national issues William!Unanikumbusha kuanzishwa vyama vingi wakati it was said that "wananchi hawataki vyama vingi"!Hizi slogan bado zipo tu!
 
Nadhani sote hatujasahau, ni kweli alisema hatagombea. Jikumbusheni kwa kutembelea link hapo chini:



Msekwa: Hakuna kustaafu

Mkuu nono shukrani kwa hii taarifa. Kweli huyu jamaa alisema hatagombea uSpika, na si kuwa alisema hatagombea Ubunge. Ubunge aliacha kugombea toka 2000, ina maana alikuwa Spika 2000-2005 lakini hakuwa mbunge, manake Spika si lazima awe Mbunge. Lakini wakati akiwa Spika 1995-2000 alikuwa pia Mbunge.
 
- Vipi ukiweka sababu za unafiki wa Mkuu William? Kuhusu Malecela sioni hoja, ya ahsante wewe huwezi kumuamulia what to write and what not to!

Respect.

FMEs!

Hizi IPs kidogo zinanichanganya!!!!
 


Nadhani yeye ni kiwakilishi cha wananchi.....76 years aendelee kuwa mbunge kwasababu huyo mzee ni chaguo la Mungu kwa wakazi wa Mtera duuuu thats very low! ni dharau kwa wale wapiga kura!
 
Mbunge wa Bukoba mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Sued Kagasheki amekanusha habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania Daima kuwa hatogombea tena ubunge maana ana kazi nyingi za kufanya.

Akiongea kupitia kituo anachokimiliki, Radio Kasilibambe FM ya Bukoba mjini. Kwa mbinde sana Kagasheki amedai kuwa hayo ni mambo ya kisiasa na kama angekuwa amefikia uamuzi huo watu wa kwanza kujua wangekuwa wapiga kura wake.
 
Kagasheki kama huna jipya kwa nini usipumzike?umeona ule umati wa Lwakatare??maana hata 2005 ulipita kwa taaabu sana sana ahadi zako zote bila bila unategemea ruzuku yako ili uje udanganye tena wapiga kura wako?sio wewe tu na wenzio woote waliotudanganya .....hadi sasa hakuna jipya akiwemo JK wenu huyooo...nae msaniii pia.
 
Kiti kitamu mwenyewe kachomowa muulizeni Zitto alivyo piga bonge la u turn ooh wazee wameniomba, sijui presha imekuwa kubwa na blah blah tele..
 
Haya funga funga uondoke kagasheki wameshakuchoka hao
 
kweli kijana kaishiwa hela ya kuchezea tena kwenye kampeni
 
unaganga njaa sasa kagasheki....na umepoteza mwelekeo
 
Aaaah Hii nchi mbona mambo ya ajabu ajabu tu kha we are tired sasa
 
Nadhani sote hatujasahau, ni kweli alisema hatagombea. Jikumbusheni kwa kutembelea link hapo chini:



Msekwa: Hakuna kustaafu

- Mkuu nono, ahsante sana eti source ya hii habari unayo mkuu uiweke hapa siikatai kwamba ni ya uongo inaweza kuwa kweli, ingawa ninajua kwamba Mtandao walimtaka aondoke kwa kumtumia ujumbe through Amina Chifupa akagoma kata kata kwamba haendi kokote, infact hata akamkimbilia Rais kumuuliza kama ni kweli hamtaki, sasa alikuwa anfanya tote haya huku ameshasema atatoka ndio nashindwa kuelewa!

FMES!
 

- Ni tathmini ya mwananchi anayelijua jimbo lake, kama tunavyotathimini hapa JF kila siku kwamba Kikwete atashinda tena bila ya matatizo, eti kwa kufanya hivyo tunawaamulia wananchi wote wa Tanzania how to vote, au kwa sababu sisi hapa JF tunaridhika naye basi wote wanaridhika naye?

- Think kabla ya kuandika mkuu! Maaan hata viongozi wengi wa upinzani wameamua kugombea ubunge kwa sababu wamesema urais hawauwezi, sasa na wao imekuwaje kuwaamulia wananchi kwamba watamchagua Kikwete na CCM? kwa mantiki yako, au?

FMES!
 

- Ahsante mkuu kwa hizi habari, nina washikaji wengi sana pale mjini Bukoba, na wengi wanasema ni wazi kwamba jamaa hawezi rudi tena hata akigombea, na hata kura za maoni hawezi pita, naona amechomoa lakini anajua kwamba hawezi kushinda tena!

FMES
 

- With all due respect mkuu, mimi binafsi sijawahi kusema kwamba nina nia ya kugombea ubunge popote pale, wala nia ya uognozi wa siasa, wananchi wa Mtera waaachiwe wajiamulie wenyewe nani wanayemtaka awaongoze.

- Sheria ni msumeno mkuu inasema nini kuhusu umri wa wabunge? Kama huyu mzee anaivunja nitakwua wa kwanza kumwambia, eti sheria inasema nini mkuu?

Ahsante

William.
 

Sijui na mzee Malecela anan'gatuka au anaendelea kung'ang'ania ili aendelee kuwa mpiga debe wa chama cha Majizi?
 
😱Kuna best wangu hapa naona maneno yake yanajirudia rudia kwenye thread nyingine baada ya nyingine. Tena anamjibia best wake mwingine na kumpa thanks. Hata hivyo ni kama vile ni yeye yule yule. Kazi ipo!😀
 
Kama gazeti limesema uongo basi na aende mahakamani na kulishitaki, hapo tutajua kweli ni uzushi. Vinginevyo atabaki na historia ileile ya kuwa alikuwa ana wa beep wapiga kura wake na cha moto kinamsubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…